Bastola iliyoua wawili Sinza ni dili kishirikina, lakini pengine pia imebeba mikosi na laana

Hawa ndiyo wanatufanya sasa hata kama ulitaka uongeze silaha ya pili nyumbani kwa ulinzi wa mali zako serikali inakupa masharti kibao.kama ulikasirika au umevamiwa kuna ile tukio la kwanza kama tahadhari huyo adui wako akuelewe unaimiliki piga juu.ya pili pia kama ameona kuna ile kama kujilinda kama tahadhari unapiga kwenye miguu tu.tatu kama alikuwa unaona na wewe maisha yako huyo mwengine ana silaha ndiyo kujiokoa ushamtahadharisha umepiga juu bado anakutafuta na silaha yake unamuwahi yeye kabla hajakuwahi ya moyo.ila huyu kaitumia silaha vibaya kwa hali zoote kwanza hao hawakuwa na silaha kama yake,ipo haja serikali ipitie upya sheria za umiliki wa silaha ili tusirudi kama mauaji ya marekani na south africa.Mambo haya tulishawahi kujadili toka zama za mkapa hapo silaha zitakapoanza kuuzwa dukani kama pipi.kwanza kuna kipengele chake unapoachiwa uimiliki huruhusiwi kwenda nayo club kama za pombe inatgemea uliiomba kama wewe ndiye mmiliki halali wa club.Huyu katuharibia ambao tunataka tumiliki silaha tena sana.Na hili litaongeaa kutubana upyaaaa.
 
Mshana kwa hiyo haya magari used ya Beforward na SBT ambayo sisi tukinunua tunaita gari mpya tuachane nayo?
 
Mshana kwa hiyo haya magari used ya Beforward na SBT ambayo sisi tukinunua tunaita gari mpya tuachane nayo?
Hapana sijasema hivyo mimi mwenyewe natumia hayo hayo ila ziogope zile zilizopata ajali nje zinarekebishwa na kuja kuuzwa huku
. kuna gari baada tu ya kununuliwa zikaondoka na mmiliki au familia
. Zingine hazikufanikiwa kupata hata namba
.Zingine kila siku zinakula hela.. Ni matatizo mwanzo mwisho
. Zingine zimefanyika baraka zina miaka hazijawahi kuchunwa hata bumper
 
Mkuu silaha ni silaha tu, imepitia mikononi mwa mtu safi ama mtu katili ishaitwa silaha. Kwa namna yoyote (ukatili/ ulinzi) kama sio kuondoa uhai wa mtu basi itamwaga damu ya mtu.
Zipo silaha zimemwaga damu lakini hazijaondoka na roho na zimeokoa wasio na hatia na kama ni kuua zimeua wabaya wanaostahili kufa
 
Sasa mimi ntajuaje hili gari lina laana na hili halina?
 
Mpe masikini kileo asahau shida zake kwa muda ila tajiri na wafalme uamuzi wao hauta kuwa wa hekima. Pombe mbaya.
Napingana nawe kwenye ubaya wa pombe...pombe sio mbaya kama mtumiaji anajitambua.. Kuna watu wamenenewa vibaya na pombe hao haiwafai. Kuna malimbukeni kuna waigaji kuna wataka sifa ... Wote hao haiwafai
 
Vipi kuhusu nguo za mitumba? % 68 tz ndio viwalo vyetu, ufafanuzi ndugu Jr.
Inategemea huko ilikotoka ilikuwa na historia gani.. Nyingi hazina shida ila kama iligusa damu ya mfu shida ipo
 
Napingana nawe kwenye ubaya wa pombe...pombe sio mbaya kama mtumiaji anajitambua.. Kuna watu wamenenewa vibaya na pombe hao haiwafai. Kuna malimbukeni kuna waigaji kuna wataka sifa ... Wote hao haiwafai
Nipe maandiko yanayo sifia pombe hasa yanayo toka katika vitabu takatifu.
 
Ndio maana nikasema tunaponunua vitu lazima tuvifanyie ibada ya kuvitakasa kwa imani zetu.. Hata kukitolea sadaka ya shukrani pia inasaidia
Imani zingine ni potofu hazina nguvu. Tuswalie hivyo hivyo hata kama hazileti impact?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…