Bastola iliyoua wawili Sinza ni dili kishirikina, lakini pengine pia imebeba mikosi na laana

Napingana nawe kwenye ubaya wa pombe...pombe sio mbaya kama mtumiaji anajitambua.. Kuna watu wamenenewa vibaya na pombe hao haiwafai. Kuna malimbukeni kuna waigaji kuna wataka sifa ... Wote hao haiwafai
Kweli kabisa maana nna miaka 30 na kitu nakida pombe,tatizo kuna vitabia mtu ukiwa navyo alafu ukichanganya na mtungi lazima itakupelekesha

Ova
 
Aise kweli kabisa
Umenikumbusha kile kisa cha yule
Prof wa udsm alikuwa anasafisha silaha yake
Hapo hapo ikamtandika mwenyewe

Ova
 
Bastola kama haijakuua basi utaua wengine hata kwa bahati mbaya. Na ukishaua mtu huwezi kuwa sawa sawa tena. Sishauri kabjsa kama Sio mtu wa ulinzi na usalama. Ishi vyema na watu, epuka wizi wizi, na ubishi ubishi usio na msingi, usiweke bifu na watu. Asilimia 80 yetu ni mania Bipolar , akiwa kwenye moody, atafanya kisha kujuta. Wengi wetu ni machizi wasomi so be careful[emoji1545][emoji817][emoji736][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Mmh kuna kilichokuwa kinamtafuta kumbe
ukipita maeneo hayo kila mtu anastory zake sema ndo hivyo
marehemu hasemwi vibaya,ila serikali iangalie tu sana vijana wengi sana sinza wana [emoji379][emoji379].

mie last week nilikuwa nadrive mbele yangu kulikuwa na crown jamaa kila nikimpigia horn hasogei baada ya kupiga horn kama dakika 5 nzma jamaa akashuka na paip,nilivyoona tu anaichomoa nikarukia mlngo wa nyuma nkafngua mlango fasta nkakimbia zangu. dogo alikuwa yank around 32years

serikali inabidi iangalie sana kwenye kutoa hvi vibal vya kumiliki silaha
 
Silaha hii nimeitumia kama kiwakilishi tu cha kuelezea tafsiri za kiroho kwenye matukio kama hayo.. Na zaidi nimeandika mengi nje ya hiyo silaha naona hukuyaona, hukuyazingatia au hukuyaelewa
Nimewahi pia kusoma makala kuwa Aridhi za Rwanda na Burundi zitakuja kupokea Roho za mauaji tena kwa sababu historia yao tangu kale ipo hivyo. Unasemaje hapo?
 
Mkuu, asante kwa mtazamo wako wa kiroho.

Pia kuna mtazamo wa kishirikina. Watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ana sifa ya ukorofi, majivuno na ubabe, na mwingine mmpole, mstaarabu na asiyependa makuu.

Nina mashaka mmiliki alizidisha manjonjo wakati anaizindua Baa kivingine "NEW ...." Tusubiri kushuhudia wateja wakiongezeka kwenye hiyo baa.

Ni mtazamo wangu tu
 
Nimewahi pia kusoma makala kuwa Aridhi za Rwanda na Burundi zitakuja kupokea Roho za mauaji tena kwa sababu historia yao tangu kale ipo hivyo. Unasemaje hapo?
Yeah.. There is always a come back.. Kuna roho zimelala kule bado zinatafuta kisasi
 
Sahihi kabisa komrade si ajabu nyuma ya pazia kafara la damu lilihitajika sana hapo na limepatikana tayari
 
Brother yupo pouwa kabisa.
Mimi nimemuelewa vizuri, wewe bado..
Hajasema kwamba tukio Hilo limesababishwa na ushirikiano, Bali , baada ya tukio Hilo, ile silaha iloyotumika ni dili, kishirikina. Tena amejaribu kutoa mfano jinsi ambavyo thamani ya silaha iliyowahi kuua Ni kubwa kuliko ile isiyoua bado.
Sasa haya matabaka ya thamani ya hizi silaha hayawezi kuwepo pasipo kuwepo na wazo la kishirikina.
Ndiyo maana kasema hiyo silaha itatafutwa kwa udi na uvumba , yote ni kwa sababu za kishirikina ambazo zinaamini kuwa thamani yasilaha hiyo ipo juu..
 
Hizi nong'ono kitaani ya kuwa mziba pancha alikuwa anaziba pancha ya my wife wa jamaa lina ukweli ndugu mchambuzi?...hebu liangalie katika vyombo vyako.
Kila kifo huja na mengi..huwa na mengi... Ni kati ya hayo mengine yote moja tu huwa la hakika
 
[emoji736][emoji817][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…