Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha (A-Town/Chuga)

[emoji1787] we jamaa umekuja mji wa watu kwa nini usituulize sisi wenyeji tukupe location mimi niko mwanza kesho weekend nitafute
Mwanza ni Mji rahisi sana kuuelewa,Barabara 3 Mji umeisha 🤣🤣..

Na ulivyo shaghalabaghala hata hauvutii mumeuharibu wenyewe Kwa ujenzi holela..

Arusha na Dom zimeiacha Mwanza mbali sana ni vile mko supported na watu wengi ila zaidi ya hapo hamna kitu..

Mwanza ni nzuri City Centre tuu kwingine kote ni tia maji tia maji..

Kasi ya ujenzi Kwa Sasa inaridhisha tofauti na kipindi naondoka japo tatizo ndio Hilo ujenzi holela na pia hakuna ujenzi wa majengo marefu..

Arusha
 
We jamaa ulivyo mjinga unalitembea jiji ukiwa kwenye hice

Unataka nini sema tukusaidie
 
Hili jengo la taasisi ndio linakutoa ushamba, leta ghorofa 10f la arusha ambalo ni la mtu binafsi, Mwanza ina majengo yaliyojengwa na wazawa na si misaada ya mashirika ya taasisi, na arusha ni makao makuu ya EA lakini bado ni jiji tia maji tia maji halina maajabu.
 
Usishindane na Arusha kwenye majengo hutoweza.Siku nyingi sijaenda Arusha hope next year nitaenda pia..

Arusha Iko hot kama Dar usilete mchezo Mzee..

Niliweka kambi maeneo ya Kirumba pale Fimbo Hotel,pale Viwanja vya Furahisha Kuna Ujenzi mkubwa sana unaendelea bila shaka litakuwa jengo kubwa but sio refu ,pia nimeona TBA pia wanajenga kando ya Barabara ya Airport jirani na lile jengo jipya la Hotel ambalo mikdle Huwa anaposti Kila siku 😀😀..

Ila kiukweli Mwanza imebadilika ,miaka 8 ni Mingi nadhani by 2020 itaungana kabisa na Misungwi nimeona ujenzi uko speed upande huo wa Shinyanga Road but shida ni Ile Ile Kwa nini hayo maeneo hampimi viwanja kuwe na proper ujenzi?
 
Ndio maaana nakuita mshamba maendeleo ya jiji hauwezi kuyaona hapo barabarani

Ilemela,pansiasi,ghana hadi mjini hayo ni maeneo ya zamani kelele nyingi kama unataka maeneo mazuri sana ambako matajiri wanaishi sema tukupe locations na kama bado upo mwanza sema kesho mimi kesho nitakutembeza kwa usafiri wangu

Mwanza imekua sana ila sio pansiasi [emoji3][emoji3]
 
Umetembelea maeneo gani kiongoz?
 
We unawauma watu wa arusha na kuwapuliza waambie ukweli kuwa wana safari ya miaka 100 kufika mahali mwanza ilipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…