Kwa Mara ya kwanza nimefika Arusha, jiji ambalo kwa miaka mingi nimetamani sana kufika bila mafanikio.
Jiji lipo busy sana kuanzia alfajiri watu ni wengi asubuhi, magari kibao.
Tofauti na mwanza hizo hamsha hamsha zipo lakini hazifikii za arusha.
Miji yote miwili hekaheka zao zote zinakata kuanzia mida ya saa mbili usiku. Arusha utaona magari mengi mtaani ila watu hakuna mtaani.
Ukitoka Arusha city center kilomita 10 kila upande, mji unakua umeuacha na hutaona maeneo mengine yaliyochangamka zaidi. Tofauti na Mwanza ambako kuna miji mingine kama nyegezi buhongwa, kisesa, igoma na buswelu ambako kunawafu wengi sana na nyumba ni nyingi mno.
Kwa upande wa barabara, Arusha imejitahidi. Mwanza bado kuona mikeka kama ya kanda ya kaskazini.
Kwa kumalizia, jiji la Mwanza ni kubwa na limepangika. Magholofa yanayopendezesha mji yamekusanyika pamoja na mengine ndio yanaendelea kutawanyika mbali na city center.
Arusha inamagholofa mengi na marefu sana na mazuri zaidi kuliko ya mwanza, lakini yapo mbalimbali.
Nakadhalika na kadhalika.
Miji yote ni mizuri sana kama serikali ikiamua kujenga miundo mbinu kama Dara. Nadhani tunaweza kua na majiji matano tu yanayoshikiria vyema taswira ya nchi yetu