Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha (A-Town/Chuga)

Ukubwa wenye uhovyo na umaskini ndani yake unatusaidia nini?

Uzuri upi ambao Mwanza inao kushinda Arusha? Barabara zipi hizo? Mimi Mwanza na Arusha kote nafahamu siambiwi.
Wivu utakuua, mitaa ya ovyo ya Mwanza ni ile ya miliman kama kule mabatini na igogo au sahara kwa juu, mitaa yote iliyotambarare imepangwa na imepitiwa kwa barabara za lami, hata huko juu kuna mitandao ya barabara za mawe na sewage system nzuri sana ambayo ilipelekea wakenya kuja kujifunza, Arusha jiji haiwez kuizidi Mwanza jiji kwa mtandao wa barabara za lami, au kwa vile tunalilia sana barabara mkajua kweli hakuna barabara, Ilemela peke ake inatosha kubattle na Arusha kwenye upande wa barabara za lami zenye viwango, me sina mengi lakini cha kuongeza Ilemela peke yake inapiga chini Arusha kwenye poshy neighbourhood.
 
Ukubwa wenye uhovyo na umaskini ndani yake unatusaidia nini?

Uzuri upi ambao Mwanza inao kushinda Arusha? Barabara zipi hizo? Mimi Mwanza na Arusha kote nafahamu siambiwi.
Taja barabara za arusha na urefu wake nikutajie za jiji la Mwanza, arusha nimeishi miaka miwili huko hakuna kitu ambacho wataishinda Mwanza labda sector ya utalii tu.
 
Mwanza yote ni hovyo na slums Kila sehemu hata huko Capripoint ni hovyo tuu na Kuna Nuka shombo ya Samaki Mji mzima.

Nilienda kule mnajenga DIT Kuna Nuka hatari Sasa sijui wale wanafunzi wataishije pale 😁😁
 
Unaongolea Capripoint kama unaongelea matundu ya vyoo, huko kunashindana na Masaki na Oysterbay tu kwa nchi hii ya Tanzania.
 
Kusoma hujui na picha huoni?
Weka picha niweke kila barabara kilometa na jina la barabara nitaanza za ilemela kwanza, nataka kukuambia kuwa Mwanza ni dude kubwa sana linalotisha sema ndo hivyo linanyimwa miradi lakini acha tuendelee kulijenga zaidi kwa nguvu zetu.
 
Utakuwa umekosea
 
Mwanza yote ni hovyo na slums Kila sehemu hata huko Capripoint ni hovyo tuu na Kuna Nuka shombo ya Samaki Mji mzima.

Nilienda kule mnajenga DIT Kuna Nuka hatari Sasa sijui wale wanafunzi wataishije pale 😁😁
Ukiombwa picha za slum kila mara unaleta ile picha yako ya Igogo, huna sera huna hoja, kila mji mkubwa haukosi kuwa na sehemu za watu maskini hata kule Jo' berg kuna slum za kufa mtu.
 
Ukiombwa picha za slum kila mara unaleta ile picha yako ya Igogo, huna sera huna hoja, kila mji mkubwa haukosi kuwa na sehemu za watu maskini hata kule Jo' berg kuna slum za kufa mtu.
Mwanza yote ni uswazi usituchoshe bana Kila mtu anajua hili.
 
Mwanza hii yenye miradi mikubwa ya kimkakati ya kuinua uchumi ije kushindanishwa na vimji vinavyotegemea ngedere kama soko lao la kuongeza kipato

Mwanza yenye SGR,
Mwanza yenye meli kubwa za mizigo na abiria,
Mwanza yenye daraja kubwa la JPM Africa mashariki na kati,
Mwanza iliyopakana na majiji makubwa ya Africa,
Mwanza yenye ziwa victoria,
Mwanza yenye mgodi mkubwa wa Nyanzaga,
Mwanza yenye viwanda,
Mwanza yenye utalii wa kitabibu,
Kuna mambo mengi nachoka kuandika😝
 
Ukiombwa picha za slum kila mara unaleta ile picha yako ya Igogo, huna sera huna hoja, kila mji mkubwa haukosi kuwa na sehemu za watu maskini hata kule Jo' berg kuna slum za kufa mtu.
Nimeambiwa stand ya buzuruga imehamishiwa nyamhongoro Tena imejegwa kisasa na inavutia mno.. Arusha mpaka muda huu hawana stand za maanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…