Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha (A-Town/Chuga)

Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha (A-Town/Chuga)

haahaahaahaa! yaan useme Arusha hawana maneno maneno? we jamaa kiboko, mall gan iyo kubwa iliyopo Arusha watu wasiijue ndugu yangu? yaan kuwe na mall kubwa tanzania nzima watu wa hapo Arusha wasijue kama kuna mall? kitanzania mall ni mliman city & rock cith ndio mall ambazo hata ukimuamsha mtu usingizin anakutajia....na ndio maana nimekuuliza we unaiongelea mwanza ya miaka gan? kama umefika siku za hv karibun huwezi ifananisha Arusha na Mwanza kaka huenda labda we unaongelea ki lifestyle tu sababu Arusha starehe zimezid lakin ki mjin mwanza mjin sana na sio ilemela tu mwanza ni mzin zaidi ya Arusha....kama ni majengo marefu mwanza mjin ni ghorofa tupu hakuna nyumba za chini
Unapoteza muda kubishana na watu wanaowaza kwa kutumia msaada wa bhangi, pia kitu ambacho sipendi ni kuifananisha Mwanza city na Arusha, kiukweli bila unafiki Arusha ina safari ya miaka 100 kufika mahali Mwanza ilipo.
 
Kimapato ni kati ya Mwanza na Arusha wapi pako juu.
Unapoteza muda kubishana na watu wanaowaza kwa kutumia msaada wa bhangi, pia kitu ambacho sipendi ni kuifananisha Mwanza city na Arusha, kiukweli bila unafiki Arusha ina safari ya miaka 100 kufika mahali Mwanza ilipo.
 
Ok, Mwanza mjini yani Ilemela, pia bado hapana maajabu ya kupafananisha na Arusha. Ukisema eti Mwanza ilitangulia kutambuliwa kama jiji, hio sio issue , population size ilibeba na pia politics. Maana ata Arusha wamewatangulia karibu kila kitu. Kwanzia magari, magorofa ya lifti, supermarkets, malls, majumba ya maana, you name it. Exposure nk nk. Na ndio maana hapo Mwanza matajiri kutoka Arusha ndio wamepajanjarusha. Alafu kila kijana wa Mwanza akiamia Arusha hataki kurudi kwao , nimeiona mara nyingi sana. na wana acknowledge mwanza bado sana.

Kimapato ni kati ya Mwanza na Arusha wapi pako juu.
Mwanza haijawahi kushuka nafasi ya pili baada ya dar
 
Nani hajapata jibu?

Mwanza sio ya kuilinganisha na vimji vya ajabu ajabu kama Arusha.

Mwanza inakimbizana na Dar kwenye kila kitu, miundombinu, mapato, wingi wa watu, uchangamfu, starehe, watoto wazuri, vyuo, nk. Muwe mnasoma hata takwimu/taarifa za serikali zinatolewa kila mara kuonyesha Mwanza is untouchable.

Arusha ilinganisheni na Kahama ama Musoma sio Mwanza ni kuivunjia heshima Mwanza.
Au wailinganishe na Katoro!
 
Chugastan is my HOME ila when it comes to comparison nadhani labda tulinganishe Misitu (uoto wa asili) ndio Arusha itaishinda MWANZA.

The rest MWANZA iko palee juuu,pesa ni nnje nnje,Nyomi la maana,Maendeleo ndio shkamooo yake..

inshort Mwanza iachwe pale.. Arusha isifiwe kwa u KIJANI tu.
 
Chugastan is my HOME ila when it comes to comparison nadhani labda tulinganishe Misitu (uoto wa asili) ndio Arusha itaishinda MWANZA.

The rest MWANZA iko palee juuu,pesa ni nnje nnje,Nyomi la maana,Maendeleo ndio shkamooo yake..

inshort Mwanza iachwe pale.. Arusha isifiwe kwa u KIJANI tu.
safiiii! yaan kwakweli hata mm ninavyoiona Mwanza infact ni untouchable.......Arusha jiji kweli ila sio la kuifananisha na Mwanza no matter Arusha ni mji wa bata sana
 
Huwezi kunidanganya lolote kuhusu mwanza...naifahamu mwanza mwanzo mwisho..nimeingia mwanza mwaka 1999....mwanza ni mji wa matukio..matajiri wa mwanza 50% ni majambazi wa kutumia siraha..uvuvi na madini wengi wao wamejificha huko....maisha ya mwanza ni ya hovyoo..japo wenyewe wanakuambia ni mepesi.....
Eti matajiri wa Mwanza ni majambazi na Arusha tusemeje sasa!
 
ndio maana nikauliza " mwanza unayoiongelea wewe mwanza ipi? sasa wewe unaongelea mwanza ya miaka 23 iliyopita hata haijapandishwa hadhi ya kuwa jiji! sasa kama mwanza ya mwaka 1999 ilikuwa vile ulivyoiona je! arusha ya mwaka huo nayo ilikuwaje? na ndio maana nikasema tuongelee current na sio miaka zaid ya 23 iliyopita. sasa angalia 1999 mpaka sasa tunaelekea 2022 ni miaka mingapi imepita?
 
Eti matajiri wa Mwanza ni majambazi na Arusha tusemeje sasa!
wakazi wa mwanza kwakweli ni wakarimu sana , hawana makuu kwa maana ya lwamba sio watu wa kujikweza wapo very simple, unakuta don yupo simple tu town hapa lakini ukiulizia habar zake hatar, sio kitu cha ajabu kuskia ana migodi yake, ana ghorofa zake 10 mjin, ana meli 10 zinabeba shehena tu mwanza - uganda, ana ferry kibao zinavusha abiria wa mwanza sengerema , ukerewe nk, ana ngombe 3000, ana mialo yakutosha ya kuvulia samaki, tata 60 zinafanya safar za town trip, bus 100 za mikoani, malori 300 yapo barabaran nk halafu unakuta hana hata mbwembwe msukuma wa watu katulia tu, sasa ingekuwa mchaga hapo hatar akiwa na duka tu akina shirima watamkoma ..... kwaiyo hiyo ndio mwanza bhana matajir kama hao kibao na hawana mbwembwe. MWANZA UNTOUCHABLE
 
hapo umetuuza bhana mdaz kusema kwa bata hata dar haiingii kwa chuga....kama umefika dar bas huwez linganisha bata la dar na mji wowote hapa bongo....tutakuwa tunadanganyana ...dar itabaki kuwa dar na wala hatuhitaji kuiongelea hapa sababu dar ndio tz
usimpinge sana huenda labda hajawahi kufika dar......maana wengine dar wanaiskia tu bomban, sitaki kuamin kama mtu alishawahi kufika dar halafu aje aifananishe dar na jiji lolote hapa tanzania labda hilo jiji litashinda kwa hali ya hewa .....dar haifananishwi na mji wowote bongo hapa zaid ya kushindanishwa na Nairobi na Mwanza wanaifananosha na Mombasa
 
Kumekuwa na sintofahamu kati ya Majiji haya mawaili yanatotikisa Tanzania ukiachilia Dar.

Majiji haya yamezua gumzo miongoni mwa watu kwa kujaribu kuyashindanisha lakini pamoja na kuyashindanisha kote bado watu hawajapata jibu la moja kwa moja kwamba ni mji gani mzuri na una fursa kubwa za kimaisha kuliko mwingine pamoja na ukuaji wa maendeleo.

Karibuni mchangie
1: Majengo marefu,
Of course mwanaza ni nzuri na ina magorofa kizuri mm nimeishi miji hii yote miwili mwz na Arusha. Mwanza ina magorofa ndio lakini ukweli ni kwamba magorofa ya mwanza sio marefu kama ya Arusha yani Arusha mjini pale kweli bana magorofa marefu yamechomoza na bado mengi yanajengwa kwa hili mwanza bado sana.

2: Exposure ya watu,
Kwa hili kwakweli mwanza ni aibu, people are not exposed kabisa yani mwanza ushamba ni mwingi sana na hata tu kwakuwaona kimwonekano hata katika mazungumzo bado sana ni hii nikutokana na kuwa na idadi ndogo sana ya mchanganyiko wa watu kutoka mataifa tofauti na Arusha amboyo imejaa wageni ambao wengi wanatembelea jiji hilo na wengi wanafanya kazi katika jiji hilo na kushi kwakuwa Kuna uwekezaji mkubwa wa kimataifa, kumwona mzungu au kudate na mzungu,mwarabu,muhindi, n.k kwa Arusha ni jambo lakawaida sana lakini mwanza mtasubiri sana watu wa mwanza wenye exposure ni wachache Arusha watu wengi wanajichanganya na watu wa mataifa mengine kwasababu ndio uhalisia na maisha yalivyo kwaajili ya utalii na shughuli za kimataifa na ndo maana kuna 5* hotels mfano hapo mwanza je kuna hoteli wanalipa USD10,000$ per night ni hoteli gani kwa Arusha iyo ni Sheraton hotel iliyoko Serengeti na Usa River.

3: Elimu na Shule,
Hahaha hapa kwakweli mwanza kuweni wapole ukianza na vyuo vya kimataifa kwa Arusha Kuna Esami iliyojaa watu kutoka mataifa ya nje ikiwa mabara Europe,US, Africa etc na wakufunzi wa mataifa ya nje na hata wa Tanzania, pia kuna chuo cha Kimataifa Mandela sihitaji kuelezea rejea hapo juu. Tukija kwenye shule za msingi, Kuna Braebun International, Jaffery International, International school of Arusha na zingine sizikumbuki kwaiyo kwa hili bado mwanza mtasubiri

4: Biashara,
Kwahili hakika hapa naweza sema kuwa kibiashara mwanza ni rafiki sana mazingira ya biashara ni rahisi ikichangiwa na utitiri wa watu wengi hapa ndipo Arusha inakuwa ngumu maana hali ya maisha kwa Arusha yako juu sana yani nikiwa na maana ya kwamba Yale maisha ya kawaida sana yani kama ya kwa mrombo au uswahilini Arusha kwa mwanza ni kawaida sana ya huduma ndogo ndogo za kawaida hayo maisha mwanza hata mjini kati yapo yani access ya kupata vitu bei ndogo mwanza ni rahisi sana na hii inachangiwa na uwingi wa watu na mazingira rahisi ya biashara hapo kwa Arusha mwanza imeshinda.

5: Population,
Dah mwanza mnazaliana ama kweli mnakipaji ndo maana watu wengi mno yani huwa najuuliza hivi hamna kazi za kufanya licha ya kuzaliana Yani unaweza kuta mwanamke anawatoto 5 wamefatana kama ngazi. Hapo Arusha hawawafikii Mwanza.
6: Miundombinu ya barabara,
Hakika mwanza mko vizuri japo sio sana kweli mmejitahidi ila Arusha ya sasa kwa upande huo wa barabara Arusha wanakuja juu kwa kasi ya 6G yani ni noma nahapo mtaumia.

7: Standi kuu ya mabasi,
Mwanza mnastandi nzuri sana na Mara ya mwisho naona ilikuwa imefingwa kwaanjili ya ujenzi mko vizuri ila maumivu mtakayo yapata kwa standi ya kisasa inayojengwa Arusha maeneo ya bypass barabara ya Africa Mashariki itakuwa ni matusi makubwa sana yani kwa swala la standi kuu ya Arusha walaa msiongeee ujenzi uko on process.

8: Maeneo ya starehe,
Mwanza kuweni wapole maana hata holeli zenye suite ya dola elfu 10 au 5 kwa usiku mmoja hakuna kwaiyo mwanza kaeni kimya pia kuna hoteli Arusha maeneo ya USA River ambayo ina open space ya mashindano ya mpira wa farasi, pia kuna wanyama pori hapo hapo hotelini wanakuja moaka mlangoni wakiwemo swala, pundamili, na nyumbu hiyo ni mjini imagine unakunywa bia au wine alafu wanyama hao wako mbele yako pia ARUSHA NDO JIJI PEKEE KWA TANZANIA NA LAPILI EAST AFRICA KUWA NA MBUGA YA WANYAMA MJINI JAPO NI NJE KIDOGO INAITWA ARUSHA NATIONAL PARK AU MOMELA KWAAJILI YA ZIWA MOMELA sasa msidhani kuwa Arusha hakuna ziwa lipo linaitwa Momela na pia ndipo eneo litwalo Serengeti ndogo lilipo ndani ya mbuga hiyo.

SWALA LA HALI YA HEWA NI USHINDI USIOPINGIKA NA WW KAMA MJANJA JENGA CHUGA BADO OPPORTUNITY YA MAENEO IPO

MENGINE MKITAKA JUA TEMBELEENI ARUSHA AU IYO KIMJI CHA ARUSHA KAMA MNAVYOITA.
 
Vitu vilivyonivutia arusha

1.uwanja wa golf mkubwa na wa kisasa EA nzima kili golf club
2. Uwanja mkubwa wa mashindano ya farasi
3.uwanja mkubwa wa mashindano na michezo ya pikipiki
4.art gallery
5.kiwanda local cha bia aina ya twiga
6.mahakama ya africa
7.eneo pekee la zipline Tanzania
8.hotel nyingi za nyota 4 na 5
9.supermarket nyingi
10.apartment nyingi na airbnb nyingi kushinda hata dar
 
haahaahaahaa! yaan useme Arusha hawana maneno maneno? we jamaa kiboko, mall gan iyo kubwa iliyopo Arusha watu wasiijue ndugu yangu? yaan kuwe na mall kubwa tanzania nzima watu wa hapo Arusha wasijue kama kuna mall? kitanzania mall ni mliman city & rock cith ndio mall ambazo hata ukimuamsha mtu usingizin anakutajia....na ndio maana nimekuuliza we unaiongelea mwanza ya miaka gan? kama umefika siku za hv karibun huwezi ifananisha Arusha na Mwanza kaka huenda labda we unaongelea ki lifestyle tu sababu Arusha starehe zimezid lakin ki mjin mwanza mjin sana na sio ilemela tu mwanza ni mzin zaidi ya Arusha....kama ni majengo marefu mwanza mjin ni ghorofa tupu hakuna nyumba za chini
Wewe ndio huijui, mbona wanaojua wanajua, Mwanza 5 star hotel ni ipi? rock city mall ya juzi tu ndio maana watu wa mwanza kwa ushamba wao wanaona ni maajabu,mbona wanaongoza vitu kibao ni vile hawana promo. Shoprite ilikuwepo arusha, shoppers plaza ipo ila mwanza hakuna why? hujiulizi?
 
Vitu vilivyonivutia arusha

1.uwanja wa golf mkubwa na wa kisasa EA nzima kili golf club
2. Uwanja mkubwa wa mashindano ya farasi
3.uwanja mkubwa wa mashindano na michezo ya pikipiki
4.art gallery
5.kiwanda local cha bia aina ya twiga
6.mahakama ya africa
7.eneo pekee la zipline Tanzania
8.hotel nyingi za nyota 4 na 5
9.supermarket nyingi
10.apartment nyingi na airbnb nyingi kushinda hata dar
Na mambo mengi zaidi. Mwanza ni likijiji likubwa tu. Sijui nani anawadanganyaga kuna mtu anapaona mwanza kama ni mji wa maana yani. eti mtu ana dream kwenda kuishi na kufanya maisha mwanza. kwa kipi? huko warundikane hao walugaluga wa kanda hiyo wajipige kifua kuwa ndio jiji namba mbili lakini halina hadhi ya jiji. East Africa wala mwanza haitajwi. Arusha is respected internationally. We kuna rais gani wa marekani anaendaga mwanza akija tanzania?
 
Back
Top Bottom