Kumekuwa na sintofahamu kati ya Majiji haya mawaili yanatotikisa Tanzania ukiachilia Dar.
Majiji haya yamezua gumzo miongoni mwa watu kwa kujaribu kuyashindanisha lakini pamoja na kuyashindanisha kote bado watu hawajapata jibu la moja kwa moja kwamba ni mji gani mzuri na una fursa kubwa za kimaisha kuliko mwingine pamoja na ukuaji wa maendeleo.
Karibuni mchangie
1: Majengo marefu,
Of course mwanaza ni nzuri na ina magorofa kizuri mm nimeishi miji hii yote miwili mwz na Arusha. Mwanza ina magorofa ndio lakini ukweli ni kwamba magorofa ya mwanza sio marefu kama ya Arusha yani Arusha mjini pale kweli bana magorofa marefu yamechomoza na bado mengi yanajengwa kwa hili mwanza bado sana.
2: Exposure ya watu,
Kwa hili kwakweli mwanza ni aibu, people are not exposed kabisa yani mwanza ushamba ni mwingi sana na hata tu kwakuwaona kimwonekano hata katika mazungumzo bado sana ni hii nikutokana na kuwa na idadi ndogo sana ya mchanganyiko wa watu kutoka mataifa tofauti na Arusha amboyo imejaa wageni ambao wengi wanatembelea jiji hilo na wengi wanafanya kazi katika jiji hilo na kushi kwakuwa Kuna uwekezaji mkubwa wa kimataifa, kumwona mzungu au kudate na mzungu,mwarabu,muhindi, n.k kwa Arusha ni jambo lakawaida sana lakini mwanza mtasubiri sana watu wa mwanza wenye exposure ni wachache Arusha watu wengi wanajichanganya na watu wa mataifa mengine kwasababu ndio uhalisia na maisha yalivyo kwaajili ya utalii na shughuli za kimataifa na ndo maana kuna 5* hotels mfano hapo mwanza je kuna hoteli wanalipa USD10,000$ per night ni hoteli gani kwa Arusha iyo ni Sheraton hotel iliyoko Serengeti na Usa River.
3: Elimu na Shule,
Hahaha hapa kwakweli mwanza kuweni wapole ukianza na vyuo vya kimataifa kwa Arusha Kuna Esami iliyojaa watu kutoka mataifa ya nje ikiwa mabara Europe,US, Africa etc na wakufunzi wa mataifa ya nje na hata wa Tanzania, pia kuna chuo cha Kimataifa Mandela sihitaji kuelezea rejea hapo juu. Tukija kwenye shule za msingi, Kuna Braebun International, Jaffery International, International school of Arusha na zingine sizikumbuki kwaiyo kwa hili bado mwanza mtasubiri
4: Biashara,
Kwahili hakika hapa naweza sema kuwa kibiashara mwanza ni rafiki sana mazingira ya biashara ni rahisi ikichangiwa na utitiri wa watu wengi hapa ndipo Arusha inakuwa ngumu maana hali ya maisha kwa Arusha yako juu sana yani nikiwa na maana ya kwamba Yale maisha ya kawaida sana yani kama ya kwa mrombo au uswahilini Arusha kwa mwanza ni kawaida sana ya huduma ndogo ndogo za kawaida hayo maisha mwanza hata mjini kati yapo yani access ya kupata vitu bei ndogo mwanza ni rahisi sana na hii inachangiwa na uwingi wa watu na mazingira rahisi ya biashara hapo kwa Arusha mwanza imeshinda.
5: Population,
Dah mwanza mnazaliana ama kweli mnakipaji ndo maana watu wengi mno yani huwa najuuliza hivi hamna kazi za kufanya licha ya kuzaliana Yani unaweza kuta mwanamke anawatoto 5 wamefatana kama ngazi. Hapo Arusha hawawafikii Mwanza.
6: Miundombinu ya barabara,
Hakika mwanza mko vizuri japo sio sana kweli mmejitahidi ila Arusha ya sasa kwa upande huo wa barabara Arusha wanakuja juu kwa kasi ya 6G yani ni noma nahapo mtaumia.
7: Standi kuu ya mabasi,
Mwanza mnastandi nzuri sana na Mara ya mwisho naona ilikuwa imefingwa kwaanjili ya ujenzi mko vizuri ila maumivu mtakayo yapata kwa standi ya kisasa inayojengwa Arusha maeneo ya bypass barabara ya Africa Mashariki itakuwa ni matusi makubwa sana yani kwa swala la standi kuu ya Arusha walaa msiongeee ujenzi uko on process.
8: Maeneo ya starehe,
Mwanza kuweni wapole maana hata holeli zenye suite ya dola elfu 10 au 5 kwa usiku mmoja hakuna kwaiyo mwanza kaeni kimya pia kuna hoteli Arusha maeneo ya USA River ambayo ina open space ya mashindano ya mpira wa farasi, pia kuna wanyama pori hapo hapo hotelini wanakuja moaka mlangoni wakiwemo swala, pundamili, na nyumbu hiyo ni mjini imagine unakunywa bia au wine alafu wanyama hao wako mbele yako pia ARUSHA NDO JIJI PEKEE KWA TANZANIA NA LAPILI EAST AFRICA KUWA NA MBUGA YA WANYAMA MJINI JAPO NI NJE KIDOGO INAITWA ARUSHA NATIONAL PARK AU MOMELA KWAAJILI YA ZIWA MOMELA sasa msidhani kuwa Arusha hakuna ziwa lipo linaitwa Momela na pia ndipo eneo litwalo Serengeti ndogo lilipo ndani ya mbuga hiyo.
SWALA LA HALI YA HEWA NI USHINDI USIOPINGIKA NA WW KAMA MJANJA JENGA CHUGA BADO OPPORTUNITY YA MAENEO IPO
MENGINE MKITAKA JUA TEMBELEENI ARUSHA AU IYO KIMJI CHA ARUSHA KAMA MNAVYOITA.