Mi kwenye ugomvi wa Mwanza na Arusha naonaga humu kumejaa watoto tu ama mabishoo wasio na tija kwa sifa za kipuuzi tu, mimi ninaishi Mwanza mjini toka nimezaliwa, na ninafanya kazi Arusha mjini na viunga vyake toka 2009.
Ukweli mfupi ni kwamba Mwanza na mikoa yote ya Kanda ya ziwa ina watu wengi sana, maeneo matatu yalio viunga vya mji ni sawa na mikoa mingine mitatu kati kati ya jiji, nikimaanisha Buhongwa kutoka juu mpaka chini, Buswelu kuunganisha na Nyamhongolo, Igoma kuunganisha na Kishili, haya maeneo matatu kila eneo moja ni sawa na pale Shinyanga au Tabora au Kigoma hivi, sema humu ndani kumejaa mihemko tu, miji ya Kaskazini katika kaya moja unakuta mtu ana watoto watatu, Kanda ya ziwa kaya moja mtu ana watoto 9 mpaka 12, mji wa Mwanza unahudumia mikoa yote ya Kanda ya ziwa, japo mkoa mmoja wa Kagera unachanganya kimahitaji kati ya Mwanza na Kampala, watu wa mikoa hiyo mitano mikubwa ya usukumani, karibu 79% wamekimbilia pale Mwanza kibiashara , changanya na uzaaji watoto watu ni wengi sana, tena hata hao M3. 6 nadhani ni wachache