Battle ya Sativa vs ZCO Faustine Mafwele bado mbichi

Battle ya Sativa vs ZCO Faustine Mafwele bado mbichi

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Nitaweka mfulizo wa posts za Sativa kutoka kwenye ukurasa wake wa Twitter akimshutumu ZCO Faustine Mafwele kuwa ndiye kinara wa utekaji na uuaji unaotekelezwa na taasisi za Serikali dhidi ya wakosoaji/ wanaharakati wa siasa.

1. Namna alivyomtambua ZCO MAFWELE

Siku ya kwanza nimeongea story yangu public niliongea kwenye Club house. Ilikuwa 7/8 saa mbili kamili usiku.

Kwenye story yangu kuna mahali nilimtaja mtu mwenye sifa hizi hapo awali sikumjua kabisa kwa majina.

Sifa nilizozitaja;

1. Mrefu
2. Mweusi
3. Mwili wa ukakamavu (kama mtu wa mazoezi)
4. Ni kama mtu wa kanda ya Ziwa kimuonekano wake (watu wa Mwanza, geita, ukerewe).
5. Alivaa jezi ya simba (ya msimu uliopita nyekundu)
6. Alivaa bukta ya kaki.
7. Mkononi alikuwa na simu nyingi kama sio 2 basi 3.

Siku 20 baadae nikaja kuona picha za huyu jamaa hapo pichani alifahamika kwa jina la MAFWELE. Siku nimeiona hii picha nilitetemeka sanaa.

Niliogopa sana nikakumbuka mateso makali niliyopitishwa, nikarudia kuangalia hii picha nikakumbuka ni yeye aliekuja kituo cha polisi usiku ule OSTABAY.

Hapo hapo nikawatumia watu wangu wa karibu kuwa huyu mtu ndie alikuja usiku ule Obay na kutoa amri niwekwe pembeni aongee na wale mapolisi waliokuja kunikamata KOROGWE.

Hili jamaa ndio lilitaka nife, Huyu ndio anahisi yeye atafika 2099 hapa duniani.

Kama kweli jina lako ndio MAFWELE NKUAHIDI tutakuwa na safari ndefu mimi na wewe.🤝

Pia soma
 
Dah nimpe pole huyu jamaa kwa nyakati ngumu alizopitia sio jambo jepesi.

Sema hapa naona kuna kitu hakipo sawa kwake.Sijui kiasi gani amejipanga kumkabili huyu mtu lakini kwa hesabu nyepesi unaona battle anaweza shindwa tena

Angeweza angemwachia Mungu au kama anataka kuchukua njia za asili hakuwa na sababu ya kuparade hizi taarifa kizembe(labda ni kutoa ufahamu kwa wengine hili wajichunge kama ndio lengo basi sio vibaya lakini kama ni lengo la kupata huruma ya watz niseme hapa uongo kwani watanzania unafiki ni mwingi)
 
Katika Qur'an, hukumu ya Siku ya Kiama inatajwa kwa uwazi katika sehemu nyingi, ikiweka msisitizo wa matukio yatakayojiri na hali ya watu wakati huo. Siku ya Kiama inaitwa kwa majina tofauti kama "Yaumul Qiyama" (Siku ya Kusimama), "Yaumul Hisab" (Siku ya Hesabu), "Yaumul Fasl" (Siku ya Tofauti), na mengine mengi. Qur'an inaeleza kuwa siku hiyo itakuwa ni siku ya haki, ambapo kila nafsi itahukumiwa kwa matendo yake ya duniani.

Baadhi ya aya zinazozungumzia hukumu ya Siku ya Kiama ni:

1. Surat Az-Zalzalah (99:7-8):
- "Basi atakaye fanya wema wa chembe ya uzito wa chembe atauona. Na atakaye fanya ubaya wa chembe ya uzito wa chembe atauona."

Aya hii inasisitiza kuwa kila kitendo, kiwe kidogo au kikubwa, kitafikishwa kwa hesabu mbele ya Allah, na kila mtu atapata malipo au adhabu kwa matendo yake.

2. Surat Al-Qariah (101:6-9):
- "Ama ambaye mizani yake ya (mema) itakuwa nzito, basi huyo atakuwa katika maisha ya furaha. Na ambaye mizani yake ya (mema) itakuwa nyepesi, basi makao yake yatakuwa Hawiya (jahannamu)."

Hii inafafanua kuwa mizani ya matendo ndiyo itakayoamua hatima ya kila mtu, ama kuingia Peponi au Jahannamu.

3. Surat Al-Haaqqa (69:18-19):
- "Siku hiyo mtafikishwa (kwa Mola wenu) hamna kilichofichwa katika siri zenu. Basi yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia atasema: Haya! Sikilizeni msome kitabu changu!"
 
Back
Top Bottom