Battle ya Sativa vs ZCO Faustine Mafwele bado mbichi

Battle ya Sativa vs ZCO Faustine Mafwele bado mbichi

Nitaweka mfulizo wa posts za Sativa kutoka kwenye ukurasa wake wa Twitter akimshutumu ZCO Faustine Mafwele kuwa ndiye kinara wa utekaji na uuaji unaotekelezwa na taasisi za Serikali dhidi ya wakosoaji/ wanaharakati wa siasa.

1. Namna alivyomtambua ZCO MAFWELE

View: https://x.com/Sativa255/status/1833929192569790685?t=BVXlaYncA5lCPAmQwUV_tg&s=19

Mara nyingi nikiangalia picha ya huyu mtu, kwa jicho la tatu, huyu ameanza kutafunwa na nafsi yake. Damu alizomwaga ni nyingi sana. Hana raha ya kipato anachopata, watoto wake wanalipiwa kwa fedha ya damu za watu masomo yao hayana baraka ya Mungu. Mkewe akivaa akadhani kapendeza ni mavazi ya damu za watu.
Muuaji wa kwanza tangu ulimwengu kuumbwa alikuwa Kaini.
Baada ya Kaini kumuua Abel, Kaini alichimba shimo akamfukia, damu ya Abel ikamlilia Mungu, Mungu akasikia kilio cha Abel. Mungu akamuita Kaini, naye akaitika Mungu akamuuliza yu wapi Abel ndugu yako? Kaini akamjibu ovyo sana Mungu eti kwani mimi ni mlinzi wake?

Majibu ya ovyo ya Kaini kwa Mungu ni dailies ya kufadhaika kwa nafsi ya Kaini. Ndivyo wauaji wanavyofadhaika. Mwisho wataanza kuelezea kwa watu kuhusu maovu waliyotenda na kamwe haitasaidia.
 
Dah nimpe pole huyu jamaa kwa nyakati ngumu alizopitia sio jambo jepesi.

Sema hapa naona kuna kitu hakipo sawa kwake.Sijui kiasi gani amejipanga kumkabili huyu mtu lakini kwa hesabu nyepesi unaona battle anaweza shindwa tena

Angeweza angemwachia Mungu au kama anataka kuchukua njia za asili hakuwa na sababu ya kuparade hizi taarifa kizembe(laba ni kutoa ufahamu kwa wengine hili wajichunge kama ndio lengo basi sio vibaya lakini kama ni lengo la kupata huruma ya watz niseme hapa uongo kwani watanzania unafiki ni mwingi)
Last time wamemwachia Mungu nini kimetokew? More peoples wamezidi kupotea
 
Waliopachikwa jina wasiojulikana lakini wanaofahamika na Polisi ndiyo hawa.

12 September 2024

Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=5OPBbiE_dtI

Mgeni rasmi Naibu waziri mheshimiwa Daniel Baran Sillo (Mb.) akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi leo Septemba 12,2024 unaofanyika mkoani Kilimanjaro Tanzania .

Ally Senga Gugu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani , IGP C.M Wambura mkuu wa Jeshi la Polisi, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro na wakuu wa polisi wastaafu ni miongoni mwa waliuhudhuria mkutano huo.

Naibu waziri Sillo anatoa salamu za Waziri wa mambo ya ndani ameshindwa kuhudhuria mkutano huo kutokana na kutingwa na shughuli maalum, hivyo naibu waziri kumuwakilisha katika mkutano huu wa Maofisa wakuu waandamizi wa Polisi (senior officers conference) mwaka huu 2024.

Maadili na nidhamu ni muhimu ili kuweza kuwa waadiĺifu katika utendaji mzuri wa kazi na kuweza kuwasimamia walio chini yao

Mwaka jana 2023 mheshimiwa rais akifungua mkutano kama huu katika ukumbi wa Oysterbay Officer Mess jijini Dar es Salaam alisisitiza ushirikiano na kuhudumia umma wa watanzania.

Makamanda na maofisi mwaka huu jeshi la Polisi linatimiza miaka 60 tangu kuanza kuanzishwa mara baada ya Jamhuri ya Muungano kuanzishwa mwaka 1964 ...


Toka maktaba
2023 4 September

Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama anafungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam leo Septemba 04, 2023.
1726160267597.png

1726160319825.png




TOKA MAKTABA:

07 July 2024​

MHE. SILLO AHITIMISHA ZOEZI LA MAFUNZO YA UPANDISHWAJI VYEO CHUO CHA MAAFISA WA POLISI KIDATU​


1719903143.jpg


SILLO AHITIMISHA ZOEZI LA MAFUNZO YA UPANDISHWAJI VYEO CHUO CHA MAAFISA WA POLISI KIDATU
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo (Mb), amehitimisha zoezi la Mafunzo ya upandishwaji vyeo ya Uongozi Mdogo kwa Cheo cha Sajini Meja (SM) na Sajini Taji (S/SGT) wa Polisi Kozi Na. 1/2023/2024 katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Tanzania kilichopo Kidatu Mkoani Morogoro.

Akihutubia katika hafla hiyo Juni 28, 2024 Mhe. Sillo amesema kuwa, anatambua mafunzo yalikuwa ya muda mfupi lakini yenye mambo mengi muhimu yaliyofundishwa kwa njia ya nadharia na vitendo na mada zote zilifundishwa.

"Lengo ni moja tu kwamba mtakaporejea kwenye vituo vyenu vya kazi muweze kuwa mmepata ujuzi na mbinu za uongozi za kuwasaidia katika usimamizi wa majukumu ya kazi mtakayopangiwa. Ni vyema nichukue fursa hii kuwapongeza wakufunzi wote waliowezesha kukamilika kwa mafunzo haya kwa ufanisi kama ninavyojionea hapa, amesema nimeelezwa na Mkuu wa Chuo kuwa wakati wote wa mafunzo mmeonesha kuwa wenye nidhamu ya hali ya juu na mmejitolea kwa moyo wa dhati katika kushiriki kwenye vipindi vyote vya mafunzo bila kutegea vipindi" Alisema Mhe. Sillo

Pia amewataka wale wote ambao bado wanaendelea na vitendo vya ukiukwaji wa maadili waache mara moja na wabadilike kifikra ili waweze kuwatendea haki wananchi kwani dhamana waliyopewa katika nchi hii ni kubwa na vyeo hivyo viwasaidie katika kuwasimamia Askari wa chini ili nidhamu na uadilifu viimarike Jeshini katika kuepuka malalamiko hayo.

Mhe. Sillo pia amewaelekeza kuhakikisha wanadhibiti ajali za barabarani, Biashara Haramu za Dawa za Kulevya ambayo inaathiri afya ya vijana pamoja na kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia na ukatili wa Wanawake na Watoto vikiwemo vitendo vya ukatili dhidi ya makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino).

"Kama kuna jambo linaniumiza sana ni ajali za Barabarani hapa nitoe rai kwa wadau wote wa usafirishaji Madereva, Watumiaji wa Barabara na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani tushirikiane kusimamia Sheria na kuzingatia alama za Barabarani zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria"

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na iliyotukuka anayofanya katika kuhakikisha nchi inakuwa salama muda wote ikiwa ni pamoja na kuliwezesha Jeshi la Polisi kwa kuwapandisha vyeo Askari katika ngazi mbalimbali sambamba na kutoa kibali cha ajira kwa Askari wapya.

"Nizidi kutilia mkazo kwenye jitihada anazozifanya IGP Camillus Wambura za kupeleka Wakaguzi wa Polisi hadi ngazi ya Kata/Shehia kwa kutambua umuhimu wa Wakaguzi wa Kata/Shehia nchi nzima kwa kuwapa motisha na kuwawekea mazingira mazuri ya kazi kama ambavyo Mhe. Mhandisi Hamad Masauni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alivyokwisha anza kwa kuwatambua wanaofanya vizuri kila mwaka" Alisema

Awali katika taarifa yake Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo CP Awadhi Juma Haji aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa jinsi wanavyoliwezesha Jeshi la Polisi kwa kulipatia Vitendea kazi vya kutosha pamoja na Rasilimaliwatu.

Mhe. Mgeni Rasmi Kozi hii unayokwenda kuihitimisha hii leo Chuoni hapa ni miongoni mwa Kozi zilizokuwa zikiendelea katika vyuo vyetu vingine hapa Nchi ambapo inafanya jumla Askari 3464 ambao wamedhuria Mafunzo na kuhitimu katika ngazi mbalimbali

Source : MOHA
 
Katika Qur'an, hukumu ya Siku ya Kiama inatajwa kwa uwazi katika sehemu nyingi, ikiweka msisitizo wa matukio yatakayojiri na hali ya watu wakati huo. Siku ya Kiama inaitwa kwa majina tofauti kama "Yaumul Qiyama" (Siku ya Kusimama), "Yaumul Hisab" (Siku ya Hesabu), "Yaumul Fasl" (Siku ya Tofauti), na mengine mengi. Qur'an inaeleza kuwa siku hiyo itakuwa ni siku ya haki, ambapo kila nafsi itahukumiwa kwa matendo yake ya duniani.

Baadhi ya aya zinazozungumzia hukumu ya Siku ya Kiama ni:

1. Surat Az-Zalzalah (99:7-8):
- "Basi atakaye fanya wema wa chembe ya uzito wa chembe atauona. Na atakaye fanya ubaya wa chembe ya uzito wa chembe atauona."

Aya hii inasisitiza kuwa kila kitendo, kiwe kidogo au kikubwa, kitafikishwa kwa hesabu mbele ya Allah, na kila mtu atapata malipo au adhabu kwa matendo yake.

2. Surat Al-Qariah (101:6-9):
- "Ama ambaye mizani yake ya (mema) itakuwa nzito, basi huyo atakuwa katika maisha ya furaha. Na ambaye mizani yake ya (mema) itakuwa nyepesi, basi makao yake yatakuwa Hawiya (jahannamu)."

Hii inafafanua kuwa mizani ya matendo ndiyo itakayoamua hatima ya kila mtu, ama kuingia Peponi au Jahannamu.

3. Surat Al-Haaqqa (69:18-19):
- "Siku hiyo mtafikishwa (kwa Mola wenu) hamna kilichofichwa katika siri zenu. Basi yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia atasema: Haya! Sikilizeni msome kitabu changu!"
Haya matakataka ndo nini
 
Last time wamemwachia Mungu nini kimetokew? More peoples wamezidi kupotea
Man hapa naongelea battle ya Sativa na huyo Afisa.Kuhusu waliopotea wengine ni jambo la vyombo vya kiusalama kufanya kazi yao(hii ngumu) au wanachi kuamka na kudai uwajibikaji wa mamlaka (hii ndio ngumu zaidi sababu ya unafiki wa watanzania)

Ndio maana nasema hapa amwachie Mungu tu maana ukiangalia mazingira ya yeye kuwa hai unaona ni nguvu ya Mungu na sio hirizi wala miti shamba
 
Back
Top Bottom