Nimesikia kuwa kesho ndo siku ya katiba.
Sina hakika hasa ni akina nani ndo wameipanga ila nahisi ni akina mwafulani.
Shughuli itafanyika hapo Segerea. Tundu Lissu atakuwa mtoa mada. Au labda mmoja wa watoa mada?
Ni jambo zuri. Katiba mpya ni kitu muhimu kwa mustakabali taifa.
It is long overdue. Way long overdue.
Baada ya Rais Magufuli kufariki, vuguvugu la katiba mpya limerudi tena.
Na sasa hivi ‘Twitter advocates’ wa hiyo katiba mpya wanasema liwe liwalo litalokuwa, katiba mpya lazima ipatikane.
Mikwara na maneno kama hayo kuhusu hiyo katiba mpya sikuyasikia sana kipindi cha utawala wa Rais Magufuli.
I wonder why 😂 🤔.
Nimefanya ka observation kangu kadogo kwa hizi siku za mwanzoni za utawala wa Rais Samia na nimegundua kwamba kuna ‘perception’ ya yeye kuwa mpole, mlaini, mdhaifu, msikivu, na vivumishi vingnine kama hivyo.
Perception hiyo ndo naona imewapa moyo wale Twitter activists kusema liwe liwalo litalokuwa, katiba mpya ni lazima ipatikane.
Juzi Rais kasema apewe muda kwanza aisimamishe nchi kiuchumi halafu ndo labda tutazungumzia na kuyaangalia hayo mambo ya katiba mpya, baadhi ya raia tumemshukia kama gunia la mawe.
Kuwa mpole na kuwa msikivu si vibaya. Ila kilicho kibaya ni watu kuwa na perception ya kwamba wewe ni dhaifu na kwamba huwezi kuwa kichwa ngumu na huwezi kustahimili mashinikizo.
Kila la kheri hiyo kesho kwa washiriki wote wa kongamano hilo la katiba mpya.
Ila sitosahau yale maandamano ya UKUTA na yale maandamano ya Instagram ya yule dada enzi Magufuli akiwa Rais 🤣.