BAVICHA kufanya Julai 1, 2021 kuwa siku ya Katiba

BAVICHA kufanya Julai 1, 2021 kuwa siku ya Katiba

Dai la katiba ni la watu wajinga wasiojua wanataka nini!

Ukiwauliza wana bavicha na hao wanaharakati wajinga kwamba unataka katiba mpya ili iweje, hana cha kujibu zaidi anafikiri katiba mpya itaweka mazingira mepesi ya kuwezesha wao kuingia ikulu kirahisi!

Kenya wana katiba tunayoambiwa ni nzuri sana lakini ni nzuri kwa wanasiasa tu maana ufisadi na maisha magumu kwa raia viko pale pale!

Wapeleke uhuni wao huko! Wao waendelee kupambana na mondi tu.
Usitishe watu wewe Kama huoni mapungufu acha wenye kuona waidai kila mtu apa dunian Ana maoni yake
 
Hivi wewe uliwahi hata kufikiria kuandamana enzi Magufuli akiwa Rais? Au ngebe zako huwa unazipigia JF tu?
Uongozi wa kisiasa ni kushawishi ufuasi kwa kujenga hoja, kupambanisha hoja na kuuza sera Magufuli hakuwa uwezo huo kabisa; kama ulivyopata kumuelezea wewe mwenyewe, village bumpkin. Kuficha huo udhaifu wake alijifungia ndani ys nchi na kuamua kutumia dola dhidi ya raia yeyotr asiykubaliana naye ndani na nje ya chama chake. Huo siyo uongozi imara wa kutukuzwa; kusema kweli ni uoga uliopitiliza. Kiongozi mshindani mwenye busara hawezi kuongoza wafuasi wake kushindana na mtu wa aina hii ambaye kwa hakika yuko tayari kuua raia wasiokuwa na silaha. Hata ccm waliomsimika waliamua kumwacha wakijua mwisho wake utafika.
 
Kama ambavyo Dikteta aliiba kura na kuzima mtandao ili atangazwe mshindi kwenye birthday yake ilikuwa ufahari??

Dikteta kwangu mimi atabaki kuwa mshamba na mtawala wa hovyo kupata kumshuhudia baada ya Bokassa
 
Hauoni kwamba ni vigumu sasa kwa hoja hiyo kuwaleta watu wawe kitu kimoja kwa sababu ya mitazamo yao ya kisiasa?

Hayo makundi mengine yapo kusubiri wanasiasa, na wala hayajawahi kuwa na maamuzi yoyote ndani ya nchi. Huo ndio ukweli hata kama utaamua kukataa.
 
Wewe ulishawahi kumsogelea kichaa mwenye kisu mkononi kwa nia ya kishindana naye kwa hoja?
Apologists wa shujaa wanatetea legacy! Kwamba eti kuteka watu, kuua, kubambikiza kesi, kufilisi, nk ndio kuwa strong leader! Huyu anayeonyesha kuwa tofauti na compromising ni dhaifu!
 
Upande wa pili ni kutotaka katiba ya wananchi? Wakati wa Tume ya Nyalali ccm walikuwa wanabeba watu kwa malori kwenda kwenye mikutano ya Tume ili kuongeza idadi ya watu wanaotoa maoni kukataa vyama vingi. Mwisho wa siku 20% tu ya wananchi walionekena kutaka vyama vingi. Pamoja na uchache huo na akijua hila zilizofanywa na ccm Baba wa Taifa akawashamgaza ccm kwa kutamka hadharani kuwa hao 20% wanapaswa kusikilizwa na kupewa vyama vingi kwa sababu ni haki yao! Vivyo hivyo kwa hili la katiba mpya, kama kuna wanaoridhika na katiba ya sasa hawatapoteza chochote kama hao wachache watatimiziwa haja yao.
 
Kwanini nyinyi mapunda wa CCM mnaiogopa katiba mpya kama mnajua haina madhara kwenu? Si muweke na tume huru tuingie uwanjani tuone kama saa 4 itafika
Kwahiyo wewe katiba mpya ni kwa ajili ya tume huru tu?
 
Dogo una miaka mingapi? Wewe ni msimbe?

Ndio maana nimekwambia hivi katiba iliyopo ni sawa na mwaume anaishi na mtoto wa mtu bila kufunga ndoa.
Kuna ubaya wowote mtu asipofunga ndoa?

Watu wakikubaliana wakaishi maisha yao pamoja bila ndoa kuna ubaya gani?
 
Dai la katiba ni la watu wajinga wasiojua wanataka nini!

Ukiwauliza wana bavicha na hao wanaharakati wajinga kwamba unataka katiba mpya ili iweje, hana cha kujibu zaidi anafikiri katiba mpya itaweka mazingira mepesi ya kuwezesha wao kuingia ikulu kirahisi!

Kenya wana katiba tunayoambiwa ni nzuri sana lakini ni nzuri kwa wanasiasa tu maana ufisadi na maisha magumu kwa raia viko pale pale!

Wapeleke uhuni wao huko! Wao waendelee kupambana na mondi tu.
Jinga wewe!
 
Hili nilisema toka mwanzo kwamba Samia awasikilizee weee, ila mwisho wa siku hadi inafika 2025 hakuna kitu watapata, na watashiriki uchaguzi watake wasitake[emoji23][emoji23][emoji23]

Tena akiwaita na kina Mbowe ikulu wakanywe juis ndio kabisa atakuwa kawamaliza
Ni nani alikatiza mchakato? Kama ni ccm sawa lakini kama alikuwa Magufuli basi lolote lawezekana.
 
Katiba inapofanywa kuwa hitaji la kisiasa, ndio kosa linaanzia hapo
Katiba inaweza isiwe muhimu ukipata rais aina ya Nyerere na hata Samia lakini aina ya Magufuli haa ni kama unaendesha garei lisilo na breki kwenye mlima!
 
Uzuri mmoja mama ni kama jk anawaachaa wafanye mikutano yao lakini masikio kayaweka mbalii wao wenyewe watachoka na watatulia
Hamna namna, ni kucheza na biti lao tu songi likiisha unaenda kulala na kuwacha na mhaho...
 
Nimesikia kuwa kesho ndo siku ya katiba.

Sina hakika hasa ni akina nani ndo wameipanga ila nahisi ni akina mwafulani.


Shughuli itafanyika hapo Segerea. Tundu Lissu atakuwa mtoa mada. Au labda mmoja wa watoa mada?

Ni jambo zuri. Katiba mpya ni kitu muhimu kwa mustakabali taifa.

It is long overdue. Way long overdue.

Baada ya Rais Magufuli kufariki, vuguvugu la katiba mpya limerudi tena.

Na sasa hivi ‘Twitter advocates’ wa hiyo katiba mpya wanasema liwe liwalo litalokuwa, katiba mpya lazima ipatikane.

Mikwara na maneno kama hayo kuhusu hiyo katiba mpya sikuyasikia sana kipindi cha utawala wa Rais Magufuli.

I wonder why 😂 🤔.

Nimefanya ka observation kangu kadogo kwa hizi siku za mwanzoni za utawala wa Rais Samia na nimegundua kwamba kuna ‘perception’ ya yeye kuwa mpole, mlaini, mdhaifu, msikivu, na vivumishi vingnine kama hivyo.

Perception hiyo ndo naona imewapa moyo wale Twitter activists kusema liwe liwalo litalokuwa, katiba mpya ni lazima ipatikane.

Juzi Rais kasema apewe muda kwanza aisimamishe nchi kiuchumi halafu ndo labda tutazungumzia na kuyaangalia hayo mambo ya katiba mpya, baadhi ya raia tumemshukia kama gunia la mawe.

Kuwa mpole na kuwa msikivu si vibaya. Ila kilicho kibaya ni watu kuwa na perception ya kwamba wewe ni dhaifu na kwamba huwezi kuwa kichwa ngumu na huwezi kustahimili mashinikizo.

Kila la kheri hiyo kesho kwa washiriki wote wa kongamano hilo la katiba mpya.

Ila sitosahau yale maandamano ya UKUTA na yale maandamano ya Instagram ya yule dada enzi Magufuli akiwa Rais 🤣.
With Magufuli in power, a new strategy was required. It was effective.
With this mama ni power, another strategy is required. This one is lesser lethal, but full of benefits.
 
Back
Top Bottom