BAVICHA: Tumesikitishwa sana na walioenda kuapa, ni kitendo cha usaliti, hujuma na hakiwezi kuvumilika. Wataka hatua kali zichukuliwe

BAVICHA: Tumesikitishwa sana na walioenda kuapa, ni kitendo cha usaliti, hujuma na hakiwezi kuvumilika. Wataka hatua kali zichukuliwe

Kuwafukuza WANAWAKE wapambanaji na WENYE MAONO ni kuwaonea tu na kurudisha nyuma DEMOKRASIA....

Mnadai Halima Kawasaliti....

Mbona ninyi MLIMSALITI Tundu Lissu kutoandamana?!!!

Nyiye kina OKW BOBAN mbona MLISALITI kwenda pale UBUNGO katika maandamano ya AMANI?!!!

Leo hii mnawaita wenzenu WASALITI?!!!

Mmesahau ya kuwa ukiwa na KIU KIKALI..na ukaomba MAJI..na kupewa NUSU GLASS...usitukane na KUBWATA...YANYWE HAYO KWANZA!!!
Hallima na wenzake wameamua KUNYWA HAYO MAJI NUSU GLASS.....
 
13m x 60 months+90m ( v8)+ 300m ( kiinua mgongo)

Jumla hapo ni 1.170 billion kwa miaka 5 hapo hatujaongelea zile laki 3 per day during a bunge sessions

Aache mzigo wote kwa ajili ya 'heshma aliyojijengea)?

Wee ungeacha kusema ukweli?
Hiyo pesa ya damu hawatakaa wawe na amani nayo. Wale vijana walio ikiwa, waliowekwa ndani kwa mateso. Walikipigania chama.
 
13m x 60 months+90m ( v8)+ 300m ( kiinua mgongo)

Jumla hapo ni 1.170 billion kwa miaka 5 hapo hatujaongelea zile laki 3 per day during a bunge sessions wala ma posho ya kamati kadhaa hasa kama ile ya PAC ambayo imemuwezesha Mtoto wa Mwandiga kuishi eneo moja na kina Bakhresa, Sofia Simba, n.k

Aache mzigo wote kwa ajili ya 'heshma aliyojijengea?

Wee ungeacha kusema ukweli?
Kama shida ni mzigo mbona alishakusanya sana au anataka kuwa Mo kwa mgongo wa ubunge?!

Aibu inamsogelea sasa.
 
Leo baraza la vijana wa CHADEMA Taifa limetoa msimamo kufuatia wabunge 19 ambao wamekwenda kuapa bungeni kinyume na msimamo wa chama.

MWENYEKITI: BAVICHA tulikutana katika kikao chetu tulichokifanya kwa njia za kidijitali kujadili mustakabali wa chama chetu kufuatia kadhia hii iliyotokea katika chama.

Jambo la kwanza ambalo BAVICHA tumekubaliana ni kuunga mkono msimamo wa chama chetu, kwanza kutotambua matokeo ya uchaguzi, kutoutambua uchaguzi wote na matokeo yake yote. Huo msimamo wa kwanza ambao umekuwa ukitangazwa na chama chetu kuanzia mwanzo huo ndio msimamo wa BAVICHA.

Pili tunaunga mkono msimamo wa chama juu ya hawa ambao walienda kuapa, walioenda kinyume na muongozo wa chama chetu, tunaunga mkono msimamo wetu wa chama kwamba watu hawa waitwe hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Tunaunga mkono msimamo wa chama kwasababu kamati kuu ya CHADEMA ambayo ina uwakilishi wa vijana kwenye kamati hiyo na muwakilishi wa vijana hao ni mimi, katika vikao vya kamati kuu ya chama hatukuwahi kujadili, hatujawahi kupitisha orodha yoyote ya wabunge wa viti maalum


Angalau hawa vijana wamethubutu, sasa ngoja tuone Mbowe na Salum Mwalimu watuhumiwa wa kula bilion 3 za Ndugai kuwauzia watumwa 19 wa kike watakuja na majibu gani kesho
 
Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa Chadema Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumuuwa Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama.

Baada ya sauti hizo kuvuja mara moja chama kilitangaza kikao cha dharura cha kamati kuu kuwahoji ili waweze kuchukuliwa hatua kali sana ikiwa pamoja na kufukuzwa Chadema.
Matokeo yake baada ya kikao cha kamati kuu hao wabunge wauaji walisamehewa na kutakiwa kuomba radhi tu!!!

Kama hali ni hiyo, wabunge wa viti maalum Chadema si wauaji na wala hawajatishia kumuuwa mtu yoyote ila wanajaribu tu kutumia haki yao ya kikatiba iweje wafukuzwe Chadema?
Kweli kuwa mwanamke Chadema ni dhambi kubwa kuliko wapanga mauaji waliosamehewa??

Tusubiri na kuona kesho kikao cha kamati kuu chadema kitaamua nini ,bila shaka Mbowe is going to be tested again na maamuzi tofauti na kufukuza yatamwimalisha ,na maamuzi ya kufukuza hao wanawake itakuwa ni kiss of death kwa Mbowe na Chadema kwa ujumla.
 
Bavicha bwana!!haya ngoja tuendelee kuona huu mchezo utaishaje...
 
Mnamuita HALLIMA MSALITI...

Hivi kuna msaliti kama Mh.MBOWE....

Aliwasaliti watu WALIOMPINGA Mzee wangu Laigwanan Lowassa....

Aliwasaliti akina Lissu na Dr.Slaa baada ya mshenga mh.Dr. GWAJIMA kuweka "mikono mezani"......hatimaye AKAIBADILISHA GIA ANGANI....

Leo BAWACHA wameibadilisha GIA ANGANI...kwa kuudurusu mustakabali wa SIASA ZILIVYO kwa "Wakati huu" mnawaona MAADUI?!!

PATHETIC
 
Mwacheni Kamanda ale za mwisho mwisho, atakuwa katimiza 20 years akiwa Mbunge akitoka Darasani Chuo Kikuu cha Dsm

Mtaani kugumu sana, si umeona Zitto kageukia Mgogoro wa Ethiopia kujifanya mtaalam wa Migogoro kwa kushina Tweeter ku post na ku tag viongozi wakubwa wa UN na AU ili apate kijiwe kipya
Kama shida ni mzigo mbona alishakusanya sana, au anataka kuwa Mo kwa mgongo wa ubunge?!
 
Chadema mmeshaona kuwa mh.Rais na policy zake ni KUIJENGA NCHI Kama alivyofanya KUN LEE YEW na Meles Zenawi.....

Mmeshaona kuwa mh.Rais ana Misimamo yake...

Busara ni KUVUMILIA...kwani KUENDELEA KUSHUPAZA MGONGO haitokuwa AFYA....

Hallima Mdee AMEAMUA KUVUMILIA...
Hallima Mdee AMEAMUA kubadilisha TACTICS....

HIZO NDIZO BUSARA
 
Hallima James Mdee Wala si MSALITI...
Siyo hivyo ipo hivi kwanza list ya wabunge viti maalum haipaswi kuwagusa wale waliogombea ubunge majimboni, huwa ni watu fresh tokea kwingine lakini hilo dili la ununuzi wa watumwa wa kike kuuzwa kwa Ndugai linaenda kukigawa chama na ndipo CHADEMA inafariki na kuwa kama TLP NCCR na CUF ya Lipumba
 
Angalau hawa vijana wamethubutu, sasa ngoj tuone mbowe na Salum mwalimu watuhumiwa wa kula bilion 3 za Ndungai kuwauzia watumwa 19 wa kike watakuja na majibu gani kesho
Hawa vijana waongowaongo tuuuu. Kama walikatamata mabox kwa nini hawakupeleka polisi.Uongo huu ndiyo mtu wenu ameupeleka kwa wazungu nao wakaupokea. Haki inatafutwa mahakamani leo kweli chadema wameshindwa kupeleka issue hii mahakamani huku vielelezo wanavyo.Kuweni serious you chadema
 
Nachosimamia tuache Unafiki

Waliokuwa wanamshinikiza yule Mbunge wa kule Mpanda Chadema asiende kula kiapo Bungeni, walipopewa fursa wao hawakusubiri kula Kiapo Ndani ya Bunge, wamekula kiapo kwny kibaraza cha Bunge kwa nje
Hukujuavua unachosimamia.
 
Hallima James Mdee Wala si MSALITI.

Kilichopo kinafichwa.

Mnyika ANAJUA kuwa SAFARI HII...BAWACHA wamekataa kuwa STAMP ya kupitisha majina "ya wabunge WANAOTAKIWA NA MWENYEKITI TU...na inner circle yake".
Hujui kwamba chama kina katiba.....!?
watu hawajiamulii tu mambo
 
Nachosimamia tuache Unafiki

Waliokuwa wanamshinikiza yule Mbunge wa kule Mpanda Chadema asiende kula kiapo Bungeni, walipopewa fursa wao hawakusubiri kula Kiapo Ndani ya Bunge, wamekula kiapo kwny kibaraza cha Bunge kwa nje
Jipongezeni kwa kufanikiwa kupata mateka wa kuoneshea wazungu kuwa mna upinzani bungeni.
 
Back
Top Bottom