BAWACHA: Rais Samia asiwatambue Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama CHADEMA

Rais wa nchi anahusikaje na kuwatambua au kutowatambua wabunge? Hilo ni suala la spika wa Bunge.

Vv
 
Sasa kama wameshawafukuza uanachama kinachowasumbua kuwa fuatafuata ni nini? waacheni waendelee na mambo yao nyie hamuwatambui mnataka wao wawatambue nyie kama kina nani? mnawapa umaarufu hebu kaeni bila kuwaongelea muone kama kuna tatizo shida mnayo nyie mnaowaongelea kila siku mmeshawafukuza basi.
Kweli aisee, wanafanya michezo ya kitoto, unamuacha demu lakini bado unaendelea kumfatilia na kila siku kuchungulia kama kaingia whatsap, mwisho wa siku unajikuta unakonda mpaka unakufa.
 
na kama wanadai wamewavua uanachama huku hawataki kusikiliza rufaa zao sasa kinachowasumbua nini ? mmemvua uanachama siyo mwanachama wenu kinachowafanya waanze kutaka kumsumbua mama avunje katiba kuingilia mhimili wa bunge ni nini?
Hapa ndo patamu. Badala ya kusikiliza rufaa zao wanakimbilia kulishinikiza Bunge liwafukuze. Ilitakiwa kwanza wamshinikize Mbowe aitishe kikao cha kusikiliza rufaa zao kwa mujibu wa katiba yao inavyosema. Halafu kama wanazitupilia mbali ijulikane kwamba wamezikataa rufaa zao.

Halafu baada ya hapo , wamuandikie Spika kuhusu kuwavua uanachama wabunge wao, siyo kuongea kwenye mitandao. Spika hawezi kufanya kazi kwa mitandao.
 
Wewe usiwe iboya kama jina lako. Katiba inatamka wazi kuwa bunge lina sehemu mbili yaani Rais na Wabunge. Ukikiri ujinga wako utapungukiwa nini?
RAIS ni mhimili unaojitegemea ni taasisi na bunge ni mhimili unaojitegemea hauwezi kuingiliwa na mhimili mwingine acha uboya wewe
 
Katika mkutano huo, Catherine Ruge amesema:

Tumeona kwenye vyombo vingi vya habari kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani anaenda kulihutubia Bunge tarehe 22 -04-2021 kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kwa rais wa JMT kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Dkt John Magufuli.

Kuelekea tukio hilo, sisi BAWACHA tuna jambo mahususi amabalo tungependa kuliwasilisha kwa Mh. Rais.

Jambo hilo ni uwepo wa wanaoitwa Wabunge 19 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa anakwenda kulihutubia Bunge hapo kesho, sisi wanawake wa CHADEMA tungependa atambue, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna watu wanaoitwa Wabunge 19 ambao wapo katika hilo bunge analotaraji kuhutubia, kinyume na katiba...

Hata hivyo, hao Wabunge 19 hawajakidhi vigezo kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwakuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameapa kuilinda katiba ya JMT na amekuwa akieleza hivyo mara kadhaa kwenye hotuba zake ambazo amekuwa akizitoa baada ya kuwa ameapishwa.

...atakuwa amevunja katiba kwa kuwaruhusu hao wanaoitwa Wabunge 19 kuhudhuria vikao vya bunge na kushiriki shughuli mbalimbali za bunge.

----- MAONI YANGU ----

BAWACHA hawaelewi maana ya kutofautisha mihimili​

Nimesikiliza maongezi ya Bawacha walivyokuwa wanaongea na waandishi wa habari Dodoma yaani inaonekana wazi kuwa hawajui ni nini wanataka au ninini wafanye.

Unapomwambia Rais anapoenda bungeni asiwatambue au aende kuongelea suala la hao wabunge ni kumkosea adabu mheshimiwa Rais.

Yaani mnamtaka avunje katiba hadharani ili baadae mje tena muanze kusema kavunja katiba; hivyo atakuwa anaingilia mhimili mwingine, hiyo haiwezekani.

tafuteni agenda nyingine siyo kumuingiza mama kwenye mifarakano ya taasisi yenu.

Asante

Wanawake wanaoneana wivu wa kitoto sana hao wakina ruge hawana lolote zaid ya wivu tu kwa wenzao

Coz kama wamefukuzwa chama na wako bungeni bila chama then wao shida yao ni nn?

Au wao ni watetezi wa wabunge wasio na chama
 
Hapa ndo patamu. Badala ya kusikiliza rufaa zao wanakimbilia kulishinikiza Bunge liwafukuze. Ilitakiwa kwanza wamshinikize Mbowe aitishe kikao cha kusikiliza rufaa zao kwa mujibu wa katiba yao inavyosema. Halafu kama wanazitupilia mbali ijulikane kwamba wamezikataa rufaa zao.

Halafu baada ya hapo , wamuandikie Spika kuhusu kuwavua uanachama wabunge wao, siyo kuongea kwenye mitandao. Spika hawezi kufanya kazi kwa mitandao.
sawa kabisa mkuu unafikiri wanaelewa hawa? halafu ndiyo wapewe nchi hiyo katiba itakuwa inavnjwa kila siku
 
siyo kweli bunge lina jitegemea na taasisi ya rais inajitegemea huwezi rais ukaanza kumpangia bunge mambo ya kufanya utakuwa umenajisi bunge muacheni mama msimvunjishe sheria

Serikali Ina mihimili mitatu,Ila nadhani umesahau kuwa Kuna muhimili umejichimbia chini zaidi😆😆😆🏃🏃
 
siyo kweli bunge lina jitegemea na taasisi ya rais inajitegemea huwezi rais ukaanza kumpangia bunge mambo ya kufanya utakuwa umenajisi bunge muacheni mama msimvunjishe sheria

Serikali Ina mihimili mitatu,Ila nadhani umesahau kuwa Kuna muhimili umejichimbia chini zaidi😆😆😆🏃🏃
 
Katika mkutano huo, Catherine Ruge amesema:

Tumeona kwenye vyombo vingi vya habari kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani anaenda kulihutubia Bunge tarehe 22 -04-2021 kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kwa rais wa JMT kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Dkt John Magufuli.

Kuelekea tukio hilo, sisi BAWACHA tuna jambo mahususi amabalo tungependa kuliwasilisha kwa Mh. Rais.

Jambo hilo ni uwepo wa wanaoitwa Wabunge 19 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa anakwenda kulihutubia Bunge hapo kesho, sisi wanawake wa CHADEMA tungependa atambue, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna watu wanaoitwa Wabunge 19 ambao wapo katika hilo bunge analotaraji kuhutubia, kinyume na katiba...

Hata hivyo, hao Wabunge 19 hawajakidhi vigezo kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwakuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameapa kuilinda katiba ya JMT na amekuwa akieleza hivyo mara kadhaa kwenye hotuba zake ambazo amekuwa akizitoa baada ya kuwa ameapishwa.

...atakuwa amevunja katiba kwa kuwaruhusu hao wanaoitwa Wabunge 19 kuhudhuria vikao vya bunge na kushiriki shughuli mbalimbali za bunge.

----- MAONI YANGU ----

BAWACHA hawaelewi maana ya kutofautisha mihimili​

Nimesikiliza maongezi ya Bawacha walivyokuwa wanaongea na waandishi wa habari Dodoma yaani inaonekana wazi kuwa hawajui ni nini wanataka au ninini wafanye.

Unapomwambia Rais anapoenda bungeni asiwatambue au aende kuongelea suala la hao wabunge ni kumkosea adabu mheshimiwa Rais.

Yaani mnamtaka avunje katiba hadharani ili baadae mje tena muanze kusema kavunja katiba; hivyo atakuwa anaingilia mhimili mwingine, hiyo haiwezekani.

tafuteni agenda nyingine siyo kumuingiza mama kwenye mifarakano ya taasisi yenu.

Asante
Right. Hiyo ni kazi ya spika.
 
Soma katiba, rais ni sehemu ya bunge. Ndio maana tunalilia katiba iliyoboreshwa ikiwemo kutenganisha kabisa mihimili ya dola.

Lakini hata mwanasheria wa serikali ni sehemu ya wabunge! Ila ni kweli huwezi kumpangia rais cha kusema.
siyo kweli bunge lina jitegemea na taasisi ya rais inajitegemea huwezi rais ukaanza kumpangia bunge mambo ya kufanya utakuwa umenajisi bunge muacheni mama msimvunjishe sheria
 
Huenda hajui kuwa anapingana na katiba au haamini ukweli wako. Tunaposema katiba yetu ina upungufu mkubwa ni pamoja na hilo!
KATIBA INASEMA HIVYO ,Wewe unasema "siyo kweli".
Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania lilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 62(1) ya Katiba na lina sehemu mbili, ambazo ni Rais na Wabunge.
 
RAIS NI SEHEMU YA BUNGE......
Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania lilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 62(1) ya Katiba na lina sehemu mbili, ambazo ni Rais na Wabunge.
Watu wengi hawaelewi tofauti ya Parliament na National Assembly. Rais anapoingia bungeni ndo linakua N. Assembly so kesho akiyaongea hayo ndani ya Bunge anakua hajavunja katiba ila sio akiwa nje wakati Parliament inaendelea

Na ndiyo maana Rais akiingia Bungeni anakaa kule mbele na yeye bila kutengua kanuni yoyote.

Pia wanasahau kuwa hata Katibu wa Bunge anateuliwa na Rais

My two cents
 
Kuna wakati kuwaelewa Chadema ni lazima unywe pombe kwanza

Wote tunakumbuka mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 Chadema ilitangaza kuyakataa matokeo yaliyompa ushindi Dr Magufuli na mama Samia na wakadai hawamtambui Rais aliyetangazwa.

Leo Chadema hao hao wanamtaka Rais Samia aliyeshinda pamoja na hayati Magufuli 2020, asiwatambue wabunge wake wa viti maalumu walioko bungeni.

Pamoja na kwamba siyo kazi ya Rais Samia kutambua nani ni mbunge na nani siyo, Chadema waelewe wanatuchanganya wafuasi wao kwa namna wanavyoendesha mambo kienyeji.

Ramadhan Kardem!
 
Kama chadema walitimiza hatua zote za kuwavua uanachama Sasa Nini Tena wasiwasi. Kikubwa Ni kutomuingilia rais kwenye majukumu yake. Yeye siyo time ya uchaguzi na pia pamoja na kuwa sehemu ya bunge suala la nidhamu ya bunge na uendeshwaji wake yupo spika
 
Mkuu @ohnthebaptist, mimi ni msomaji mzuri wa mada zako na huwa nachangia. Ila hii iko chini ya kiwango. Ukiweza i-DELETE
Imelenga ukweli mtupu!
CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO huwa hamna sera zaidi ya majungu tu.
 
Back
Top Bottom