Inajulikana wazi kuwa Rais Samia Suluhu kabla ya kukabidhiwa madaraka haya ya urais, aliapa kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi.
Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, katika Ibara ya 67(1)(b) inaeleza wazi kuwa huwezi kuwa mbunge wa Bunge letu, bila kwanza kuwa mwanachama chama cha siasa nchini.
Tunajua pia kuwa chama cha Chadema kilishawavua uanachama wao hao wanaoitwa ni wabunge wa viti maalum wa Chadema
Sasa tunamtegemea Rais wetu Samia Suluhu, alihutubie Bunge baadaye leo majira ya saa 10 jioni na kukitengua kitendawili hicho.
Aidha awe upande wa Spika Ndugai, ambaye kila mwananchi anajua kuwa ameivunja Katiba ya nchi, kwa kuendelea kuwatambua na kuwakumbatia hao wabunge akina Halima Mdee, au asimamie Katiba ya nchi na kumueleza Spika Ndugai kuwa anakosea kuendelea kuwakumbatia wabunge hao, kwa kuwa siyo wabunge halali, kwa mujibu wa Katiba yetu.
Kwa kuwa Rais wetu ameonyesha wazi kuwa anaitii na kuiheshimu Katiba ya nchi yetu. kwa hiyo "ramli" ya nini kitatokea baada ya hotuba yake hiyo kuhusiana na wabunge hao kinatabirika!