BAWACHA: Rais Samia asiwatambue Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama CHADEMA

Wewe ndio mjinga kama unawakubali wabunge wasio halali.
 
Hilo ni swala la Tume ya uchaguzi!
 
Hiko kitendwali hakiwezi kuteguliwa na Rais kwa sababu yeye sio mkuu wa mhimili wa bunge. Msitegemee lolote kutoka kwake kuhusu kwake. Hiko ni kitendwali cha Ndugai.
 
Nitaisikiliza hotuba mwanzo mwisho; asipotatua swala la kina Mzee Mdee na Covid-19 wenzake, nitasikitika sana
 
Sasa tunamtegemea Rais wetu Samia Suluhu, alihutubie Bunge baadaye leo majira ya saa 10 jioni na kukitengua kitendawili hicho.
Mbunge akishaapa,ni mahakama tu
Badala ya kuharibu kutafuta huruma ya Rais,ni bora mkapeleka mapambano mahakamani
 
Mbona afadhali ya mwasilisha mada kuliko hoja yako isiyo na nukta ya uelewa? Kwa kuwa mtz tu bila kujali elimu ungeujua ukweli
 
SEMA SASA YAKO AMBAYO SIO RUBBISH
 
Jikite kwenye hoja bimkubwa.
 

Ishu ni kuwa je ni kwanini chadema iliwavua wakina mdee uanachama?

Wakina mdee wamevuliwa uanachama kwa sababu moja tu ya kutii katiba na sheria ya inchi

Jambo la viti maalum sio jambo la chadema ni jambo la kisheria

Sasa kisa tu Bwana mjika madem zake hawapo kwenye ubunge ndio wanune?

Kama ni kuibiwa kura nitajie ni mwaka gani chadema hawajaibiwa kura na mbona walikuwa wanaenda bungeni?
 

Na ukumbuke katiba ndio inataka viti maalum so wakina mdee hawajavunja katiba yoyote
 
Mleta mada, kwa Mama Samia hili kwake ni gumu kwa sababu hahusiki nalo! Anachotakiwa kufanya ni kupiga tu jiwe kizani kueleza ni namna gani hafurahishwi na jinsi uvunjwaji wa wazi wazi wa katiba kwenye taasisi mbalimbali ikiwamo bunge. Kinyume na hapo, asithubutu kabisa kugusia moja kwa moja suala hilo kwa sababu ataonekana anaingilia mhimili mwingine!
 
Ana wakati mgumu sana. Ile kauli yake kwamba yeye na JPM ni mtu mmoja haikuwa nzuri. Aachane na kivuli cha mtangulizi wake akitaka kuheshimu katiba na kutenda haki.
 
Anahusika kikatiba. Hilo liko wazi ingawa kwako ni maji marefu.
Akifanya hivyo itakua haingilii mhimili wa Bunge??

Katiba inasemaje kuhusiana na mamlaka ya Rais juu ya Mbunge na ukizingatia sio wa Chama chake??
 
Hivi kwa mazingira ya Tanzania kipindi cha Mwendazake unadhani Chadema wangeenda kufungua kesi haki ingetendeka?

Hapa duniani kuna kitu kinaitwa KARMA ndio kipo na nilazima ifanye kazi. Naimani Rais wa sasa Mama Samia ni Mungu pekee ndio kamweka hapo alipo kwa makusudi flani, na siku zote kusudi la Mungu ni lazima litimie. Kila mtu kashuhudia uvunjifu wa wazi wa katiba juu ya wabunge 19 pale bungeni, na hili sio jambo dogo na nilazima litatuliwe la sivyo Karma itafanya kazi yake.

Mh. Rais Mama Samia leo tunapaswa tumuombee kwa Mungu ili atende sawasawa na mapenzi ya Mungu ili kuepusha Karma.

Tukutaneni Dodoma bungeni saa 10 jioni
 
Hili suala halina ugumu wowote ila kama yeye atamlinda Ndugai kwkw wote ni CCM. Na CCM ndiyo iliwapa zawadi hao covid-19.
Kikatiba wabunge wote pamoja na Ndugai mwenyewe wapo pale kutokana na uchaguzi mkuu wa 2020 uliokuwa wa mabavu. Mbaya zaidi ni kwamba SSH nae ni mnufaika wa mbinu zilizowaweka wenzake bungeni.
Hawezi kuwasaliti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…