BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua

Katika watu wote walioshitakiwa kwa ubakaji umewahi kuona video yoyote ya mtu akibakwa au unajitoa akili tu??
 
Yeye alikuwa anatoa bahasha so hawa waliopo wamewapelekea clip na kuwatisha wanaitoa, nadhani wamegoma wakawaa "toeni ashakufa mwenyewe"

Si unajua waandishi na njaa [emoji2]
Sio waandishi wote wana njaa, hasa unapozungumzia waandishi wa chombo kikubwa kama BBC cha ulimwengu wa kwanza ambaacho kinatoa hadi taarifa hasi za mabilionea mara nyingi tu.
 
Nikisikia haya majina,mwamposa, gwajima, kapole,na wengine wengi wanaojiita manabii,huwa naona opportunist tu.
Ni wezi, ambao,wamekosa njia ya kutafuta pesa,sasa ni kuuza injili, miaka kumi nyuma, hawa wangekuwa motivational speakers, watu waliwashitukia, wakaona watoke kiimani!
 
Mimi ninachojiuliza kwa nini wamesubiri kuitoa wakati ameshafariki
Nakazia: Na tutawaaminije hao BBC kwamba ni kweli hiyo Taarifa yao ukizingatia kwamba Mchungaji TB Joshua (Mtuhumiwa)hayupo tena ili aweze kujitetea.
 
Interesting....
 
Sema bongo tungepata waandishi kama Mohamed tungetolewa tongotongo nyingi. Jamaa alikuwa na full evidence
Dah!.....hatari sana hizo kazi....unaweza kupotea kama Azory Gwanda.
 
Yaani ngozi nyeupe na wao walinyanyaswa huku Africa na Joshua (Rip)..... interesting...

Kiranga
Kwenye documentary kuna disciple mmoja wa TB Joshua anasema kwamba TB Joshua alimwambia wazi kwamba ana mpango wa kuja kuwatumikisha wazungu Afrika kama wazungu walivyotumikisha mababu zetu.
 
Kwenye documentary kuna disciple mmoja wa TB Joshua anasema kwamba TB Joshua alimwambia wazi kwamba ana mpango wa kuja kuwatumikisha wazungu Afrika kama wazungu walivyotumikisha mababu zetu.
Daaah ndio ivyo kafa bila ndoto zake kutimia
 
Sio waandishi wote wana njaa, hasa unapozungumzia waandishi wa chombo kikubwa kama BBC cha ulimwengu wa kwanza ambaacho kinatoa hadi taarifa hasi za mabilionea mara nyingi tu.
Mambo ya rohoni husemwa kwa maneno ya rohoni.
 
Vita vyetu si juu ya damu na nyama bali ni falme na mamlaka na wakuu wa giza hili na majeshi ya pepo wabaya.
 
Neno la msalaba kwao wanaopotea ni upumbavu bali kwa wanaookolewa ni nguvu ya mungu
 
BBC ni nani mpaka wajue unabii fake na unabii wa kweli? Wamefunga maombi Mungu akawaonyesha unabii huo? Kwa Tb Joshua wameenda maelfu ya watu toka pande kuu nne za dunia na viongozi wakubwa wamefika kupata huduma za kiroho na asilimia 90% ya huduma yake ilikuwa live kila mtu alikuwa anaona namna ya mapepo yanavyotolewa, mimi nimefuatilia hao watu wanaotuhumiwa mbona ni maelezo tu bila hata video zinazoonyeshwa huo unyanyasaji? Kwa Tb Joshua wengine walikuwa wanakerwa wakiwa vichaa ili waombewe , mtu kichaa lazima afungwe kamba ili asilete madhara kwa watu wengine. Maswali ya kujiuliza
1. Unawezaje kuamini maelezo ya watu 30 na wakati wanaoenda pale scoan ni maelfu ya watu, kama hau ni maadui zake inakuaje?
2. Hao wanaodai wamedharirishwa kwanini watafute media badala ya kwenda mahakamani kumshitaki?
3. Kwanini wasubiri mtu amekufa ndoa watoe malalamiko hayo ?
4. Usafi na uhalali wa BBC kuhoji mambo ya kiroho wanaitoa wapi? Mbona ushoga unaolingana na biblia wameukumbatia?
5. Kwanini wengi wanaolalamika ni wale waliotolewa maepo na Tbl Kishua?
6. Mbona hao BBC hawaelezi mema yaliyofanywa na Tb Joshua ya kutumia billions of money kusaidia wasijiweza, kusomesha watu?
5 Tunajua huduma ya Tb Joshua iliharibu biashara za wakubwa duniani, ilifikia hatua wenye kansa, HIV, uvimbe, sukari na magonjwa mengi yanapona kwa njia ya maombi bila kutumia dawa.
Palipo na mafanikio chuki lazima, na mti mwema hutupiwa mawe.

BBC hawezi kutuelekeza mambo ya Mungu kuwa huyu ni mtumishi fake au wa Mungu. Hizo scandal wanazotengeneza hazifanikisha mipango yao ya kutaka kufuta legacy ya TB Joshua.
 
Tulia dawa iingie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…