BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua

BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua

Mimi sio mlokole na infact nimuumini wa Logic zaidi kuliko believes ila T.B Joshua kwangu alikua mtu noble sana.
Jamaa alikua mtoaji sana, habagui dini. Ametembelea nchi zenye ukristo na uislam mkali na amesaidia taasisi na orphanage nyingi sana duniani, wanafunzi kwa wazee wamebenefit sana na huyu mtu.
Heshima yangu kwake kamwe haiwezi kushuka.
Hata mafisadi, wauza dawa za kulevya na wafanyabiashara wakwepa kodi huwa wanasaidia sana watu.
Pablo escobar alikuwa anajenga hadi shule, viwanja vya mpira na makanisa. Vita vya madawa ya kulevya Mexico imekuwa ngumu zaidi kwa sababu cartels wanasaidia sana watu na taasisi mbalimbali.
 
BBC waache unafiki, abrakadabra ziko nyingi hata kwenye dini zenye watu wengi, mbona huko hawachokonoi? Akina Rushdie walithubutu kuchimbua ushetani ulioko kwenye dini fulani kubwa duniani wakaishia kutangaziwa kifo popote walipo na juzijuzi huyo mwandishi wa kitabu hicho nusura wapoteze maisha yake huko alikokimbilia tangu miaka mingi. BBC wanaona hakuna madhara watayopata toka kwa wafuasi wa TB Joshua na yeye hayupo duniani kuwajibu ndio wanajitia wazimu kuchokonoa imani hiyo. Hebu wajaribu kuchokonoa ile imani ya dini ile machachari kama wataacha kuona rangi zote. Kila dini ina abrakadabra zake na watu wanaamini
Sio kila kitu ni habari, sio kila abrakadabra za dini ni habari. Mbwa kumng'ata mtu haiwezi kuwa habari kubwa ila mtu kumng'ata mbwa ni habari kubwa.
 
sijawahi kuwa mfuasi wa tb joshua na wala kuamini miujiza yake sambamba na wengine wa aina yake waliopo hapa nchini. Fahamu kuwa hata huko unakoamini/kuabudu mungu wako/dini yako ni abrakadabra tu inayotakiwa kuwekwa wazi na sio akina tb joshua tu
Habari ya TB Joshua inahusu unyanyasaji katika mfumo wa "human trafficking" na udanganyifu/utapeli wa kukusudia.
Pia kuna habari nyingi sana kuhusu dhuluma za kingono katika kanisa Katoliki ambazo zimewahi kuripotiwa na BBC na vyombo vingi vikubwa vya habari.
 
Mimi sio mlokole na infact nimuumini wa Logic zaidi kuliko believes ila T.B Joshua kwangu alikua mtu noble sana.
Jamaa alikua mtoaji sana, habagui dini. Ametembelea nchi zenye ukristo na uislam mkali na amesaidia taasisi na orphanage nyingi sana duniani, wanafunzi kwa wazee wamebenefit sana na huyu mtu.
Heshima yangu kwake kamwe haiwezi kushuka.
Mazuri unayofanya hayafuti mabaya unayofanya. Hata kwenye Biblia mazuri na mabaya ya manabii yameanikwa wazi kudhihirisha kuwa watu si malaika, tuna upungufu mwingi.
 
Inategemea wamepata habari lini. Kuna vitu/siri nyingine hujulikana baada ya mtu kufariki. Mimi huyu hata kabla hajafariki nilishajua ni mwongo. Kuna siku aliponya mtu kasema am,etoka Tanzania huku anazungumza ikiingereza kila cha ki-nigeria
Lakn mwamposa unamuamn?
 
Breaking News: BBC inatazamia kuchapisha nakala ya uchunguzi wa kuacha vinywa wazi inayoeleza matukio ya kikatili, Miujiza ya Kughushi, uhalifu, na ubakaji uliofanywa na Marehemu Mchungaji Temitope Balogun Joshua, almaarufu Nabii TB Joshua!!!

Kupitia page ya twitter ya Sahara Reporters wameelezea matukio aliyofanya ambayo yanatarajiwa kupostiwa na BBC katika video
View attachment 2864719

Tizama kipande hiki cha BBC wakihoji watu waliokumbwa na unabii feki wa TB Joshua....
Hii inashangaza!!! 😱🚴🏿‍♀️🚴🏿‍♀️🚴🏿‍♀️💨

📺 Video Credit: BBC
View attachment 2864718

TB Joshua alikuwa ni mchungaji maarufu wa Kikristo na mwanzilishi wa kanisa la Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) huko Lagos, Nigeria. Alikuwa na ushawishi mkubwa katika jamii na alihusika katika huduma za kiroho, uponyaji, na mafundisho ya Biblia. Hata hivyo, alifariki dunia mnamo Juni 2021.

Pia soma: UCHUNGUZI WA BBC: TB Joshua aliwanyanyasa na kuwabaka wafuasi wake
Huo uchunguzi wa kuhoji watu ndio waseme maneno yao dhidi ya mwingine haufai

waweke vithibitisho live mtu akibakwa,akinyanyaswa,kama kuna video watoe
sio kutafuta mtu unamuhoji akuelezee alafu unaenda kutangazia dunia, huo sio uandishi wa habari,
Bbc hawana maadili

huo uchunguzi wao unaweza kua umejengwa kwa chuki

Hata wewe watu wanaweza wakahojiwa wakakuzungumzia vibaya tu

Wanaleta uchunguzi kwa mtu ambae hayupo na hawezi kujitetea tena,walikua wapi miaka yote?

Hawa wazungu hawataki black people to shine

Waache zao,ule uchunguzi wao kwa Uebert Angel kwani uliishia wapi?Mbona wamepotea hawajaletea mrejesho
 
Dah Ile ilikuwaga ya motooo mno full ushahidi
Watoe ushahidi,sio kutafuta Raia wameshawapanga waseme nini ndio unawahoji
Hatutaki ushahidi wa mdomoni,watoe ushahidi halisia

Nje ya hapo waache propaganda na hatutawaamini tena kama hawatakua na ushahidi unaojieleza wenyewe
 
Na Kwa Propaganda wapo vizuri,katika hili tutegemee chochote50/50
 
Hao sahara wameripoti kama nilivyoripoti mimi.... Lakini BBc wameshaachilia teaser ya video..... Au ujaiona hapo, au unakaza Fuvu
Bbc should give tangible/solid evidence not talks

Maneno wanayoongea hao huo sio ushahidi ni kuchafuana
Huwezi kupublish habari kama hizo kwa maelezo ya hao wahojiwa wakati hawana solid evidence

Ndio mjue hawa bbc sio chombo cha habari tena,alafu mbona tafiti zao wanahangaika na blacks only?
 
Naisubiri hiyo video, na waitoe ili kuonesha hadhi Yao ya habari.
 
Alafu mwisho wanaambiwa "Piga makofi kwa bwana yesu" [emoji23]

Yaan yesu anapewa zawadi ya makofi... saa zingine wanaimbishwa kama watoto wa chekechea, eti "Sema Ayayaaa" na wao wanasema [emoji23][emoji23][emoji23]

Kweli mwalimu wa wanawake ni kipofu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1487]
Waseme ayayaya[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Breaking News: BBC inatazamia kuchapisha nakala ya uchunguzi wa kuacha vinywa wazi inayoeleza matukio ya kikatili, Miujiza ya Kughushi, uhalifu, na ubakaji uliofanywa na Marehemu Mchungaji Temitope Balogun Joshua, almaarufu Nabii TB Joshua!!!

Kupitia page ya twitter ya Sahara Reporters wameelezea matukio aliyofanya ambayo yanatarajiwa kupostiwa na BBC katika video
View attachment 2864719

Tizama kipande hiki cha BBC wakihoji watu waliokumbwa na unabii feki wa TB Joshua....
Hii inashangaza!!! [emoji33][emoji2196][emoji2196][emoji2196][emoji100]

[emoji342] Video Credit: BBC
View attachment 2864718

TB Joshua alikuwa ni mchungaji maarufu wa Kikristo na mwanzilishi wa kanisa la Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) huko Lagos, Nigeria. Alikuwa na ushawishi mkubwa katika jamii na alihusika katika huduma za kiroho, uponyaji, na mafundisho ya Biblia. Hata hivyo, alifariki dunia mnamo Juni 2021.

Pia soma: UCHUNGUZI WA BBC: TB Joshua aliwanyanyasa na kuwabaka wafuasi wake
Binadamu wa sasa wanavyo ambiwa utapeli wa hawa manabii fake hawaelewi sijui kwanini.
Haya sasa nyie endeleeni na akina Mwamposa and Co
 
Mimi ninachojiuliza kwa nini wamesubiri kuitoa wakati ameshafariki
Ni mtu wao na wasingeweza kutoa chochote alipokuwa hai, sasa kwa kuwa amekufa ndio wanatoa ili waobekane kuwa ni wachimbuaji mahiri
 
Mimi ninachojiuliza kwa nini wamesubiri kuitoa wakati ameshafariki
Yeye alikuwa anatoa bahasha so hawa waliopo wamewapelekea clip na kuwatisha wanaitoa, nadhani wamegoma wakawaa "toeni ashakufa mwenyewe"

Si unajua waandishi na njaa 😃
 
Back
Top Bottom