Offline User
JF-Expert Member
- Dec 20, 2010
- 3,828
- 2,393
- Thread starter
-
- #21
Hii bbc bado ipo? Tangu aingizwe kayanda nilijua imebinafsishwa na tbccm
​BBC mpo! Lawama ndio hizo kuwa mnaripoti tofauti na weledi wenu wa zamani. For the first time nimesikia mmeitwa makanjanja. Hasa hao watu wapya.
Nami nahisi tangu wahamie DSM, imebinafsishwa! Sio BBC niliyoifahamu kabla! Kwao habari ni Al Shabab, Boko Hram, Ebola na ISIS
wewe waamini mbowe slaa na lissu ni redio tosha...aah nimesahau na lema yule mbunge wa arusha.Nilikuwa ninawaamini sana BBC, ila vile sijasikia wakiripoti kile kinachoendelea Dodoma siku za hivi karibuni, kweli siwaamini tena!
Tusikimbilie kuwalaumu labda masharti waliyopewa ndo hayo au kureport kinyume ila wao wameona ni bora kutoreport kabisa kuliko kureport uongo
BBC kila taarifa ni Kenya tu. Tumeacha hata kuiangalia. Hakuna taarifa za Tanzania. Wapelekeeni Wakenya au waingereza TV yenu. Salm umetuangusha sana.
wewe waamini mbowe slaa na lissu ni redio tosha...aah nimesahau na lema yule mbunge wa arusha.
Vinginevyo wana political aspiration au ni waajiriwa wa wangoa kucha au wanawaogopa wang'oa kucha wasiwadake wakiwa wanarudi nyumbani baada wa kutoa taarifa nyeti,si unajua tena wako hapa hapa dsm
Nimewahi fanyiwa mahojiano na BBC kuhusu tatizo flani hapa nchini,siku mahojiano yalipo rushwa hewani zile points zenye ukweli mchungu kwa serikali waka edit na kubakiza supporting points tu.
Nilichukia sana.
Kweli kabisa,wamebakiza habari za kisa na mkasa,hata kama hawana nauli ya kuwaleta dodoma,hata televisheni hawaangalii wakati linarushwa live? Vyuo vikuu vipo vingi lakini hata kuwahoji wahadhiri hapana,wakati wako uingereza walikuwa bize na akina lwaitama,wamehamishiwa bongo ni kimya, hivi anold kayanda aliyezoea kumuhoji juma nature atamuhoji rais wa nchi gani? Labda wa TFF, hata mwalekwa pale hapamtoshi, ni mara ya kwanza bbc inakuwa na mwandishi darasa la saba, mc wa kitchen party,labda wamchukue yule jamaa wa star tv dotto bulendu, he is a journalist heavyweight enough for the job,anaweza hata kuandaa kipindi cha review ya magazeti ya africa na ulaya
Huyu Salimu nadhani na yeye Mahakama ya Kadhi si inamuhusu?. Au huyu nae ni Sheikh Jongo?.
??? Sheikh jongoo,
Wadau,
Tangu upigaji kura wa rasimu ya katiba kuanza, nimegundua kuna hivi vyombo viwili vya habari vya kimataifa (Radio) vimekua na misimamo tofauti. Huku DW ikituhabarisha kile kinachoendelea Dodoma kinagaubaga ikiwa ni pamoja na vitisho walivyopewa baadhi ya wajumbe waliopiga kura za Hapana, hali imekuwa tofauti kwa BBC ambao hawariporti kabisa kuhusu BMK! Je pengine BBC wametishwa kwa vile baadhi ya matangazo yao yamehamishiwa DSM? Source ni mimi mwenyewe ninayefuatilia matangazo yao kwa ukaribu!
Yawezekana wanahabari waliowapata kwa Tanzania ni magamba...so usishangae kwa nn bbc hairiport...Kikeke na Hilary ipi ni sahihi!