BBC vs DW kuhusu Bunge Maalum la Katiba (BMK)

BBC vs DW kuhusu Bunge Maalum la Katiba (BMK)

Offline User

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
3,828
Reaction score
2,393
Wadau,

Tangu upigaji kura wa rasimu ya katiba kuanza, nimegundua kuna hivi vyombo viwili vya habari vya kimataifa (Radio) vimekua na misimamo tofauti.

Huku DW ikituhabarisha kile kinachoendelea Dodoma kinagaubaga ikiwa ni pamoja na vitisho walivyopewa baadhi ya wajumbe waliopiga kura za Hapana, hali imekuwa tofauti kwa BBC ambao hawariporti kabisa kuhusu BMK! Je pengine BBC wametishwa kwa vile baadhi ya matangazo yao yamehamishiwa DSM?

Source ni mimi mwenyewe ninayefuatilia matangazo yao kwa ukaribu!
 
...bbc walisha tishwa kufungiwa,isitoshe tayari wabongo wamejaa wanaendeleza kasumba ya vyombo vya bongo...
 
Yawezekana wanahabari waliowapata kwa Tanzania ni magamba...so usishangae kwa nn bbc hairiport...Kikeke na Hilary ipi ni sahihi!
 
BBC kila taarifa ni Kenya tu. Tumeacha hata kuiangalia. Hakuna taarifa za Tanzania. Wapelekeeni Wakenya au waingereza TV yenu. Salm umetuangusha sana.
 
...bbc walisha tishwa kufungiwa,isitoshe tayari wabongo wamejaa wanaendeleza kasumba ya vyombo vya bongo...

Kweli kuwajaza akina, Kayanda, Baruan Muhuza, Regina Muziwanda imekua na sura ya kibongo hasa! Inapoteza mvuto!
 
Yawezekana wanahabari waliowapata kwa Tanzania ni magamba...so usishangae kwa nn bbc hairiport...Kikeke na Hilary ipi ni sahihi!

Hapo niliongelea hasa upande wa Radio mkuu! Akina Kikeke na Hilary ile ni habari nyingine kabisa!
 
Kwa kweli mkuu afadhali umewka uzi huu. Huo nasikiliza BBC asubuhi hazungumzi chochote kuhusu BMK. Hivi kweli chombo hiki cha habari hakioni umuhimu wa kutupasha na kuchambua mambo yanavyoendelea dodoma?. Tutawakumbuka sana watu sampuli ya akina TIDO MHANDO. Kukosekana kwao tunakosa uhondo wa habari. BBC ya sasa sitofautishi kabisa na any local broadcasting media.
 
BBC wamekuwa kimya kuhusu habari za TZ, hasa tangu wafungue studio dar! Wanacho nipatia sicho nilicho kitarajia! Habari za BMK ndo haziguswi kabsaaaa!. Bora bbc ya akina ntetema enzi hizo.
 
mnategemea nn kama bbc inachukua hadi wahuni wa clouds fm hamna kitu pale
 
Pia DW ina wazanzibar wengi ambao kimsingi ni wadadisi wa mambo

mcubic unachosema ni kweli! DW bado inao wakongwe wa tangu enzi hizo na umahiri wao wa habari unajulikana. BBC wakongwe hawapo tena bali wamejanza makanjanja tu ambao uwezo wao tunaujua-fikra finyu! Wanatuletea ushabiki ule ule wa Clouds FM, RFA et al! Kweli imepoteza mvuto!
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli mkuu afadhali umewka uzi huu. Huo nasikiliza BBC asubuhi hazungumzi chochote kuhusu BMK. Hivi kweli chombo hiki cha habari hakioni umuhimu wa kutupasha na kuchambua mambo yanavyoendelea dodoma?. Tutawakumbuka sana watu sampuli ya akina TIDO MHANDO. Kukosekana kwao tunakosa uhondo wa habari. BBC ya sasa sitofautishi kabisa na any local broadcasting media.

Heri nisikilize kipindi cha "patapata" Wapo redio, napata habari za uhakika kwa wakati!
 
Hii bbc bado ipo? Tangu aingizwe kayanda nilijua imebinafsishwa na tbccm
 
Na mimi huwa nashangaa BBC ya leo, hakuna habari ya maana inayorushwa toka Tanzania! Kimekuwa ni chombo cha propaganda cha "wenye imani kali"- Fuatilieni kwa makini mtagundua ukweli.
 
​BBC mpo! Lawama ndio hizo kuwa mnaripoti tofauti na weledi wenu wa zamani. For the first time nimesikia mmeitwa makanjanja. Hasa hao watu wapya.
 
Back
Top Bottom