BBC waendeleza ubeberu: Eti Tanzania nchi ya 23 kijeshi Afrika, Uganda ya 14 na Kenya ya 12

Uko sawa kabisa mkuu,jeshi gani linashabikia chama cha kipumbavu kama CCM? JWTZ ni Tawi la CCM siyo jeshi imara kabisa
 
hii siyo ajabu ndugu yangu.kwani mbona tunaambiwa Tanzania ni kisiwa cha amani lakini ni jambo la kushangaza kwenye listi ya nchi 50 zenye amani dunianiTanzania haipo .Tuendelee kuishi kwa matumaini
Kumbe tunadanganywa?
 
Kenya no doubts, hakuna nguvu za kijeshi bila uchumi imara
 
Bro safi sana. Leo nilitaka nimtafute mchambuzi anifafanulie ishu ya Tigray bahati mbaya mambo yakawa mengi. Kama hutajali fungua hata uzi tufahamu huo mgogoro wa Tigray ulivyo. Mawazo yangu yananipeleka nidhani mgogoro wa Tigray ni kama wa Rohingya
 
JWTZ ni jeshi imara kwa sababu ya intelijensia yake. Ni jeshi lililoweza kuzuia majaribio mengi ya uasi na uvunjifu wa amani. Huu upumbavu wa kusema tafiti hupingwa kwa tafiti ifike mahala uachwe. Waliokuja na hii kauli ya tafiti hupingwa kwa tafiti ndo walituambia mzungu Rebman aligundua Mlima Kilimanjaro. BBC ni wa kupuuzwa kwasababu wana nia ovu. Adhabu ya hao BBC ni kukaliwa tu kimya na kuwaona kama wendawazimu. Kwa mission ambazo JWTZ imezifanya za ukombozi Afrika itoshe kusema ni jeshi imara la kuaminika. Kaburu kasumbuana sana na JWTZ. Watanzania wengi bado wana imani na JWTZ. Ni miongoni mwa taasisi chache za nchi ambazo zinaheshimika na kuaminika.
 
Nguvu sio weledi, unaweza kuwa na jeshi kubwa hakuna weledi. Wingi wa vifaa, wingi wa askari hauwezi kufidia ukosefu wa weledi.
 
Kweli ubeberu mtupu. Ni misinformation. Nimeonda wakongo wakitamba eti nchi yao jeshi imara namba 10. Jeshi la ovyo kama drc rushwa imetawala na majenerali feki wanaotokana na waasi wa maimai na wa kitutsi m23.
 
Nguvu za jeshi la nchi halipimwi kwa vita ilizoshinda, bali kwa vifaa vya kivita ilivyonavyo. Kama nguvu ya jeshi ingekuwa inapimwa kwa vita ilizoshinda, chna isingekuwa ya pili au tatu, maana zaidi ya vita ya wao kwa wao haijapingana vita yoyote muhimu.
 
You have hit the nail on the head. Huwa najiuliza Sana ikatokea Hamza hamsini wameingia mtaani au kwenye soko Kama la kariakoo itakuaje?
Hapo ndgu yangu umesema uongo. Ungesema police na siasa ningekuunga mkono, lakini siyo jeshi. Ngoja nikimbie kwa daktari mizii, nitaongezea baadaye.
 
Tigray anaelekea kushindwa,mkuu.
 
Matifa wanayoyaangalia ni yale yaliyofanya biashara ya kununua silaha waziwazi na kumbukumbu zipo wazi lakini Tz Mtindo wake wa ununuzi wa zana za vita upo kisiri sana hivyo hawana takwimu
 
Matifa wanayoyaangalia ni yale yaliyofanya biashara ya kununua silaha waziwazi na kumbukumbu zipo wazi lakini Tz Mtindo wake wa ununuzi wa zana za vita upo kisiri sana hivyo hawana takwimu
ni jambo jema kuwa na usiri ktk silaha na mbinu za kivita kwa ujumla.ila naona maonyesho ya majeshi yetu wakati wa sikukuu ya UHURU ni mambo yalopitwa na wakati sana.kwa mfano kuvunja matofali,kubeba mavitu mazito,kutembea kwenye kamba nk.ni vizuri jeshi letu lingejikita kwenye TECHNOLOGIES .siku ya sherehe ya uhuru waje na maonyesho ya TECHNOLOGY,
kwa mfano wanaweza kuwa viwanda vya kuzalisha silaha hapa Tz,viwanda vya magari , tractors, electronic surveillance, computer technologies nk.hii itajenga jeshi imara lenye ubunifu wa hali ya juu ktk technologies na kusaidia kukuza na kuendeleza viwanda Tz,
 
Vipi wametoa list ya kijeshi Ulaya?
Maana Uingereza sio ya kwanza.
 
Weka hapa link ya hiyo habari, halafu tuwekee hapa utafiti wako
 
M Mbona mtandao wa GLOBAL FIRE POWER unaonyesha hivyo hivyo, kuwa Tz ni ya 23 kwa nguvu za KIJESHI Afrika?

 
Tuombe vita ya kirafiki baina ya nchi na nchi final tujue nchi ipi inaongoza kijeshi.
 
Ni kweli maana jeshi letu siku wakisema wapigane vita watakaopigana ni robo yao tuu maana wengi watapiga simu kwa baba zao ambao ndo wakuu ,hili jeshi ni wamejaa wala mshahara watoto wao wenyewe jeshi ni la kisiasa aliajiri vijana wazarendo ambao wapo tayari badala yake nawfasi wanapewa wakuu ili waweke nduguzao

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…