BBC waipongeza JamiiForums, wadai ndio tegemeo pekee la habari za uhakika nchini Tanzania, wampongeza Melo na watendaji wake

BBC waipongeza JamiiForums, wadai ndio tegemeo pekee la habari za uhakika nchini Tanzania, wampongeza Melo na watendaji wake

Magu na lile genge lake la kijani huko waliko watakuwa wameumia sana kusikia hizi habari.

Sasa hivi utasikia JF ni wakwepa kodi na wahujumu uchumi, genge la mabeberu nk.
Wamiliki wake watakamatwa na watachakaa kwa kukaa rumande. Kama huamini wewe subiri tu.
Kwani Jf ni wanasiasa?
 
Ni kweli chombo pekee huru cha habari kilichobaki Tanzania ni JamiiForums.

Ambapo ni vigumu kununulika maana kuna mamia ya watu huru walio member na wageni wanaochangia mada bila hofu yoyote.

Vyombo vingine ama vimenunulika kusifia au vimeamua kujiweka mbali na habari ambazo wanahisi zitawaudhi watawala.

Mfano ni vigumu vyombo vya habari kufanya taarifa za uchunguzi, kuhoji au kukumbushia matukio yanayoiannika serikali kweupe.

Mfano vyombo vya media wataripoti wabunge wa CHADEMA ni watoro Bungeni bila kukumbushia kuwa wamefunguliwa kesi nyingi za utata na utawala wa awamu ya 5 ili wasiweze kuwepo Bungeni kwa muda mrefu.

Lakini JamiiForums habari kama hiyo ya 'watoro' wataongeza na angalizo, historia , video clips ,matamko ya watawala n.k ndiyo yamewafanya wapinzani kuwepo ktk hali ngumu na hatari kisiasa.
Hivi kati ya Jf na Twitter wapi pana freedom of expression ?
 
Wanatapatapa
Magu na lile genge lake la kijani huko waliko watakuwa wameumia sana kusikia hizi habari.

Sasa hivi utasikia JF ni wakwepa kodi na wahujumu uchumi, genge la mabeberu nk.
Wamiliki wake watakamatwa na watachakaa kwa kukaa rumande. Kama huamini wewe subiri tu.
 
BBC wameipongeza JamiiForums kwa kuwa kimbilio la wananchi kupata habari za ukweli na uhakika

Sasa Maxence Melo anahojiwa mubashara kuhusu tuzo anayoipokea nchini Marekani.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia
Muda huo-hjo wewe na wenzako hapo Lumumba mkiongozwa na Musiba mnatafuta namna ya kuifutilia mbali JF
 
Hizi chanel nyingine zinaishi kwa vitisho ndo maana kwa sasa zote zimejikita kwenye kusifia sifia tu.TUMECHOKA KILA KONA KUNA WATU WANALISIFIA MBAYA ZAIDI WANAOMSIFIA WAO PIA WAMEKUNJA SURA INA MAANA WANALAZIMIKA TU.
 
Habari,
Shujaa wetu wa Jamii Forums Mexemo Mero, jioni hii ametoka kuongea na BBC na miongoni mwa yale aliozungumzia ni pamoja na Tuzo ya uwanahabari uliotukuka inayotolewa leo hii huko New York Marekani na taasisi ya CPJ anakabidhiwa leo hii.

Pia amezungumzia changamoto za vyombo vya habari nchini kwetu Tanzania ikiwemo: vyombo vya dora kuwakamata ovyo wanahabari.

Sheria zinazowabana wanahabari.
Yeye mwenyewe ameenda mahakamani mara 137. Ameshitakiwa mara 80. Na sasa ana kesi tatu moja ikiwa imefungwa.
Nini kifanyike: amesema sheria ziboreshwe

Ulinzi na usalama ujue upo kwa ajili ya kuwalinda waandishi sio kuwapa kesi.
Watendaji serikalini watoe ushirikiano kwa waandishi wa habari.

MIMI NAMPA HONGERA , PIA NA WANAJAMII WOTE KWA TUZO HIYO YA KIMATAIFA.
 
Hongera zake kwa hatua hiyo

Sisi wote tunaifanya jf iwe Sehemu ya Mijadala ya kujenga Taifa
 
Back
Top Bottom