Ni kweli chombo pekee huru cha habari kilichobaki Tanzania ni JamiiForums.
Ambapo ni vigumu kununulika maana kuna mamia ya watu huru walio member na wageni wanaochangia mada bila hofu yoyote.
Vyombo vingine ama vimenunulika kusifia au vimeamua kujiweka mbali na habari ambazo wanahisi zitawaudhi watawala.
Mfano ni vigumu vyombo vya habari kufanya taarifa za uchunguzi, kuhoji au kukumbushia matukio yanayoiannika serikali kweupe.
Mfano vyombo vya media wataripoti wabunge wa CHADEMA ni watoro Bungeni bila kukumbushia kuwa wamefunguliwa kesi nyingi za utata na utawala wa awamu ya 5 ili wasiweze kuwepo Bungeni kwa muda mrefu.
Lakini JamiiForums habari kama hiyo ya 'watoro' wataongeza na angalizo, historia , video clips ,matamko ya watawala n.k ndiyo yamewafanya wapinzani kuwepo ktk hali ngumu na hatari kisiasa.