BBC waipongeza JamiiForums, wadai ndio tegemeo pekee la habari za uhakika nchini Tanzania, wampongeza Melo na watendaji wake

BBC waipongeza JamiiForums, wadai ndio tegemeo pekee la habari za uhakika nchini Tanzania, wampongeza Melo na watendaji wake

Nimefurahi sana kuona BBC wametoa hiyo habari ya Mello kupata hiyo tuzo. Ukweli ni kuwa JF ndio chombo pekee cha habari hapa nchini kilichobaki kutoa habari kwa uhuru. Huku jf ndio pekee maoni yako balanced na kila mtu yuko huru kuchangia. Hongera sana Mello kwa kututoa kimasomaso wanajf.
 
Kumbe na Maxence ni muandishi wa habari, sikujua hili. Nimesoma post ikizunguka kusema wasio wasomi wa habari hawatakiwi kufanya kazi hiyo, hii ni baada ya msanii Steve Nyerere wa Filamu kutangaza EFM.
 
Hongera sana kaka Maxence Melo kwa hiyo tuzo na kuonana na raisi wa Marekani Trump
Ombi langu kwako ujitaidi jf app iwe na version Kama ya Twitter ila baki kuwa kama jf dare talk more
 
Nashukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa kuniwezesha kuishi vema bila hofu ya kuugua kula cha mtu na kulala muda muafaka hongereni sana
Ccc NAKWEDE
 
BBC wameipongeza JamiiForums kwa kuwa kimbilio la wananchi kupata habari za ukweli na uhakika

Sasa Maxence Melo anahojiwa mubashara kuhusu tuzo anayoipokea nchini Marekani.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia
Kiongozi wa malaika hatofurahishwa na hii habari
 
Hongera zake kwa hatua hiyo

Sisi wote tunaifanya jf iwe Sehemu ya Mijadala ya kujenga Taifa

Mmenajisi vyombo vingine vyote vya habari watu wengi hawaangalii tena maana vimegeuka kusifia tu. Hata hii jf ni kwasababu huyo Mello amegoma tu kumsujudu shetani na mambo yake yote. Hata ww uko huku humu lakini hupati raha maana huku hamna sifa za kinafiki, na ukisifia ujinga unapewa kubwa yako.
 
Pia Mex apunguze uoga wakutufutia nyuzi zenye mvuto wakisiasa hasa zinazo guza vigogo na mtakatifu, na kuacha za mapenzi kama "kula tunda kimasihara"......... always freedom fighter don't fear death or jail....big up mex...
Naunga mkono hoja ,jamii forum wanafuta Sana nyuzi ,komaeni acheni woga achieni nyuzi.
 
Jamani wana Jf nasi tumuandalie Tuzo maalumu ndugu Maxmelo anafanya kazi kubwa sana ya kulinda faragha za members vinginevyo akina Johnbabtist wangesha washudhurikia wakosoaji wengi sana
 
Ni kweli chombo pekee huru cha habari kilichobaki Tanzania ni JamiiForums.

Ambapo ni vigumu kununulika maana kuna mamia ya watu huru walio member na wageni wanaochangia mada bila hofu yoyote.

Vyombo vingine ama vimenunulika kusifia au vimeamua kujiweka mbali na habari ambazo wanahisi zitawaudhi watawala.

Mfano ni vigumu vyombo vya habari kufanya taarifa za uchunguzi, kuhoji au kukumbushia matukio yanayoiannika serikali kweupe.

Mfano vyombo vya media wataripoti wabunge wa CHADEMA ni watoro Bungeni bila kukumbushia kuwa wamefunguliwa kesi nyingi za utata na utawala wa awamu ya 5 ili wasiweze kuwepo Bungeni kwa muda mrefu.

Lakini JamiiForums habari kama hiyo ya 'watoro' wataongeza na angalizo, historia , video clips ,matamko ya watawala n.k ndiyo yamewafanya wapinzani kuwepo ktk hali ngumu na hatari kisiasa.

Vipi Tanzania Daima. Ni chombo Huru
 
Wacha uongo Bagamoyyo ni mara ngapi tumeandika hapa kwamba Jamii Forum imenunuliwa, umbeya huo.
 
Hivi hiyo tuzo aliyopata, kuna chombo chochote cha habari cha ndani kinaweza fanya mahojiano naye? Au hata hilo wanaliogopa?
 
Mungu ni mwema, tunaendelea kumwomba ailinde JF, pamoja na misukosuko mingi sana anayoipata Maxence Melo.

Mungu mbariki Melo, Mungu ibariki JF
 
Mabeberu nayo yameanza undumila si yanasema hakuna uhuru wa habari sasa JF inaripotia kwenye ardhi ya bbc .inabidi yakanushe madai yao
 
Kiongozi bado upo ccm?

Umechange ghafla Sana na kuanza kutumia akili kufikiri

Kwa sasa umeanza kuwa mwana taaluma na mtu wa kufanya analysis

Umeuvua uchama, Ni salama huko ccm kweli?

Hapa Jf ulionekana ni mtu ambaye akili yako imeshikwa na umebaki kopo tupu

Ulikuwa mtu uliyekufa kifikra siku nyingi ingawa mwili wako ulikuwa unaishi, umepatwa na nini?
Huenda kuna msigano wa kimaslahi ama kuna "makwazo ambayo hayakutarajiwa" katika kuunga juhudi...
 
Back
Top Bottom