BBT waanza mafunzo, hii ni safari ya kuelekea katika kilimo cha biashara

Serikali iache siasa, tatizo la wakulima nchini ni MITAJI NA MASOKO. Ijikite kutatua hilo
Mitaji inatolewa kwa wakulima na riba imepungua pia masoko yapo ya kutosha nje ya nchi kipindi hiki cha uongozi wa Rais Samia Suluhu kilimo kimepewa kipaumbele na kuna dalili zote za wakulima wengi kuwa matajiri wakubwa maana pembejeo za kilimo zinapatikana kwa gharama ndogo sana na wanauza mazao kwa bei ya juu na sio bei ya kupangiwa
 
Watanzania tuna kasumba kubwa sana kwenye kutoa vitu kutoka kwenye makaratasi/mahubiri kwenda kwenye uhalisia na vitu vikaonekana vile vinavyohubiriwa tuko vyema sana kwenye kufanya siasa na kupiga mdomo zaidi ya vitendo, ndio maana jirani zetu Wakenya hawaishi kutusema kuwa sisi tuko na Kiswahili kingi lakini utendaji hakuna na ukitazama hili ni kweli kwenye utendaji ukipima wenzetu wako mbali sana na wanachapa kazi kweli sio masihara nafikiri sababu ya mila na tamaduni zao za kutoendekeza uzembe katika kazi.
 
kwaiyo tukae hapa tusubiri jinsi vijana wengi watakavyonufaika na kilimo
Vijana wangenufaika kama kila kijana angeingia kwenye kilimo ktk eneo analoishi siyo asubiri kuhamishwa na serikali kwenda sehemu nyingine. Hii ni ajira kwa mgongo wa nyuma. Na tunataka vijana wajiajiri siyo waajiriwe.
 
Are you serious?
 
Nioneshe hata kitu kimoja Cha maana ambacho CCM wamewahi kufanikiwa?
 
💯 Correct question!.
 
....ingefaa kutolewa zaidi mashuleni kilimo kikipewa kipaumbele kama sehemu ya mafunzo ya lazima kwa vijana.....
 
Product km hii imekuwa ikifanywa na SUGECO kwa kuwagharamikia vijana kwenye mafunzo ya kilimo na ufugaji huko Rufiji bad enough vijana wanaopata nafasi hakuna wanachokifanya baada ya kutoka huko
 
Mitaji inatolewa wapi ndugu? Bank ya kilimo imejaa ukiritimba wana zaidi ya mwaka sasa wanafuatilia mikopo yao bila mafanikio, acheni siasa na porojo kwenye mambo ya msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…