Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Aaha kumbe ukienda kununua Kuna doc unapewa za utangulizi kujua condition ya gari??? Lakini nadhani kampuni ingekuwa inawapa doc wateja bila kuulizwaa..
hapa sasa kwenye hali kama hii inabaki serikali yetu kupitia mamlaka zake kuhakikisha raia wake hawaingizwi kingi kwa kufanya vitu kama hivi viwe vya lazima, mimi naamini nchi za wenzetu kudhulumu watu hata kama mtu hana uelewa ni ngumu kwa sababu kabla kujamuingiza mtu kingi unakua umekutana na mamlaka zao
 
kwani yard za magari yale ni mapambo wameweka? tabu yote ya nini kuagiza gari toka nje. ulimbukeni na ushamba tu. watu weusi bado ni warugaruga ila mnatofautiana viwango vya urugaruga. umejitakia.
 
Huyo ujuaji umemponza ofc za beforwad Tanzania zipo posta kwanini yeye awasiliana na ma agent wa sehemu nyingine alafu jumba bovu uwape watu wa nchi yako..
 
kwani yard za magari yale ni mapambo wameweka? tabu yote ya nini kuagiza gari toka nje. ulimbukeni na ushamba tu. watu weusi bado ni warugaruga ila mnatofautiana viwango vya urugaruga. umejitakia.

Hata wewe inaonekana ni mshamba pia ingawa unajiona mjanja. Gari za yard hapa bongo asilimia 80 wameshachezea mileage na bei ziko juu.
Na nia yangu ni kukuambia kabla hujamcheka mwenzio au kumuona boya kuwa mnyenyekevu na msaidie. Usifikiri tunaoagiza nje hatuzioni yard au tunaleta ujuaji. Binafsi nishaagiza gari kama 5 Japan(2 hazikuwa zangu) na zote sijajuta. Muhimu kujua unachofanya.
Tusaidiane badala ya kuchekana.
 
ningekua sirikali ningepiga marufuku kuagiza magari mnatujazia matakataka. ukiagiza uagize gari mpya. mnunue za yard ziishe. huo utafiti wako wa 80% umetoa wapi? tafuta fundi makini nenda naye afanye kazi yake ya ukaguzi uchomoe chombo.
 
Mkuu kama hutojali hiyo website iweke hapa jukwaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…