Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Mimi nahisi Singapore nao wananunua magari used kutoka Japan, wakiyachoka wanayauza na wao!

Hivi Wajapan wenyewe orijino wanaweza kuwa matapeli tapeli mana wanasifika kwa kufanya kazi na umakini? Au watakuwa wamefundishwa utapeli na Waafrika ambao wameweka makazi yao huko Japan?
 
Kuagiza ni Bora zaidi SEMA kama hujui uliza maana Kuna website ukiingiza you chasis numba unapata full history ya gari hasa kwa zilizopo Japan
Gari imesajiliwa lini
Imeshamilikiwa na watu wangapi
Accident history
Km ilizoingia nazo kwenye auction
Grade iliyopewa
Service history
Aina ya matumizi iliyokuwa inafanya(town trip or high way)
Hiyo gari ninauhakika hiyo engine huwenda ilibadilishwa maana engine za 2az za chino ya 2005 zilikuwa na shida ya nati kati ya Brock na cylinder head kufunga Kwa mizunguko michache hivyo kuleta tatizo la kuachia kutokana na compression ya engine hata ukaze vipi
Hiyo gari imeharibiwa na mafundi uchwara gear box haikuwa na shida
Hapo ilibidi kupeleka block engineering lakini sio reliable au ununue block ila hakikisha imetengenezwa zaidi ya 2005/6
Pia badili oxygen air sensor pia inachangia gari kukosa nguvu
 
ningekua sirikali ningepiga marufuku kuagiza magari mnatujazia matakataka. ukiagiza uagize gari mpya. mnunue za yard ziishe. huo utafiti wako wa 80% umetoa wapi? tafuta fundi makini nenda naye afanye kazi yake ya ukaguzi uchomoe chombo.
Ukutane na grade R
 
Mimi nahisi Singapore nao wananunua magari used kutoka Japan, wakiyachoka wanayauza na wao!

Hivi Wajapan wenyewe orijino wanaweza kuwa matapeli tapeli mana wanasifika kwa kufanya kazi na umakini? Au watakuwa wamefundishwa utapeli na Waafrika ambao wameweka makazi yao huko Japan?
Huwezi tapeliwa Japan
Tena kama ni member wa JUMVEA unafungiwa Moja Kwa Moja kufanya biashara
 
Ni ya 2014, gari haiwezi kwenda hata Kariakoo inachemsha! Naomba ushari nifanyeje na hii gari. Je Toyoto Tanzania wanaweza nisaidia, maana gereji za mitaani hii imewashinda
How so? Yani gari inamshindaje fundi? Hauna service manual ya hiyo gari? Ni mechanical au electrical issue?

Mnableed coolant vizuri kutoa air bubbles?
Thermostat inafanya kazi?
Cylinder head na gasket vimepimwa?
Radiator haijaziba au kupata tatzo? Maana unebadilisha gearbox, je coolant ilichanyika na gearbox oil?
Mfuniko wa radiator unahifadhi nakuachia pressure?
Feni zinafungua ipasavyo?
 
Mimi nahisi Singapore nao wananunua magari used kutoka Japan, wakiyachoka wanayauza na wao!

Hivi Wajapan wenyewe orijino wanaweza kuwa matapeli tapeli mana wanasifika kwa kufanya kazi na umakini? Au watakuwa wamefundishwa utapeli na Waafrika ambao wameweka makazi yao huko Japan?
Watu wana sikia singapore ndogo barabara zote lami afu magari hayali mileage kubwa[emoji81][emoji81]kumbeee
 
Nikiangalia Majibu ya Mtoa Mada inaonekana ana kaujuaji flani na kaubishi(Samahani kama yatakuwa maneno siyo Sahihi).
Next time watumie SBT hata kama gari ina minor scratch wanakwambia na huwa wanakupa Account manager wako na customer care nzuri sana hatua kwa hatua anakupa mrejesho.

Note: Gari za Singapore ni hatari kwa afya yako watu washaongea sana humu ila wabongo huwa wabishi hatutakagi kuelewa pia hatupendi kujifunza.​
 
ningekua sirikali ningepiga marufuku kuagiza magari mnatujazia matakataka. ukiagiza uagize gari mpya. mnunue za yard ziishe. huo utafiti wako wa 80% umetoa wapi? tafuta fundi makini nenda naye afanye kazi yake ya ukaguzi uchomoe chombo.

Yani kwenye soko huria, dunia ya leo Serikali ilete biashara za kuchaguliana pa kununua vitu?! Serikali ishaweka mifumo ya kukagua magari kabla hayajaletwa nchini. Kama ni kuishauri Serikali ni bora kuishauri isimamie ufanisi kwenye ukaguzi wa magari kabla hayajaja na si kuanza kutengeneza mazingira ya wachache kuwa na kauli kwenye soko.
Sirudii kusema mengi yanachezewa ili kuharibu biashara za watu ila ‘buyer beware’
Kama unajua unachokifanya, kuagiza inaweza kuwa bora zaidi kwa mazingira ya biashara zilivyo sasa. Kujua unachofanya ni pamoja na kujua uchague gari gani, ununue wapi na vitu gani vya kuwa navyo makini. Ukijua hili utaokoa pesa yako nyingi tu
 
I have a friend ambaye mwaka jana alikuwa anataka gari. Nikamuelekeza aangalie kwenye site ya Be Forward. Alipata gari atakayo ila ikawa ni ya Singapore (huwa zimeandikwa THIRD PARTY SELLER). Nikamwambia aachane na ya Singapore.

Akapata nyingine ya Japan na nikamuelekeza aende kwenye ofisi za Be Forward (Dar).

Kule ofisini, agent aliyekuwa anamuelekeza akamwambia aachane na ya Singapore kwa sababu hakuna mkaguzi huko. Akiichukua hivyo hivyo inaweza kuwa mbovu na hatoambiwa.
 
Back
Top Bottom