Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

TCV Wana magari mazuri ila watu hawajui tu

TCV ni dalali, ila sina hakika kama ana gari zao pia au zote ni hizo anazowela za kampuni nyingine. gari nyingi ukienda kwenye mitandao ambayo wanatoa hizo gari unakuta bei zimepoa kidogo. Kwa mfano utakuta wanatoa gari realmotor japan, sbi motor, enhance auto n.k. Ila kama wana guarantee ubora na usalama nayo ni option.
 
Gari mpaka kufika 26M, mbali ya ushuru. Ilipofika tu service kwenye yard ya Be Forward ilikwenda zaidi ya 250,000 maana TBS walikataa kurelease gari. Baada ya gari kutoka nimelipeleka gereji nyingi sana na nimetumia zaidi ya 10,000,000 kujaribu kulirepair lakini wapi. Mpaka nilinunua Gear Box mpya lakini wapi.!
Mmmmmmhmn 10milion mbona ni hela nyingi sana mzee?
 
Gari mpaka kufika 26M, mbali ya ushuru. Ilipofika tu service kwenye yard ya Be Forward ilikwenda zaidi ya 250,000 maana TBS walikataa kurelease gari. Baada ya gari kutoka nimelipeleka gereji nyingi sana na nimetumia zaidi ya 10,000,000 kujaribu kulirepair lakini wapi. Mpaka nilinunua Gear Box mpya lakini wapi.!
Noma Sana.
 
Suala sio bei, hizo zote ni gari zipo kwenye kampuni ya Be forward. Singapore ni tawi la Beforward na wale ni wao wenyewe. Hata pesa nillipa kupitia account ya Be forward Japan. Na kama gari wameona ina shida kwanini hawakuandika kwenye statement yao au kwenye mawasiliano niliyodanya nao watu wa Japan???
Screenshot hayo mawasiliano, halafu weka sawa na rekodi zako za gharama ulizoingia, kisha nenda kwa mwanasheria ambaye yupo vema kwenye international laws akupe ushauri wa namna ya kudai fidia yako sababu huo ni utapeli wa mchana kweupe.
 
Ndio hivyo na gari ipo juu ya mawe, inaniumiza sana. Mbaya zaidi Be forward hawakutaka kunisaidia kwa lolote. Imenikatisha sana tamaa ya kutumia Be forward, na sifahamu sana mitandao mingine ambayo ni genuine ya kuagiza magari
Andaa viambatabishi kwa ushahidi halafu katafute wakili mzuri ambaye anaweza kukuwakilisha kisheria ukafungue madai upewe fidia kama sio kurudishiwa pesa yako wakutafutie gari mpya nzuri ambayo itakaguliwa na kuwa na viwango. Na hapo wakushitakiwa ni Be forward sababu uliagizia kupitia brand yao na sio wengine.
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Aaha kumbe ukienda kununua Kuna doc unapewa za utangulizi kujua condition ya gari??? Lakini nadhani kampuni ingekuwa inawapa doc wateja bila kuulizwaa..
Muda mwingine unakuta details za hizo documents zinawakosesha biashara wanaona bora kutozitoa kabisa.


Kwa mfano, disclosure ya taarifa iseme gari ilishawahi kupigwa banzi ikafanyiwa service kubwa na kunyooshwa wewe mteja utanunua hiyo gari?

Hata kama inaonekana imesimama wima kama mnara.
 
Pole sana mkuu sikuhizi ushindani ni mkubwa sana sie wengine tumeamua kabisa kuwa na watu wetu japan kwa ajili ya kukagua gari moja kwa moja.

Pili kuna documents ulinyimwa iwe ni kwa kutokujua au kwa kujua na mwisho alphard kwa singapore mpka inafika dar inaweza kufikia mpka 22m au hata 18m sababu gari za kule nyingi ni low ended car mtu akiagiza gar singapore ana tofauti ndogo sana na aliyeagiza gari Zanzibar.

Mwisho kama ni mkazi wa dar ziko kampuni nyingi sana sku hizi zinauza magari hapa hapa dar kwa bei kama ya japan unakagua chuma yako unajiridhisha unatumia ipo alphard ofisini hapa mwaka 2007 ungekuwa na 25m tungekupa au kama utaongeza hela tuje ikagua hyo yako tuvunje uongeze hela tukupe hii
Mleta uzi, njoo hapa kuna jambo lako.
 
Ni ya 2014, gari haiwezi kwenda hata Kariakoo inachemsha! Naomba ushari nifanyeje na hii gari. Je Toyoto Tanzania wanaweza nisaidia, maana gereji za mitaani hii imewashinda
But umefanya service ya aina gani hadi imefikia 10+ milioni?

Hapo me nadhani ungeshusha engine na gear box ukafunga vipya basi gari ingekuwa mukide.

Kitu watanzania wanapenda ni service za kitapeli za mafundi wetu za kukuaminisha kuwa wanaweza kufumua engine na kuinyoosha kumbe wajanja wanakutajia magonjwa nusu nusu na gari haitapona mwisho wa siku ukijumlisha umetumia kiasi gani unakuta mkeka unasoma mamilioni.

Cha msingi ukiona gari inazingua engine sijui gear box. Tafuta pesa agizia engine na gear box kutoka huko japan au Dubai moja kwa moja. Ilete toa zile za zamani kwenye gari weka store funga hizi mpya gari inakuwa kama mpya unaitumia kwa raha kabisa.

Haya mambo ya kusumbuana na service za kufunga na kufungua engine na hawa mafundi uchwara ambao wanajua kabisa shida ni nini ila wanakuchezea akili utapoteza muda hadi ukome.
 
Mkuu, unataka kupeleka Toyota Tanzania? No way.. Kwa humu JF namjua fundi mmoja mzuri sana JituMirabaMinne ungeanza nae. Kwasababu gari la kisasa 2014 lazima lifanyiwe diagnosis. Na yeye ni Master.
Diagnosis gani unahitaji baada ya kujua gari imeshapigwa rangi kwa kurudiwa, engine inavuja oil.

Hapo mimi sihitaji diagnosis kujua gari nimepigwa.
 
Ndugu yangu.....nimezunguka gereji nyingi, inaonekana hizi version zinawasumbua mafundi wengi. Kila mtu anasema lake, mpaka nimenunua gear box mpya 800,000 na bado gari haijapona! Ndio maana nikaona labda niende Toyota Tanzania. Kama kuna fundi anaweza niashukuru
Toyota inakusumbuaje mzee, kuna gari za kusumbua sio toyota mzee.
 
Don’t buy used car from Be Forward..!! Gari zao zimechoka sana sana, wanaziosha na kuzipiga polish na little maintenance alafu wanakwambia iko vizuri sana, ujue Be Forward ni ya Mkinga mtanzania yuko Japan, kusema ukweli, magari mengi mno ya Be Forward ni mabovu sana na customer care yao mbovu sana..

I always buy cars from Japan kwa kufuata mwenyewe huko Japan au kupitia mitandao kama SBT Tz au TCV etc..!!
Mmmmmmhmn we utakuwa umetumwa sio bure. Magari karibia 70% yanayoingia bongo ni kupitia beforwad company, sasa mwenzetu sijui walikukosea nini?
 
Nashukuru mkuu, nitatfuta SBT na TCV nione option zake. Je hao wana ofisi hapa TZ?? Maana Be forward wapo Kariakoo na Posta na baadhi ya mikoa, ila huduma zao ni mbaya sana. Inasikitisha
Beforwad wapo vema sana na ndie car dealerships kubwa kwa hapa Tanzania ukilinganisha na wengine wote.

Nadhani ulichopitia ni matokeo ya kukosa consultant mzuri wa beforwad ambaye alitakuwa kukulinda. Ungeenda kwenye ofisi zao before haujaagiza haya yasingekukuta.

Kuna gari wanakuwa nazo kwenye stock na hawajazipost bado unapata kwa bei nzuri sana na zipo katika auction grade nzuri sana ya kuanzia 4.5.

Rafiki yangu juzi tu hapa amechukua Subaru Forester XT imesimama vizuri ukiambiwa ni used unakataa. Ila tulienda hadi ofisi za beforwad na kupata ile one on one consultation na kuuliza maswali yote kujiridhisha.

Unapoagiza gari unatakiwa usikubali kupangiwa ila wewe ndie upange masharti ya namna unataka gari yako iweje na ifike katika hali gani na ikitokea kinyume mkubaliane kabisa nini kitafuata.
 
Gari mpaka kufika 26M, mbali ya ushuru. Ilipofika tu service kwenye yard ya Be Forward ilikwenda zaidi ya 250,000 maana TBS walikataa kurelease gari. Baada ya gari kutoka nimelipeleka gereji nyingi sana na nimetumia zaidi ya 10,000,000 kujaribu kulirepair lakini wapi. Mpaka nilinunua Gear Box mpya lakini wapi.!
Mkuu pole,hiyo pesa uliyonunulia gari ni halali yako 100% ??
Naona kuna kitu hakipo sawa kwenye ulimwengu wa kawaida hata wa kiroho.
Pole sana.
 
Halafu kuna sehemu nakumbuka niliona hapa ndani mtu alipost ukitaka kuona details za gari unayotaka bila kuuliza mtu yoyote. Ni website sijui niliiona wapi ile website.
 
Mbona lakini hata ukiingia pale kwenye website ya beforwad wanakuandikia kabisa "Third-party dealership". Yaani kama gari unayoiona hapo kwenye stock ya mzigo wao kama beforwad bali ni wauzaji wengine ambao wametumia platform ya beforwad.

Na pale utaona location wanakuonyesha kabisa kama ni Singapore au Japan.

Ni vema kujifunza kabla ya kuagiza gari mwenyewe. Ni bora usikie maoni ya wazoefu kabla haujaingia na kuchezea za uso.
 
Back
Top Bottom