'Beach boy' jela maisha kwa kumbaka mtoto akimfundisha kuogelea

'Beach boy' jela maisha kwa kumbaka mtoto akimfundisha kuogelea

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mahakama ya Wilaya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, imemhukumu Dunia Suleman (36) maarufu P squre, kutumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti wa miaka nane.

Suleman, ambaye ni beach boy na mkazi wa Msasani wilaya ya Kinondoni, anadaiwa kumbaka binti huyo wakati akimfundisha kuogelea katika ufukwe wa Coco, uliopo Bahari ya Hindi.

Mshtakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho na Hakimu Mkazi Mkuu, Erick Rwehumbiza, baada ya mshtakiwa huyo kukiri shtaka lake. Pia, mahakama hiyo imetoa amri tube ya tairi ya gari, iliyotumika kutendea kosa hilo, iharibiwe. Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Rwehumbiza alisema mshtakiwa ametiwa hatiani kama alivyoshtakiwa.

“Mahakama imekutia hatiani kama ulivyoshtakiwa baada ya kukiri shtaka la kubaka mtoto, hivyo utatumikia kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa wenzako,” alisema Rwehumbiza.

Awali, wakili wa serikali, Michael Shindai, aliiomba mahakama itoe adhabu kali dhidi ya mshtakiwa kwa kuwa vitendo vya ubakaji watoto vimekuwa vikiongezeka kila siku.

“Mheshiwa hakimu, kwa kuwa mshtakiwa amekiri shtaka lake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu, naomba mahakama yako itoe adhabu kali kukomesha vitendo hivi,” aliongeza Shindai.

Pia upande wa mashtaka uliwasilisha vielelezo vinne ambavyo ni fomu ya PF3, maelezo ya onyo ya shahidi, hati ya gwaride la utambuzi na hati ya kuchukulia mali ambayo ni tube ya tairi la gari lilitumika kutendea kosa.

Kabla ya kupewa adhabu hiyo, Mahakama hiyo ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea kwanini asipewe adhabu kali.nHata hivyo, mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na kwamba alipitiwa na shetani.

“Naomba mama wa mtoto huyu, anisamehe sana, nilipitiwa na shetani, naomba msamaha,” alidai mshtakiwa.

Hakimu Rwehumbiza alitupilia mbali maombi ya mshtakiwa huyo na kumhukumu kifungo cha maisha jela.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, P square anakabiliwa na kesi ya jinai namba 183/2022, mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 13, 2022 katika ufukwe wa Coco, uliopo wilaya ya Kinondoni. Inadaiwa siku hiyo ya tukio, Suleman anadaiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8, kinyume na kifungu 130(1)(2)e na kifungu 131(1) cha kanuni ya adhabu.

Wakili Shindai alidai kuwa mshtakiwa alipewa watoto wawili wa familia kuwafundisha kuogelea, lakini badala ya kuwafundisha alimchukua binti huyo na kumpeleka baharini na kisha kumbaka. Hata hivyo mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka lake, alikiri na ndipo mahakama hiyo ilipomtia hatiani.

Kwa mara ya kwanza, mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama hiyo, Agosti 24 mwaka huu kujibu shtaka hilo.
--
Pia soma > Serikali iingilie kati juu ya Ubakaji unaoendelea Coco Beach jijini Dar!
 
Kwangu mm lawama zote nawapa Hao waliomkabidhi mtoto mdogo tena wakike kwa Huyo punguani ilikua Kuna ulazma gani wajifunze kuogelea mtu humjui mmekutana beach tu Ni ufedhuli wa hali ya juu Hapo wazaz watakua wanajilaumu Sana kwa hilo washenzi kabsa, ningekua ndugu wa hao ningeanza kudeal na aliemkabidhi MTOto...
 
Miaka 36 unafanya kazi ya beach boy! Unapewa kazi ya kiwafundisha watoto wadogo (kwa Jiji la Dar mtoto wa miaka 8, ni hatari kweli kweli) ghafla shetani anakupitia! Unambaka.

Kesi inapelekwa mahakamani, unakubali kosa faster! Unakula zako kifungo cha maisha jela!! Kazi kweli kweli. Yaani hakitaka kabisa kuisumbua mahakama.
 
Miaka 36 unafanya kazi ya beach boy! Unapewa kazi ya kiwafundisha watoto wadogo (kwa Jiji la Dar mtoto wa miaka 8, ni hatari kweli kweli) ghafla shetani anakupitia! Unambaka.

Kesi inapelekwa mahakamani, unakubali kosa faster! Unakula zako kifungo cha maisha jela!! Kazi kweli kweli. Yaani hakitaka kabisa kuisumbua mahakama.
Alijua akikiri mapema atasamehewa.
 
Miaka 8 kweli? Hiyo ni zaidi ya tamaa,kwanini asingesubiria kwanza wale wadada wakubwa,awale kama wanavyowalaga mlemle majini,halafu ndiyo awafundishe hao watoto akiwa hana ashki?
Pole yake,jela hakuzoeleki.
Jamaa ameponzwa na kazi yake ya u beach boy. Ni kama tu kazi ya ualimu ilivyo na majaribu. Ukiruhusu tu shetani akupitie, basi unakutana na mlango wa jela mbele yako.
 
Kmmk ilifaa kwanza na yeye wamsafishe njia la mlango wa uwani.

Inaumiza sana mtoto mdogo kufanyiwa hivyo
atakutana na wababe wenzie huko huko ndani ataolewa tu.

Ila huyo mama wa mtoto ama yeyote aliyekwenda na mtoto huko beach anapaswa apewe japo miezi 6 ndani.

Mtu na akili zako timamu unaruhusu vipi beach boy 'amfundishe' mwanao kuogelea mbali ya upeo wa macho yako.

Kila siku swala la wafundisha kuogelea wa Coco linaongelewa kuwa sio watu wa kuaminika lakini bado mtu unaenda kuruhusu mtoto mdogo ashikwe nae.

Watu wazima tu wanabakwa na hao watu itakuja kuwa binti wa miaka 8?
 
Aisee hwa vijana ni wahuni mno unaenda beach wanakufata wanakutupia mpira ule wakijidai wanakufundisha kuogelea ukikubali tu imekula kwako wanakupeleka kwenye kina kirefu ambacho ukicheza unakufa aisee lzm utatoa mzigo tu ukibisha bisha anakuachia unywe maji ya kutosha ni wengi sana wamama watot na wadada. WanaLiwa kimasiara sna kwenye maeneo ya beach za Coco na mbezi beach

Hawa vijana wapigwe marufuku maana wageni WanaLiwa kila kukucha na hao waogeleaji

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom