'Beach boy' jela maisha kwa kumbaka mtoto akimfundisha kuogelea

'Beach boy' jela maisha kwa kumbaka mtoto akimfundisha kuogelea

Wazazi nao walaumiwe hapo na iwe funzo kwa wazazi wengine.
Kama ni kumfundisha mtoto basi uajiri personal trainer na sio tu just anybody.
Hao hao personal trainer ndio wanakula na kumshikashuka mtot viungo hatarishi ukizani anafundishwa kumbe mtoto Alisha tekenywa mnoo anatoka ktk maji kachoka kumbe wamesha mtekenya vibaya mno

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Wazaz tuwachunge sana mabinti zetu hasa Hawa wadogo, usimwani hata mjomba,sijui binamu nk dunia ishaharibika hii.
Sio mabinti Tu mkuu...hata watoto wetu wakiume usiruhusu sijui kulala na ndugu au wajomba,au wageni wamekuja kwako kukutembelea wakalala na kijana wako.

Hawa ndio huwaingiza katika ushoga mapema....kuna ushahidi juu ya mambo hayo
 
Unadhani ukiwaita kwa kizungu "personal trainer" ndio inapunguza hatari kwa mwanao? Tena huyo atafanyia hapohapo nyumbani kwako usipokiwa makini
Sio kizungu, risk zipo kila sehemu
Ila atleast ukiajiri mtu maalum au kumpeleka shule zenye hizo mambo inapunguza risk.
 
Personal trainer bado kuna shida bado watu hawaaminiki, cha muhimu mzazi wa kiume mfundishe wa kiume, mzazi wa kike ruka na wako wa kike kazi kwisha😁😁
Sio wazazi wote wanajua kuogelea
 
Nimewaza aliamua nini kukiri? Au alitaka kwenda jela?

Maana kwa kesi hiyo uthibitisho ungekuwa mdogo, kesi ingeenda muda mrefu
Inaonekana kweli katenda na wamemshauri kubali yaishe na yameisha kweli, mtoto miaka nane aysee hii dunia kweli tupo mwishoni,,,
china wana mkata kichwa ili iwe fundisho kwa wajinga wengine.
 
Sio kizungu, risk zipo kila sehemu
Ila atleast ukiajiri mtu maalum au kumpeleka shule zenye hizo mambo inapunguza risk.
Imani yako kubwa kwa shule zenye facilities za kisasa ndio itakuwa anguko lako. Somo usiamini yeyote.

Chunga mwanao kama unavochunga moyo wako, Patrice Evra alikuwa abused katika shule hizohizo na mtu aliyeaminiwa na familia
 
Miaka 8 kweli? Hiyo ni zaidi ya tamaa,kwanini asingesubiria kwanza wale wadada wakubwa...
Mara ya Kwanza kuona mwanamke akibakwa ni kawe beach enzi hizo za ujana,nilikuwa mtu wa beach sana maana nimetoka mkoani kuna bahari so nilikuwa napenda kuogelea tangu nikiwa mkoa..

Jamaa wawili wamempandisha mdada mmoja mkali Sana mweupee anaonekana km wa Arusha maana hajui kuogelea na Kiswahili cha chuga.Wahuni walianza nae mdogo mdogo wakimpetipeti Kama malkia yeye amejilaza Tu kwenye Ile tube, taratibu wanasogea nae maji makubwa.

Kuja kustuka wanebaki watatu tu tena wamejitenga mbali na watu..baada ya dakika Kama kumi binti anatapatapa pale kwenye tube Kwa mbaliii kumbe wahuni wanaichakata mbususu Kwa chini..Dakika mbili bibie anakuja nchi kavu huku macho yamemtoka km ngumi alafu mekundu balaa, wenzie aliokuja nao wanamuuliza vipi mbn upo hivyo,akawajibu tuondokeni huku machozi yanamlenga..Jamaa mmoja pembeni yangu akasema huyu tyr w*sh*mt©mb@ kule kwenye maji mengi ndiyo maana amepagawa hivi halafu hasemi tatizo

Mwingine nilishuhidia wakimbaka longoni beach,Kwa wanajeshi pale kigamboni,binti walimvuta Hadi kwenye ksiwa cha jiwe Fulani kubwa(wanaopajua longoni beach wanaelewa) wakamwambia hapa hatukurudishi na tairi tunalitoa hewa ukitaka Toa mzigo tuchakate.

Hizi beach ni hatari siyo Kwa watoto pekee Bali pia hata Kwa wadada/mabinti,wengi sn wanabakwa na hawasemi wansona aibu
 
Mara ya Kwanza kuona mwanamke akibakwa ni kawe beach enzi hizo kabla za ujana,nilikuwa mtu wa beach sana maana nimetoka mkoani kuna bahari so nilikuwa napenda kuogelea tangu nikiwa mkoa...
Kuna uzi humu mrefu unajadili matukio haya cocobeach. Afadhali mmoja kafungwa, haitamaliza tatizo ila itatuma ujumbe kwa mabazazi waliosalia. Kikubwa watu wakienda beach waende kuinjoi maji na ufukwe waachane na masuala ya kujichanganya na strangers kwa sababu yoyote ile ikiwamo kufundishwa kuogelea
 
Kwangu mm lawama zote nawapa Hao waliomkabidhi mtoto mdogo tena wakike kwa Huyo punguani ilikua Kuna ulazma gani wajifunze kuogelea mtu humjui mmekutana beach tu Ni ufedhuli wa hali ya juu Hapo wazaz watakua wanajilaumu Sana kwa hilo washenzi kabsa, ningekua ndugu wa hao ningeanza kudeal na aliemkabidhi MTOto...
Kama alitorokea huko ukukweni mwenyewe au alienda na wenzie
 
Mara ya Kwanza kuona mwanamke akibakwa ni kawe beach enzi hizo kabla za ujana,nilikuwa mtu wa beach sn maana nimetoka mkoani kuna bahari so nilikuwa napenda kuogelea tangu nikiwa mkoa....
Kuna Haja ya Serikali katika maeneo husika ,kuwa na Muongozo ,utakao elezea utaratibu wa Namna ya Kuwalinda Watoto wa kike katika Maeneo ya fukwe,

Kwa maelezo yako ,Nashawishika kuamini ya kwamba ,Watoto wa kike wanafanyiwa vitendo vya kikatili ,hasa katika maeneo ya Fukwe za Bahari Dar El salaam,

Hatua stahiki zinapaswa kuchukuliwa ,ili kuzuiia Vitendo hivi vya kikatili.
 
Dunia hii Jamani kila tunapo amka tukumbuke kusali ili mungu atuepushe na mambo mabaya yanayoweza kututokea kwenye harakati za kila siku.

Mfano huyo jamaa juzi tu August 13 alikuwa mtaani anakula raha, Ila leo ananyea ndoo for the rest of his life
 
Mara ya Kwanza kuona mwanamke akibakwa ni kawe beach enzi hizo kabla za ujana,nilikuwa mtu wa beach sn maana nimetoka mkoani kuna bahari so nilikuwa napenda kuogelea tangu nikiwa mkoa...
Beach za tanga walikataza kufundisha kuogelea kutokana na haya matukio

Ukikuta unafundisha mtu imekula kwako
 
Hao mabeach boy wanajua wanachofanya na malengo yao.kwanza uwa hawafundishi kuogelea.uwa na mapira yao na lengo ni kuwagonga mademu.watoto wa shule za secondary wamegongwa san a na hawasemi tu.
Jamaa ameponzwa na kazi yake ya u beach boy. Ni kama tu kazi ya ualimu ilivyo na majaribu. Ukiruhusu tu shetani akupitie, basi unakutana na mlango wa jela mbele yako.
 
Mahakama ya Wilaya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, imemhukumu Dunia Suleman (36) maarufu P squre, kutumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti wa miaka nane.

Suleman, ambaye ni beach boy na mkazi wa Msasani wilaya ya Kinondoni, anadaiwa kumbaka binti huyo wakati akimfundisha kuogelea katika ufukwe wa Coco, uliopo Bahari ya Hindi.

Mshtakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho na Hakimu Mkazi Mkuu, Erick Rwehumbiza, baada ya mshtakiwa huyo kukiri shtaka lake. Pia, mahakama hiyo imetoa amri tube ya tairi ya gari, iliyotumika kutendea kosa hilo, iharibiwe. Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Rwehumbiza alisema mshtakiwa ametiwa hatiani kama alivyoshtakiwa.

“Mahakama imekutia hatiani kama ulivyoshtakiwa baada ya kukiri shtaka la kubaka mtoto, hivyo utatumikia kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa wenzako,” alisema Rwehumbiza.

Awali, wakili wa serikali, Michael Shindai, aliiomba mahakama itoe adhabu kali dhidi ya mshtakiwa kwa kuwa vitendo vya ubakaji watoto vimekuwa vikiongezeka kila siku.

“Mheshiwa hakimu, kwa kuwa mshtakiwa amekiri shtaka lake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu, naomba mahakama yako itoe adhabu kali kukomesha vitendo hivi,” aliongeza Shindai.

Pia upande wa mashtaka uliwasilisha vielelezo vinne ambavyo ni fomu ya PF3, maelezo ya onyo ya shahidi, hati ya gwaride la utambuzi na hati ya kuchukulia mali ambayo ni tube ya tairi la gari lilitumika kutendea kosa.

Kabla ya kupewa adhabu hiyo, Mahakama hiyo ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea kwanini asipewe adhabu kali.nHata hivyo, mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na kwamba alipitiwa na shetani.

“Naomba mama wa mtoto huyu, anisamehe sana, nilipitiwa na shetani, naomba msamaha,” alidai mshtakiwa.

Hakimu Rwehumbiza alitupilia mbali maombi ya mshtakiwa huyo na kumhukumu kifungo cha maisha jela.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, P square anakabiliwa na kesi ya jinai namba 183/2022, mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 13, 2022 katika ufukwe wa Coco, uliopo wilaya ya Kinondoni. Inadaiwa siku hiyo ya tukio, Suleman anadaiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8, kinyume na kifungu 130(1)(2)e na kifungu 131(1) cha kanuni ya adhabu.

Wakili Shindai alidai kuwa mshtakiwa alipewa watoto wawili wa familia kuwafundisha kuogelea, lakini badala ya kuwafundisha alimchukua binti huyo na kumpeleka baharini na kisha kumbaka. Hata hivyo mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka lake, alikiri na ndipo mahakama hiyo ilipomtia hatiani.

Kwa mara ya kwanza, mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama hiyo, Agosti 24 mwaka huu kujibu shtaka hilo.
Huyu beach boy muuaji mkubwa hajui athari aliyoicha kwa binti huyu na walimkabidhi mtoto kwa mtu huyu nao wanapaswa kujitafakari
 
Back
Top Bottom