Beatrice Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake kwamba ana fedha nyingi lakini hamsaidii mama yake

Comment yako imenigusa sana. Pia mimi nina mdogo wangu ambaye hata ukitaka umsaidie inakuwa ngumu sana kwasababu yeye mwenyewe haelewi anataka nini.
Inaumiza alafu sasa watu baki wanakuwa ma-baba / mama washauri kwamba "msaidieni ndugu yenu"....na kwenye maisha unakutana na watu baki wengi wazuri unakuta mnapeana support, sasa ndo hapo ndio inapoonekana una support watu baki na si ndugu
 
Aaache upumbavu kulia lia kwa watu ni upumbavu huyo Martha yumo humo? Si amfuate alipo? Aache kulia lia. Ni upumbavu.
 
Hakuna pesa za shetani ndugu Kugawa gawa pesa ni chanzo cha umasikini tafuta pesa kwa jasho lako tamu kuzitumia usililie pesa za mtu mwingine
Yeah sure mkuu.

Hakuna pesa za kishetani.

Ni waafrika wavivu na maskini wasiotaka kuhustle wenyewe wana tegemea pesa za watu.

Na wasipo pewa wanaanza kusema ni pesa za kishetani.
 
Tatizo la huyo ndugu yako wa kuzaliwa limetengenezwa na mzazi ..kama uamini niambie nije nikuulize maswali kisha nitakuambia tatizo lilianzia wapi na kwa nani na kwa sababu gani ...hata hiyo misahada mnayo mpa mnampa kwa wakati sahihi au ni sawa sawa na mzazi kumpa mtoto wake mil10 wakati tayari huyo mtoto amesha vulugikiwa au kesha kuwa teja au kesha kata tamaa ya maisha nk
 

Sikiliza vizuri ile video ndio utoe maoni inaonesha hajasikiliza
Beatrice hajaongelea kuhusu kusaidiwa yeye Bali anamkumbusha dada Ake kuhusu mama yao,lkn pia kaongea kuwa huyo mtoto Joan sio mtoto wake Wala sio ndugu yao,sasa mzee wewe umesikiliza clip ipi?mpaka utoe ushauri huo?
 
Wazazi wetu wa kiafrika wanashida Sana hasa kina mama,mchezaji mpira wa Togo Emanuel Adebayo alimfanyia vitu vyingi mama yake lakini bado hakuridhika akawa anaungana na wadogo zake Adebayo kumpiga hela tu mpaka jamaa akataka kujiua kwa msongo wa mawazo
 
Inaumiza alafu sasa watu baki wanakuwa ma-baba / mama washauri kwamba "msaidieni ndugu yenu"....na kwenye maisha unakutana na watu baki wengi wazuri unakuta mnapeana support, sasa ndo hapo ndio inapoonekana una support watu baki na si ndugu
Kwenye familia tutasaidiana na anayetaka kusaidiwa. Kama mtu hataki maendeleo tutabaki tu kuwa ndugu na kubaki kusaidiana vile vitu basic kama ndugu. Kwa mfano ndugu yako kakamatwa hutavumilia lazima utaenda kituoni kumtoa kwanza.
 
We nae tumia akili
Unavyomuona huyo beatrice ana akili??? Kwa alozungumza tu
Mi naona yuko sahihi, makanisani leo hasa ya kilokole waumini wanawafanya wachungaji, mitume manabii kama ndio wazazi wao na kuwasahau wazazi wao wa asili, wewe kama husali huko huwezi kuelewa na baadhi yao hubadili mpaka majina ya pili wanaweka ya baba zao wa kiroho na hii kimaandiko siyo sahihi.
 
Ameongea kwa wivu sana wamechangia baba tu iweje martha atunze mama wa kambo ni lazima?
 

Joan anawazazi wake inakuaje anabadili jina la Baba yake nakutumia jina la Mwaipaja mzazi wa Martha!
 
Mji mzito..kusagana, uchungaji, uimbaji nyimbo injili sjui, yote yanafanyika
 
How are you Kaveli ?
Merry Christmas in advance😊
YNWA

I am doing fine my dearest sis friend. How about you?

Thanks a bunch mtakatifu Anne. Hunaga baya mama. 😊

Mwaka ushaelekea kibra. Nakutakia tamati njema ya mwaka huu.

-Kaveli-
 
I am doing fine my dearest sis friend. How about you?

Thanks a bunch mtakatifu Anne. Hunaga baya mama. 😊

Mwaka ushaelekea kibra. Nakutakia tamati njema ya mwaka huu.

-Kaveli-
Amen
Mungu akuvushe wewe, pamoja na wapendwa wako .
 
"Dada yangu anatembelea gari la million mia..."

Zengwe lilianzia hapo. 😎

-Kaveli-

Kauli hiyo ina reflect husuda kali alonayo Mdogo mtu kwa dada yake .

WAT-u mnaweza kuzaliwa tumbo moja lakini msipendane kwa dhati ya moyo , ikawepo husuda wivu hata kurogana na kuharibiana
Na kukwamishana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…