Behewa za SGR zaanza kuwasili nchini Tanzania

Mwanzo tuliahidiwa hivi[emoji1313][emoji1313][emoji1313]Picha namba 1
Tumeletewa haya mabox Picha namba 2
Ni huzuni[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

View attachment 2424970View attachment 2424971
Hapa ninachokisoma na kinachokanushwa ni vitu viwili tofauti, kwanza Watanzania tunapaswa kuambiwa ukweli
1. Taarifa ya TRC inasema vichwa vipya na mabehewa mapya, lakini ukweli ni kuwa ni vichwa mitumba na mabehewa mitumba ya mwaka '1947'!.
2. Mkataba ni wa ukarabati na kutiwa nakshi nakshi kwa vichwa na mabehewa mitumba!, na sio kuundwa kwa vichwa na mabehewa mapya!.
3. Hakuna ubaya nchi kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, kitu muhimu ni Watanzania tuelezwe ukweli!.
4. Jee hivyo vichwa viliundwa lini, wapi na vimetumika muda gani kabla sisi hatujauziwa?.
5. Mitumba hiyo imenunuliwa kwa bei gani na inakarabatiwa kwa bei gharama gani?.
5. Tufanyiwe comparative analysis, kama tungenunua vichwa vipya na mabehewa mapya, tungetumia gharama kiasi gani, compared na kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, ili tujue tumeokoa fedha kiasi gani kwa kununua mitumba hiyo?.
6. Japo gharama za kununua vitu vipya ni juu ila maintance cost ni ndogo, unaweza kununua mitumba kwa bei poa kumbe ni mitumba choka mbaya, hivyo maintenance cost ikawa juu.
7. Sii wengi wanajua kazi ya CAG sio kutoa tuu zile ripoti za hesabu za serikali, CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, ufhibiti unafanywa kabla ya manunuzi, jee kulifanyika tathmini yoyote rail worthness report ya vichwa mabehewa hayo mitumba kabla hayajanunuliwa?. Then CAG atufanyie value for money audit, msikute mitumba hiyo tumepewa bure, huku watu wakipiga kubwa tunauziwa kwa bei ya mapya!.
8. Ukiingia mkataba wa manunuzi, mzigo ukanunuliwa, delivery ndio ikachelewa, huwezi kuvunja mkataba huo ukabaki salama, hivyo kesi ikifunguliwa, Tanzania tunashindwa hata kabla kesi haijaanza!.
9. Tulivinja mkataba wa Dowans, watu wakajiapisha "over my dead body", tulishitakiwa, tukashindwa, tukadaiwa tukasema hatulipi!, ukweli ni kuwa tumelipa kwa siri, Watanzania hatukuambiwa!.
10. Tulipo vunja mkataba wa Dowans, Zitto akashauri tuitaifishe mitambo ile, Wabunge wetu wakagoma kuwa Tanzania hatununui mitambo mitumba!.
11. Mitambo ile ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule wa Dowans tuliovunja, kwa gharama zile zile na tukawalipa!.
12. JPM alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, JPM akagoma kulipa!, ila baada tuu ya JPM kuitwa kule, huku nyuma, sio tuu tumelipa, bali pia tumeinunua ile mitambo kwa bei ya ajabu!, sasa mitambo ile tuliosema ni mtumba hatununui, sasa ni mali yetu na malipo yote yaliisha fanyika chap chap!, ila Watanzania hatuambiwi!.

Tuambiwe tuu ukweli!.
P
 
Mkuu pascal Nyie ndio wazee wazalendo bhana mnajigamba kuwa sisi vijana wa siku hizi hatujielewi ni wajinga wajinga.

Ila tunawashangaa nyie wazee wetu mliosomeshwa bure bila kutakiwa kurejesha hata senti mnavyo ongoza hii nchi na namna mlivyo waongo, walafi msivyoridhika..

Hii nchi mnaitia laana na mikosi mnaturithisha uongo uwe sehemu ya maisha. Mwishowe tunaonekana ni nchi ya wapumbavu na wajinga.

Wazee wetu nyie mnalinajisi hili taifa kwa mambo ya aibu mnayolifanyia hili taifa.
 
Mwanzo tuliahidiwa hivi[emoji1313][emoji1313][emoji1313]Picha namba 1
Tumeletewa haya mabox Picha namba 2
Ni huzuni[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

View attachment 2424970View attachment 2424971
Na bado picha kamili ni pale litapoanza kufanyakazi hilo treni muda tulioaidiwa sijui dar to moro ni 1 hour itakuwa 4 hours..ni hapa nimeweka kambi subilini muone..

Hii nchi inaviongozi waongo alafu ni wale wasioogopa kusema uongo kila sehemu ni uongo uongo tanesco uongouongo na janjajanja, maji huko ni yaleyale, elimu hivyohivyo .
 

Duh, inzi wanatafuta hela za uchaguzi
 
Mabaki ya vita ya pili ya dunia🤣,
Hii nchi hii tuna laana.
 
Behewa 14 za SGR zimeanza kuwasili nchini Tanzania kutoka nchini Korea View attachment 2424514
Magonjwa ya Africa ni mengi kiasi kwamba huwezi yaponya kwa mpigo,umasikini wa Kutoka uchumi wa kati na kurudishea chini ni swala kubwa,imagine hata margarine inatoka nje ya nchi, blueband,vitasa na plywood hii ni nchi imeamka jana tutulie mpqka sindano itulie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…