Behind the curtain: September 11

Behind the curtain: September 11

BEHIND THE CURTAIN: SEPTEMBER 11



SEHEMU YA 11





Katika sehemu ya 10, nilimalizia makala ile kwa swali hili?





Sasa, kwanini mtu ambaye japokuwa CIA wanaficha na kumficha lakini imethibitika pasina shaka yoyote kuwa ni "asset" ya CIA awe na mafungamano kiasi hiki na Bin Laden?? Je Bin Laden alikuwa ni mahirika pia wa CIA/Marekani??


Wacha nieleze tena japo kwa uchache ambapo kwa makusudi kabisa kuna dalili zinaonyesha kuwa watu wa ngazi za juu kabisa labda waliacha kwa makusudi kabisa Osama ajiimarishe na mtandao wake wa Al-Qaida kushamiri.



MAY, 1998

CIA kwa miezi kadhaa walikuwa wamekusanya Intelijensia ya kutosha kuhusu eneo fulani nje kidogo ya mji wa Kandahar nchini Afghanistan.

Katika eneo hili kulikuwa na nyumba za matofali ya matope zipatazo themanini ambazo ziko ndani ya ukuta wenye urefu wa futi kumi.

Kwa kutumia Intelijensia kutoka kwa asset baadhi ya raia wa Afghanistan walikuwa wanaishi karibu na eneo hilo, CIA walifanikiwa kuitambua nyumba mojawapo kati ya hizo themanini kuwa ilikuwa ni nyumba ya moja ya wake wa Osama bin Laden, na Osama huwa anaenda kulala hapo mara kadhaa.

CIA wakafanikiwa 'kumap' eneo lote hilo na kutengeneza 'compound' kama hiyo nchini Marekani kwa ajili ya mazoezi.

Mwaka 1997 wanafanya mazoezi ya kina Kwa mara mbili.

Mwaka 1998 wanafanya tena mazoezi kuhusu oparesheni waliyokuwa wanataika kuifanya.

Mwaka huo huo 1998 wakaijulisha Ikulu ya Marekani kuhusu mpango huo waliokuwa nao. Rais Bill Clinton akakataa CIA kuhusika moja kwa moja kutekeleza oparesheni hiyo ili isije kuleta mdororo wa kidiplomasia ikitokea Afghanistan na nchi za kiarabu wakigundua.

Hivyo CIA ikabidi wabadili mkakati wao, safari hii wakaja na mpango wa kutumia vikundi viwili vya kikabila ndani ya Afghanistan kufanikisha oparesheni hiyo.
Mpango wao ilikuwa kwamba, siku ambayo Osama ataenda kulala hapo kwa mkewe basi kikundi kimoja kitamkamata kisha watampeleka mpaka jangwani na kumkabidhi kwa kikundi cha pili ambacho watakaa naye kwa mwezi mzima (ili kuondoa hisia za uhusika wa Marekani) kisha watamkabidhi kwa CIA ambao watamsafirisha mpaka kwenye jela zao za siri Ulaya au nchi rafiki ya Kiarabu.

Mwezi March 1998, wanafanya mazoezi ya tatu kuhusu hiyo Oparesheni wakihusisha pia wawakilishi wa vikundi hivyo vya kikabila kutoka Afghanistan.

Tarehe 20 mpaka 24 May yakafanyika mazoezi ya mwisho yaliyohusisha Maafisa wa CIA, FBI na wawakilishi kutoka Afghanistan.

Tarehe 27 May, Mkurugenzi wa CIA aliandika MNO (Memorandum Of Notification) kwenda Ikulu kwa Rais Bill Clinton kuomba 'Approval' ya oparesheni hiyo ambayo walipanga ifanyike June 23 na Osama asafirishwe kutoka Afghanistan mwezi mmoja baadae yaanj July 23.
Pia MON iliomba wawakilishi wa CIA wafanye kikao Tarehe 29 na washauri wa Rais kuhusu masuala ya Usalama.

Jambo la kushangaza ni kwamba, kikao hicho hakikufanyika (washauri wa Rais hawakutokea kwenye kikao), ile MON haikujibiwa na hawakupewa 'Approval' ya Oparesheni hiyo.

Bw. Tenet ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa CIA kipindi hicho, anaeleza kuwa yalikuwa ni moja ya maamuzi ya kushangaza zaidi ya Rais Bill Clinton ambayo mpaka leo hii hajui alitumia utashi gani kuyafanya.



December 1998

Kwa mara nyingine tena CIA walikusanya Intelijensia na kubaini kuwa Osama atakuwepo kwenye jumba linaloitwa Haji Habash ambayo ni sehemu ya makazi ya gavana wa Kandahar.

CIA wakapendekeza lifanyike shambulio la Anga (air strike), lakini Rais Clinton akakataa kutoa ruhusa na baada ya kumng'ang'aniza sana akatoa ruhusu labda wamkamate akiwa hai (Capture Operation) lakini sio air strike.

Sababu yake kuu, ati alikuwa anahofia maisha ya watu wasio na hatia kwenye jumba hilo.


February - March 1999

CIA walipata taarifa za Intelijensia kuwa Osama alikuwa anatembelea mara kwa mara kwenye kambi za uwindaji maeneo ya jangwani mwa Kandahar ambako kulikuwa na wageni kutoka Emirates.

CIA wakajitahidi kupata Intelijensia kujua Osama huwa anakaa kwenye mahema gani akitembelea kambini hapo.

Baada ya kuwa na taarifa za kutosha kwa mara nyingine wakapendekeza kufanyika air strike siku Osama akiwa kambini hapo, lakini kwa masikitiko makubwa Bill Clinton akakataa akidai kuwa kuna taarifa kuwa moja ya wageni hao kutoka UAE ni Prince wa Emirate hivyo anahofia kuharibu mahusiano ya kidiplomasia.




November - December, 2000.

Al-Qiada walikuwa wamefanikiwa kufanya shambulizi kwenye kituo cha kijeshi cha Marekani nchini Yemen na kuna wanajeshi kadhaa.

Kwahiyo Osama alikuwa anahisi Marekani lazima watafanya oparesheni ya kisasi (Retaliation).
Kwahiyo ili kuchukua tahadhali kwa kufunga kwa muda kambi zake za mafunzo huko Kandahar na pia akawagawanya viongozi wakuh kwenye maeneo tofauti tofauti ili wasiwe sehemu moja ikitokea wameshambuliwa.

Kamanda wake mkuu wa jeshi, Mohammed Atef akajificha pembezoni mwa mji wa Kandahar, msaidizi wake mkuu Ayman al-Zawahiri akaenda Kabul na yeye mwenyewe akawa anabadilisha makazi kila kukicha.
Kwanza akaenda Kabul, kisha akaelekea Khowst, baadae akaenda Jalalabad na kisha akarejea tena Kandahar.

Akiwa Kandahar kulikuwa na nyumba sita ambazo alikuwa anabadilisha ratiba ya kulala kila siku.

CIA walikuwa wanafuatilia nyendo zake zote hizi, na baada ya kuwa na Intelijensia ya kutosha kuhusu 'rotation' ya movement zake wakapendekeza kwa Rais Clinton ifanyike Air Strike katika nyuma anazoishi mjini Kandahar.

Kwa mara nyingine tena, Rais Clinton akakataa kutoa approval ya air strike akidai kuwa labda wafanye 'capture oparation'

Kutokana na risk kubwa ya capture Opararion, ikawabidi kwa mara nyingine tana CIA kuhahirisha Oparesheni.


Sasa,

CIA walikuwa wanang'ang'ana kum-neutralize Osama mapema kwa kuwa walikuwa wanaamini kuwa yuko kwenye mipango ya kutekeleza tukio kubwa sana.

Ni ajabu sana jinsi ambavyo Rais Clinton na viongozi wa juu walivyokuwa wanakwamisha juhudi za kum-neutralize Bin Laden.! Labda kuna jambo walikuwa wanalijua ambalo majasusi wengine hawakulijua..

Labda, Osama alikuwa anaachwa kwa makusudi ajinenge na mtandao wake ushamiri kwa makusudi.!!



"…lawama za tukio la 9/11 zinapaswa kuelekezwa kwa watu ambao waliicha Al-Qiada ikue na kushamiri na maamuzi ta kumpoteza kiongozi wao hayakufanywa pale ambapo fursa ilijitokeza.. Sio mara moja, bali mara nne nzima.. Rais Clinton hawezi kuepuka lawama hii.."

-Senata Marco Rubio, Mogombea tiketi ya Urais katika chama cha Republican. (Alisema haya kwenye mdahalo wa February 13, 2016).





Nimeeleza kwa kina namna gani kunaonyesha kwamba kulikuwa na dalili ya kumuacha Osama bin Laden na mtandao wake wa Al-Qaida wakue na kushamiri.. Sasa twende mbele kidogo uone upotoshaji na uongo uliokuja kufanyika wenye kutia mashaka makuba..






‘UONGO 'ULIOTUKUKA'


Mara baada ya kutokea shambulio la 9/11 viongozi wa juu qa serikali karibia wote walijitokeza hadharani na kutoa kauli mbali mbali.

Moja wapo ya kauli hizi zilitolewa na wafuatao;

Rais George W. Bush,

"..nobody in our government at least, and I don't think in the prior government, could envisaged flying airplane into buildings.."

("..hakuna mtu katika serikali serikali yetu, na nadhani hata serikali iliyopita (Bill Clinton), ambaye angeweza kudhania kungekuwa na shambulio ambalo litatumia ndege kulipua majengo..")

Kauli hii ya Rais George Bush ikafuatiwa na kauli ya Mwanamama Condoleezza Rice kipindi hicho akiwa mshauri wake Mkuu wa masuala ya Usalama (National Security Advisor).

"..no one could have predicted that they would try to use an airplane as a missile.."

(".. Hakuna ambaye angeweza kubashiri kwamba watajaribu kutumia ndege kama silaha..")


Kauli hii ikaja kuungwa mkono pia na Jenerali wa Jeshi la Anga (Air Force).

"..something we had never seen before, something we had never even thought of.."

("..(hiki) ni kitu ambacho hatujawahi kukiona, kitu ambacho hatujawahi hata kufikiri..")



Mkurugenzi Mkuu wa FIB naye wa kipindi hicho, Bw. Robert Mueller akajazia uzito kauli hizi,

"…there were no warnings signs that I'm aware of, that would indicate this type of operation in the country.."

("..hakukuwa na tahadhari au onyo ambalo nimewahi kulisikia ambalo liliashiria kutakiwa na shambulio la dizaini hii ndani ya nchi..")



Ukizichunguza kwa makini kauli zote hizi za hawa mabwana wakubwa wanalenga kuwaaminisha Wamarekanimambo mawili;

Moja: kwamba serikali na vyombo vya Usalama havikuwa na intelijensia yoyote kuhusu mipango ya shambulio hili.

Pili: hata kama intelijesia yao ingeshuku au kuhisi mipango ya tukio hili, kamwe wasingeliweza kudhania kwamba ndege ndio zingetumika kama silaha, kwasababu ni jambo ambalo hawakuwahi kudhania na halijawahi kutokea. Hivyo kamwe wasingeweza kuhisi shambulizi la kutumia ndege.

Kauli hizi zina uwongo wa nje nje ambao ndio unafanya wengi katika Jamii ya Intelijensia waamini kuwa kuna mambo yanafichwa kwa makusudi.
Kwanza si kweli kama Rais Bush na wenzake wanavyodai kuwa hili ni suala jipya hivyo wasingeweza kuhisi kutumika ndege kama silaha, na pia si kweli kwamba serikali haikupewa tahadhari..

Nitaeleza….



Mwaka 1994; kuna ndege binafsi ambayo ilikuwa imembeba mtu mmoja tu ambaye yeye mwenyewe akiwa kama rubani kwa makusudi kabisa aliidondosha ndege katika Ikulu ya Marekani, Washington kwa lengo la Kufanya shambulio. Kwa bahati nzuri ndege ikadondoka kwenye viambaza vya Jengo la Ikulu (lawn).

Kwahiyo hii kauli ya Bush kwamba "…nobody…. could envisaged flying airplane into building.." ni kauli ya uongo wa makusudi kabisa.

Si hivyo tu,

Mwaka 1995; nchini Ufilipino lilitokea mpango wa shambulio lililofeli, ambalo linajulikana kwa jina maarufu la Bojinka Plot. Shambulio hili ambalo lilipangwa na Khalid Sheikh Mohammed lililenga kuteka ndege za Marekani na kwenda kuzibamiza kwenye majengo. Bahati nzuri CIA kwa kushirikiana na Idara Ya Intelijensia wakaepusha shambulio hili kabla halijatokea.
Ndipo hapo ambapo miaka ya baadae KSM akapeleka wazo hili kwa Osama.

(Nilieleza kisa hiki kwenye sehemu za mwanzo za makala hii)

Kwahiyo kauli ya Jenerali wa Air Force kwamba "…something we have never seen before…" ni kauli ya uongo wa makusudi kabisa

Pia,

Mwaka 200, Federal Aviation Administration (FAA) katika ripoti yao ya Usalama wa Anga, kuna vipengele kadhaa wanaonyesha wasi wasi wao kuhusu kutokea kwa ugaidi na kuna paragraph wanamtaja kabisa Osama bin Laden.

Nanukuu kipande kifupi,

"..considering Bin Laden anti-Western and anti-American attitudes, makes him and his followers a significant threat to civil aviation particularly to United States Civil Aviation.."

("..kwa kuzingatia mitazamo hasi ya Bin Laden juu ya nchi za magharibi na Marekani, kunamfanya yeye na wafuasi wake kuwa tishio kubwa kwa usafiri wa Anga na mahususi usafiri wa Anga wa Kibiashara/kirai nchini Marekani..").

Hii ni ripoti ya kiusalama ya Idara kubwa ya nchi ya Marekani inayosimamia usafiri wa Anga. Wanaonyesha wasi wasi wao juu ya Usalama wa usafiri huo na wakimtaja kabisa Osama bin Laden kwa majina yake.

Inashangaza sana kwanini Bush, Condoleezza, Jenerali na Mkurugenzi wa FBI waseme kwamba, kutumika kwa ndege kama silaha ni kitu ambacho wasingeweza kukidhania au kukihisi.

Si hivyo tu,

Mwanzoni mwa Mwaka 2001 (February): NORAD (North American Aerospace Command) walipata 'alert' kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi kwa kutumia ndege.

Mwanzoni walidhania kwamba ndege hizo zinaweza kuingia Marekani kutokea Ulaya, kwahiyo wakaanza mazoezi katika bahari ya Atlantic ili kuona namna bora ya kudhibiti ndege hizo ikitokea hilo suala likatokea kweli inabidi wadhibiti ndege kabla haijaingia Marekani.

Kwahiyo mazoezi yao kwenye bahari ya Atlantic yalienda mbali mpaka kufikia hatua wakawa wanarusha ndege chakavu na kuzidungua.

Baadae wakahamia kwenye mazoezi ya "simulation".
Moja ya sehemu waliyofanya mazoezi hayo ilikuwa ni World Trade Center kwa maana walihisi kuna uwezekano wa majengo hayo kulengwa.
Baadae wakaomba kibali wafanye mazoezi hayo ya " simulation" kwenye majengo ya Pentago. Lakini ajabu ni kwamba kamati ya Majedari wa vikosi vya ulinzi (Joint Chiefs of Staff) wakatoa amri ya kusitishwa kwa mazoezi hayo wakiwapa sababu moja tu kwamba, suala hilo wanalolihisi (Shambulio la ndege) ni "too unrealistic "



Nitoe mfano mwingine ili khonyesha uongo wa kauli hii ya Rais Bush na wenzake kwamba, Shambulio la ndege ni kitu ambacho wasingeweza kudhania.

July, 2001, khlikuwa kunafanyika kongamano la G8 (G8 Summit).
Katika hali inayodhihirisha kwamb a walikuwa na taarifa kuhusu tahadhari ya Shambulio la ndege, kwenye majengo ambayo mkutank ulifanyika kulifungwa "Anti-Aircraft missile battery" ili kujihami na Shambulio la ndege walilokuwa wanalihisi kuwa linalenga kumuua Rais Bush na viongozi wengine.


Si hivyo tu,

THE PHOENIX MEMO

July 10, 2001, Afisa wa FBI, Special Agent Kenneth Williams ambaye alikuwa ofisi ya Arizona alikuwa na assignment ya kuwafanyia uchunguzi wanafunzi kadhaa katika vyuo vya urubani kutokana na wanafunzi hao kutiliwa shaka nyendo zao.

Baada ya kuwachunguza kwa miezi kadhaa, Special Agent Kenneth Williams akaandika barua kwenda FBI makao makuu kuwapa tahadhari na kupensekeza ufanyike uchubguzi kwenye vyuo vyote vya urubani nchi nzima kwani anahisi kuna mapandikizi ya ugaidi ambao wanaweza kuleta madhara.

Nanukuu sehemu ya barua yake;

"…would like to advise the Bureau and New York of the possibility of a coordinated effort by Osama Bin Laden to send students to the United States to attend Civil aviation Universities and Collages. Phoenix has observed an inordinate number of indivie of investigative interest who are attending civil aviation Universities and collages in the state of Arizona.."

("..naishauri/naitahadharisha Idara na jimbo la New York juu ya uwezekano wa uratibu makini wa Osama bin Laden kutuma wanafunzi nchini Marekani kuhudhuria vyuo vya urubani. Phoenix tumegundua uratibu was watu kadhaa wenye kupaswa kuchunguzwa ambao wanasomea urubani katika vyuo mbali mbali jimboni Arizona..")

Barua hii ikatumwa makao makuh ya FBI.

Kwa utatibu wa Jamii ya Intelijensia (Intelligence Community) taarifa hii ilikuwa inapaswa pia kushirikishwa watu wa CIA.

Ajabu ni kwamba baada ya barua hii kufika makao makuu, wakubwa "wakaifinya" na kukaa kimya mpaka pale wafukunyuka katika Jamii ya Intelijensia walipokuja kuiona hii barua Mwaka 2002 tukio likiwa limeshatokea.

Kama hiyo haitoshi,



March 2001, Idara ya Ujasusi ya Italia, ilinasa mawasiliano ya simu ya wanachama wa kijiwe (cell) cha ugaidi nchini jijini Milan.
Baada ya kuchambua mawasiliano hayo wakagundua kuwa walikuwa wanaongelea mpango wa ulipuaji majengo Marekani kwa kutumia ndege.

Bila kuchelewa, Idara ya Ujasusi ya Italy ikawajulisha suala hiyo wamarekani.


Mwaka 2001, Idara ya Ujasusi ya Jordan iliwatumia taarifa serikali ya Marekani kwamba wana Intelijensia ya kutosha kujiridhisha kuwa Al-Qaida wanapanga shambulizi katika ardhi ya Marekani na wanahisi ndege zinaweza kutumika.

Mwezi huo huo July 2001, Idara ya Ujasusi ya Misri inawaonya wenzao wa Marekani kwamba wana Intelijensia inayoknyesha kwamba kuna watu 20 wamepenyezwa nchini Marekani na Al-Qaida na wanne kati ya hao ishirini wanasoma kwenye vyuo vya Urubani.


Mwezi August 2001, Mossad wanawapatia Wamarekani orodha ya watu 19 ambao wameingia nchini Marekani ambao Mosaad waliamini kuwa wameenda nchini humo kwa ajili ya kufanya Shambulio.

Mwezi huo huo August 2001, Idara ya Ujasusi ya Uingereza inatuma taarifa Mara mbili kuwa wana taarifa ya Intelijensia kuonyesha kuwa kuna magaidi wamepanga kufanya Shambulio ndani ya Marekani muda si mwingi.

Mwisho mwawezi huo wa August, Uingereza inatuma tena taarifa ya tatu na kuwaambia kuwa Shambulio wanalolihisi litatumia ndege.
Kuna ushahidi kuwa taarifa hii ya tatu ilipelekwa moja kwa moja kwa Rais Bush na Wasaidizi wake.



Mwanzoni mwa mwezi September 2001, kwa mara nyingine tena Idara ya Ujasusi ya Misri wanawasiliana na Marekani kuwataarifu kuwa wana Intelijensia ambayo inathibitisha kuwa magaidi waliopandikizwa nchini Marekani wapo kwenye "advanced stage" ya kutekeleza Shambulio siku chache zijazo.






Licha ya maonyo yote haya, tahadhari zote hizo na taarifa za Intelijensia zilizoshiba, je Rais Bush na wenzake walifanya nini??

NOTHING..!!


Yes, hakuna chochote ambacho walikifanya na kwenye taarifa zao za awali baada ya tukio pasipo kujua watu watafukunyua haya masuala, wanawadanganya Wamarekani kwamba "..hawakujua na wala wasingeweza kuhisi au kudhania Shambulio kama lile lingeweza kutokea.."

Huu ni "uongo uliotukuka" kwani ushahidi unaonyesha dhahiri kuwa walikuwa na taarifa za Intelijensia kuhusu 9/11 kabla haijatokea..
Na kama ni kweli ilikuwa ni Bahati mbaya, basi huu ulikuwa ni uzembe uliopitiliza ambao hawezi hata kutokea kwenye Idara zetu za Ujasusi kwenye nchi zetu za Ulimwengu wa tatu.




Nikirudi katika sehemu ya 12, nitaeleza mambo kadhaa yanayoashiria dhamira ya kwanini tukio hili la 9/11 liliachwa litokee. Tutaendelea Ijumaa..


Good Afternoon.!!
 
SEHEMU YA 11, POST # 1014


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu @charmie DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome
 
Back
Top Bottom