Wakenya wapo sahihi sana kwenye hili. Station ya Soga ilitakiwa iwe kubwa na ya kisasa zaidi kwani ina represent mkoa mzima wa Pwani, mkoa ambao ni unofficial Industrial region ya Tanzania.
Viwanda vingi sana vinajengwa mkoa wa Pwani na vingi zaidi vitajengwa si mbali sana na Soga, hicho ki station kama boksi karne hii hakifai kabisa. Designers wetu ni bogus kabisa.
Station ya Soga in a very near future itakuwa busy kuliko ya Dar kwa sababu Dar hakuna expansion ya jiji, expansion yoyote itaelekea magharibi ya Dar. Miaka 20 ijayo Soga station itakuwa katikati ya metropolis.
Watanzania tupo kama kipofu aliyeona punda.