Bei ya mafuta kuanzia Aprili 1, 2026: Petroli Dar imefikia TZS 3,820; Kagera ikigonga TZS 4,070. Dizeli ipo kati ya TZS 3,806 - 4,078

Bei ya mafuta kuanzia Aprili 1, 2026: Petroli Dar imefikia TZS 3,820; Kagera ikigonga TZS 4,070. Dizeli ipo kati ya TZS 3,806 - 4,078

Huyu mama ni kilaza kabisa!

Wafanyabishara wa mafuta wanapiga super profit sana
Kama alialika watu wamchangie na wakachanga unategemea Nini?

Mie naona effects za wale jamaa ndio zinaanza kuonekana the next 2. Umeme kukatika hovyo na kupanda

3. Gas kupanda japo tunayohapahapa nchini

4. Maji kuwa n shida hasa kwenye miji mikubwa


Hapo Bei za chakula na usafirishaj tutajikuta Ili siku Yako kwa mtanzia wa kawaida mambo yaende sawa at least 20,000/= ikatike hapo huna gari Wala pikipiki
 
Nimejaribu kuwaza tu kwa saiti.Serikali walidai kuna akiba ya mafuta ya miezi mitatu mbele inakuwaje leo wanaweka kigezo cha vita kama sanabu ya kupandisha bei?
 
Mbona inatisha mno!

Hii vita ilishabikiwa humu - kumbe inakuja kutuathiri vibaya mno!
Kumbe isingeshabikiwa mafuta yasingepanda bei.

Sasa mods si wawapige ban wanaoshabikia hiyo vita ili mafuta yashuke bei
 
Ifike tu ata ten ma nina zao tuone km wanaccm wao na sheli zao za kwenda kuchukua mafuta kwa 2000
 
CCM HAIJALI WANANCHI WAKE!!KODI KWENYE PETROL ZIPO 19 NCHI 53 ZA AFRICA ZIMEJARIBU KUWAJALI WANANCHI WAKE KWA KUPUNGUZA KODI LAKINI CCM HAWAJALI HILI ,KANYAGA TWENDE.UTASHANGAA MISAFARA ITAONGEZA KAMA KAWAIDA ,MBIO ZA KIBATARI ZITAENDELEA KAMA KAWAIDA HUKU BEI ZA MAFUTA ZIKIWA JUU
 
Siyo Kwamba EWURA wametumia April 1(Fools Day)?
Umejifungia ndani huna kazi mkuu?

Tuliopo road kitambo tumeona kila petrol station bei ni 3820 kwa petrol sasa unaposema sijui habari za sikukuu ya wajinga inasikitisha.
 
Wafanyabiashara wa bidhaa za vyakula nao hawatasubiri fursa iwapite utasikia kuanzia wiki hii tu bidhaa hazishikiki zitakuwa bei juu sana.

Hata mtu aliyekuwa na stock ya kutosha ya mchele atauza kwa kuzingatia trend ya soko hawezi kusubiri stock iishe ndiyo auze bei mpya.
 
Upande wa usafiri na usafirishaji nao soon utasikia nauli ipo juu hasa upande wa daladala na mabasi ya mkoani.

Milio itakuwa mingi sana kila kona na bahati mbaya hata mafuta yashuke nauli hazishuki ng'o watu wanaendelea kupiga pesa kutoka kwa masikini bila huruma.
 
Kuna wakati unajiuliza kazi ya LATRA ni kupandisha tu nauli?

Maana kama nauli itapanda kisa mafuta yamepanda, vivyo hivyo wanatakiwa kushusha nauli pale bei ya mafuta inapoporomoka.

Kuna wakati bei ya mafuta inakuwa chini mno wakati huo wananchi wanaendelea kuumia kwa nauli kubwa hali inayosababisha wengine washindwe kutoka kujitafutia riziki.
 
Umejifungia ndani huna kazi mkuu?

Tuliopo road kitambo tumeona kila petrol station bei ni 3820 kwa petrol sasa unaposema sijui habari za sikukuu ya wajinga inasikitisha.
Nakupata, lakini kwa jicho la Tatu. Ni kuwa EWURA wametuonyesha kuwa hatuko salama kabisa. Maana kama watu wanaweza kusimamia na kusema tuna reserve ya miezi mitatu na mwezi haujaisha unasema mafuta hayapo ( kupandiaha bei)! Hii ni hatari kubwa. Siamini ubinafsi umepitiliza hivi!

Narudia sisi hatuna Ugomvi na Iran, Urudi na kadhalika tunakosaje mafuta?
 
Hii ndiyo maana ya athari ya vita inayopiganwa mashariki ya kati.

Tulisema sana humu, ingawa hatuna uwezo kusitisha wala kuendesha vita kuna mashabiki uchwara walioshabikia vita hiyo.

Athari ya vita hii itamgusa kila mmoja bila kujali ushabiki wetu.
Na bila shaka bei itaendelea kupanda kadri vita itakavyo endelea
 
Sisiem sio wa kuwaamini
IMG_9571.jpeg
 
Nimejaribu kuwaza tu kwa saiti.Serikali walidai kuna akiba ya mafuta ya miezi mitatu mbele inakuwaje leo wanaweka kigezo cha vita kama sanabu ya kupandisha bei?
ilikuwa ni propaganda tu kuzuia taharuki kwa wananchi kuambiwa hali halisi kuwa mafuta yatapanda bei kutokana na mnyukano wa marekani/israel na iran
 
Stock kuwepo naamini ipo, ila kwenye kujishkilia kwa bei ya zamani ili wananchi wapate nafuu ndo mtiti, maana watakulaje kwa urefu wa kamba?
Kuwaamini hawa vibaka kunahutaji mtu ujitoe ufahamu sana though anything is possible, watu ambao hawajali wala hawathamini utu wa raia wala hawathamini mustakabali wa taifa wanaweza kufanya chochote, kusema lolote na kuamua mambo pasina kujali madhara yake.
Wao huangalia faida zao binafsi tu.
 
Back
Top Bottom