Bei ya Mafuta kushuka kwa Shilingi 29, Mnaelewaje hapa?

Hii hapa ni summary ya hotuba ya Waziri kuhusu Mafuta. Mnaonaje? Mnaielewa ama tumechezewa tu?

View attachment 2220833
Wewe ni WA wapi Mzee? Hizo tozo zilishushwa kipindi kile mafuta yaanza kupanda bei..
Hii hapa ni summary ya hotuba ya Waziri kuhusu Mafuta. Mnaonaje? Mnaielewa ama tumechezewa tu?
View attachment 2220833
Unapotosha kwa maslahi ya nani? Ukipotosha wewe unanufaikaje?

Hizo bei ni za zamani walipunguza hizo tozo mafuta yalipoanza kupanda lakini hazikusaidia kitu..

Punguzo la Sasa litakuwa Kati ya sh.200-250 Kwa ruzuku ya mwezi mmja.
 
Ndiyo. Walichelewa kulishughulikia na hiki wanachofanya sasa ni too little and too late. Hakuna sababu yo yote kwa nini majirani zetu wawe na bei za chini kuliko sisi wakati wengine ni landlocked....

Mipasho ya kila kitu kitapanda sababu ya vita. Kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba yake. Marekani bei iko chini kuliko sisi. Anayeona maisha magumu ahamie Burundi....na ubabaishaji wa huyu bwana mdogo wa Bumbuli umetoa picha mbaya kuwa hawajali. Hata hii nadhani wamefanya tu baada ya vilio kuzidi mitandaoni humu.

Kuna ombwe la uongozi...na kufanya maamuzi magumu kwa wakati na kwa faida ya wengi
 
Hizi 200 - 250 zitakuwa ni kwa lita moja au kila ukienda kuweka mafuta? Si waseme tu kiasi walichopunguza ili watu waelewe? Si kuna kitengo cha mawasiliano huko wizarani? Hata hili nalo ni la kushikiana mashati na kupayukiana mitandaoni humu?
 
Ndugu yangu unanionea bure tu Mimi.

Hilo ponguzo hapo juu ni sawa kabisa na Julma ya Billion 100 anayoitaka Rais.

Kipindi kile January alipunguza Shilingi 100 kila lita.

Sijui kama tumeelewana hadi hapo.
 
Walitoa ruzuku ya bilioni 100, wao hawatakusanya bilioni 102 kwa mwaka, hapo kuna bilioni 2 za ziada.

Ukisema waongeze kiasi maana yake wakatafute pesa nyingine mahala pengine kwa ajili ya kuongeza ruzuku ya bei ya mafuta.
 
[emoji81][emoji81][emoji81] hii nchi ngumu sana
 
Majiuliza sina majibu,kama hizo idara walibajeti kwa mwaka Yshs 1 bil na kutokana na ongezeko la bei makusanyo yameongezeka si waache kuendelea kukusNya.nazungumzi zile taasisi zinazocharge kwa % .
Pili tozo nyengine ziwe ni kwa shilingi moja moja kama zinainhia lita milion 400 maana yake watapata pesa hiyo 400 mil.

Ninachosikitika ni kuona pamoja nabpunguzo hilo ETI TUKOPE NJE KUFIDIA HIYO 100 BIL.
 
Lawama ziende kwa marekani na urusi kwa kuchochea vita huko Ukraine
 
Hivi hawa watu wapo serious kweli na hili swala la mafuta?? kwamba kikao na Rais nso kimepitisha hilo swala?? Siamini hata!!
Hiyo ndio huruma ya Rais... Yaani huwa nasema Mwigulu hamtakii Mama nia njema kwa Watanzania.. Ana penda watu waseme hii nchi imemshinda Mama. Kama Mama halioni hilo acha yamkute yatakayo mkuta.
 
Ndugu yangu unanionea bure tu Mimi.

Hilo ponguzo hapo juu ni sawa kabisa na Julma ya Billion 100 anayoitaka Rais.

Kipindi kile January alipunguza Shilingi 100 kila lita.

Sijui kama tumeelewana hadi hapo.
Una matatizo ya uelewa
 
Mfumo mbovu wa Ujamaa umefilisi nchi ndiyo maana hata jambo la dharula likitokea kwa mfano vita ya Ukraine kupandisha bei ya mafuta dunia nzima, serikali haina hela ya kutoa ruzuku, haina uwezo wa kupunguza tozo. Hata zile enzi za Nyerere, ilivyotokea vita ya Kagera uchumi uliachwa hoi maana Ujamaa ulioanza na Azimio la Arusha tayari ulishaharibu uchumi.
 
CCM wanatakiwa wapimwe akili zao, inaonyesha wana akili za uzandiki sana. Kama nchi tujitafakari hawa watu watakuwa wanatuharibia nchi yetu. Kama kweli hilo ndilo punguzo basi watoke ofisini wajiudhuru kabla ya 2025
 
Sasa ukipunguza 200 au 250 kwenye 3,258 utakuwa umesaidia nini, ikiwa mwanzo bei zilikuwa kwenye 1800......hii inakuwa sawa na kucheza sarakasi...
 

Lita ya mafuta Zanzibar ni 2,600 sasa unaposema ni tatizo la dunia sijui Zanzibar iko sayari gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…