Umefikiria sana na kuja na tafsiri yako ya namna ulivyofikiri...
Lakini mimi nafikiri tofauti na wewe, kwamba;
1. Hiyo jumla ya tozo ya Tshs bilioni 102 zinazoondolewa na serikali ni sehemu ya nafuu inayotengenezwa na serikali kwa wananchi...
2. Ukijumuisha na subsidize/ruzuku ya Tshs bilion 100 inayoanza kutolewa na serikali kama walivyosema kuanzia 1 Juni, 2022, maana yake serikali itabeba gharama ya wananchi wake ya jumla ya Tshs bilioni 202..
3. Mpaka hapo, kama mtazamo wangu uko sahihi, basi ukikokotoa bei mpya, inawezekana ikapungua kwa kati ya Tshs 350 na 600 kwa lita...!!
## Hii ndiyo tafsiri yangu mimi...