Bei ya Mafuta kushuka kwa Shilingi 29, Mnaelewaje hapa?

Ndugu yangu acha uongo.
Mleta mada yuko sahihi na ukweli.
Taarifa yake iko rasmi kwenye taarifa za serikali iliyotolewa kwa umma iliyotolewa 10/May/2022. Ni kweli kabisa hiyo ruzuku aliitangaza makamba bungeni jana itapunguza shilingi 29 tu kwenye kila lita ya Petrol kwenye bei ya sasa.

Kama huamini, tazama hiyo picha ya mchanganuo uone ni tangazo la lini, kama hutaona ni tarehe 10/may/2022.
 
Ruzuku ya bilioni 100 kwa nchi nzima yenye watu milioni 60 unafikiri ingekupa punguzo gani? CCM kama hauwajui, utahangaika sana!
Hivi hawa watu wapo serious kweli na hili swala la mafuta?? kwamba kikao na Rais nso kimepitisha hilo swala?? Siamini hata!!
 
Kuna mtu anasema hiyo Billion 100 wabaki nayo.
 
Lita ya mafuta Zanzibar ni 2,600 sasa unaposema ni tatizo la dunia sijui Zanzibar iko sayari gani.
Swali zuri sana; ila ni kweli kuwa sehemu nyingi sana za dunian zinakaribiana na tatizo la bei ya mafuta ispokuwa zile zenye kuchimba mafuta tu. Kuna serikali nyingine zinaweka ruzuku kubwa kwenye bei ya mafuta kuwanusuru raia wake, inawezekana Zanzibar nayo imeweka ruzuku au inapewa msaada wa mafuta ya bure kutoka kwa wachimabji.
 
Leo nimetoa laki nikawekewa wese lita 30 na kasoro....roho bado inauma kinyama yani
 
Nakumbuka tu alivyokuwa amepiga nne eti anawasikiliza wawekezaji wa kwenye gas anataka mchakato uanze haraka sana tumechelewa.

Inventory planning ya kuagiza mafuta kuelezea anaona anatoa somo gumu kweli watanzania kumuelewa. Sasa huko kwenye gas ambapo kuna scenarios za inflation, probability za return za low, medium na high kutokana external environment factor hizo hizo za mafuta only this time watu wanataka chao inabidi nchi ikose mapato, sensitivity analysis ya kupanda na kushuka bei za gas, weighted average costs of capital, capital structure ya hiyo $30 billion imetokea wapi, deal za interet na nonsense kibao za finance kuzi-mention hadithi ndefu.

Bi Tozo anakwambia January Makamba ndio mtu sahihi wakuratibu zoezi la uwekezaji wa uchimbaji wa gas na January mwenyewe anaongea hadharani confidently hilo jukumu analimudu.

Waliokuwa wanadengua kwenye huo uwekezaji hawakuwa wapuuzi it’s part of the negotiation tactic ata ikichukua miaka 10 muhimu ni mkataba sahihi na wenye tija, unataka wao wakubembeleze kama Museveni alivyowafanyia kwa kuweka demands sio wewe ubembeleze; huo mkataba wa mafuta autowekwa hadharani kamwe kwa jinsi tulivyoingia kichwa kichwa.

Inventory ya mafuta na stabilisations ya prices shida, halafu anataka kujifanya mjuaji kwenye mikataba ya uchimbaji wakati hakuna anachojua zaidi ya local content sijui nani aliwaambia hizo ndio ‘nitty gritty’ za mkataba wenyewe, binafsi nilipomuona na wawekezaji nikawa najiuliza hivi anaongea nini kuhusu mikataba mtu mwenyewe clueless.

Nchi inauzwa in Ndugai’s voice.
 

Utetezi wa kulazimisha.
 
Hii hapa ni summary ya hotuba ya Waziri kuhusu Mafuta. Mnaonaje? Mnaielewa ama tumechezewa tu?
View attachment 2220833
Hii Taarifa sio sahii kwa kigezo kuwa, Mama ametoa shs Billion 100 kwa mwezi June pekee; na hiyo taarifa inasema Bilioni 102 kwa MWAKA mzima hivyo ni feki (FAKE NEWS!)
 
Hii Taarifa sio sahii kwa kigezo kuwa, Mama ametoa shs Billion 100 kwa mwezi June pekee; na hiyo taarifa inasema Bilioni 102 kwa MWAKA mzima hivyo ni feki (FAKE NEWS!)
Unazani hiyo billioni 100 itapunguza Nini?

Fanya 100,000,000,000 gawanya kwa lita wastani wa matumizi ya Mafuta kwa mwezi utapata mlemle.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…