Bei ya mafuta soko la dunia imeshuka chini ya Dollar 90 Kwa pipa moja Ila EWURA wanasema imepanda

Kwa hizi bei zao za kiboya wanazotupiga hata wangetaka kufanyia mkutano sayari nyingine wasingeshindwa. Awamu yao hii, wacha wale.
 
Msipende kupotosha,wamesema mwezi ujao mafuta yatashuka ila haya yanayotumika sasa yalinunuliwa kipindi Bei ikiwa juu.
Wewe sasa ndo unatuvuruga! Walinunua bei ikiwa juu, lini? Tangu bei imeanza kupanda hapa nchini, haijawahi kushuka hata baada ya kudanganya na ruzuku ambayo kimsingi inaliwa tu.

Tunajua kuwa soko la dunia, zaidi ya miezi 2 sasa bei imeshuka.

Sasa wewe utuambie, stock ya nchi ina last for how long na bulk ya mwisho ambayo ndio tunayotumia sasa ililetwa lini ili tuone kama kuna justification ya kupandisha bei kwa zaidi ya sh 340 kwa lita ndani ya miezi 2 tu.

Bei inayoongezeka kila mwezi inatokana na nini ukilinganisha na stock iliyopo? Hiyo bidhaa itakayouzwa mwezi wa 8 imeshaingia nchini? Iliagizwa lini? Kwa bei gani imeagizwa ili tuone kama kweli kuna haja ya ruzuku au ndo wanachukua ili kuwahonga kina Uwoya?

Au serikali yenu nayo haina transparency na hasa kwenye hali ngumu kama hii?
 
Mafuta huwa yananuniliwa miezi 2 kabla,kwa mfano mafuta ya kutumika mwezi ujao yaliagizwa toka mwezi wa 7..ndio maana Ewura wamewaambia Bei zitapungua kidogo mwezi ujao..

Mafuta hayaagiswi kama kwenda Duka la Mangi.
 
EWURA wao ikipanda huko hata kama walinunua miezi 3 iliyopita watapandisha tu¡ lakini ikichuka uwii huwaoni kamwe.[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Waendesha nchi wanafanya biashara ya mafuta. Kwenye Roma ya zamani, wanasiasa hawakurusiwa kufanya biashara. Sasa leo unaweza kuta hata 30 % ya wabunge wana vituo vya mafuta.
 
Mafuta huwa yananuniliwa miezi 2 kabla,kwa mfano mafuta ya kutumika mwezi ujao yaliagizwa toka mwezi wa 7..ndio maana Ewura wamewaambia Bei zitapungua kidogo mwezi ujao..

Mafuta hayaagiswi kama kwenda Duka la Mangi.

Y yasibaki na b ya long
 
Halafu linakuja humu, eti tuna mama. Tozo kama zote, mafuta juu, halafu yuko busy na safari.
 
Kupanda kwa mafuta ni fursa kwa wajasiliamali ukifunza kutengeneza diesel na petrol utapiga pesa nyingi Sana wao wanauza 3500 we uza 3000 kwa lita. Hivi vitu muhimu vilivyopanda bei mfano vifaa vya ujenzi na mafuta ukitengeneza mbadala wake then uza kwa bei ya chini utapata pesa nyingi Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…