Bei ya mafuta ya petroli, dizeli toka Urusi sasa ni $30 kwa pipa. China na India wachangamkia fursa. Kwanini Tanzania isifanye hivyo pia?

Mwamba wa Dunia USA wakisikia tutapigwa ban IMF, WORLD BANK, na kuzuiwa kuuza chochote duniani
Waulize ma Ayattollah wa Iran nchi yao inavyoteseka
Unauhakika na kuteseka huko!? Brics inakuja.
 
Mwamba wa Dunia USA wakisikia tutapigwa ban IMF, WORLD BANK, na kuzuiwa kuuza chochote duniani
Waulize ma Ayattollah wa Iran nchi yao inavyoteseka
... ni rahisi zana kwao; they will just disconnect us from SWIFT; that simple. Hakuna kununua wala kuuza.
 
Nakumbuka Mzalendo #1 aliwahi kusema tutumie fulsa ya kuuza chakula kwenye nchi zilizokuwa na njaa watu wakamjia juu na kusema huwezi kuombea mwenzio apate njaa ili wewe unufaike.
Yap, mara zote ni vigumu kukubali ukweli na hata ukiukubali bado utaufanya kwa njia nyingine kuepuka kuonekana unafanya kutoka kwa aliyesema ukweli.

Na issue ya ununuzi wa mafuta yasiyo safishwa ndg waziri akiona fulsa hiyo lazima atengeneze issue ya 10% kufufua zile mashine za tipper ili tuyanunue, vinginevyo hayana kazi yakifika.
 
Ukisikiliza viongozi wetu wanavyoongea kwenye vyombo vya habari, utajua kabisa kwamba hapa hatuna viongozi.. kuwaambia wachangamkie fursa ya mafuta ya Russia ni kuwatwika zigo wasiloweza
 
Hapo unazungumzia crude Oil. Sasa sisi tukinunua hiyo crude oil tutaiweka wapi. Hatuna refinery wala nini. Sisi tupambane na petroli zetu tu
Siku zote ukisikia bei ya mafuta kwenye soko la dunia hua wana maana ya crude oil na sio petrol, diesel nk. Well, OPEC kwa ujumla wake leo wanauza dola 130 hiyo hiyo crude oil
 
Mleta mada unaongelea Crude oil "Mafuta ambayo hayajasafishwa" Hao India na China wanazo Refinery za kusafisha hiyo Crude oil,
Sasa Bongo wakinunua hizo Crude oil watasafishia wapi? ni lazima uwe na Refinery.
Kusimika mitambo ya kuchuja inagharama kiasi gani? Au kutafuta mwekezaji alete mzigo wa refinery na ifanyike hapa nchini
 
Tunaweza kununua kupitia Marafiki zetu China na India, hakuna vikwazo

Wao wanayo refinery, na watatupa unafuu

Makamba afufue TIPER , refinery yetu
Makamba hana akili ya kufufua refinery, bali ana akili ya kuiba tu kura.
 
Wahenga walisema, 'Kufa kufaana'. Kwenye kila tatizo linalotokea hapa duniani huwa linafungua fursa kwa baadhi kufaidika nalo. Badala ya kukaa tunalialia linapotokea tatizo, tunapaswa kutazama upande wa pili wa shilingi kwamba tutafaidikaje na hilo tatizo. Hata lile tatizo kubwa la mlipuko wa covid 19, yapo makampuni na nchi zilizopiga pesa ile mbaya wakati wengine wakiwa wameji lockdown na zingependa mlipuko huu wa covid 19 uendelee kudumu!

Hii vita ya Urusi na Ukraine, mara tu ilipoanza nchi kama za Saudi Arabia na zingine zote za OPEC ziliona ni fursa, na zikaanza kupandisha bei ya mafuta yao. Nchi za Ulaya na Amerika walipoamua kususa mafuta ya Russia, nchi za OPEC na Saudia zikachangamkia fursa hiyo kwa kasi zaidi ya kuendelea kupandisha bei ya mafuta yao na hadi sasa yamefikia zaidi ya $ 120 kwa pipa. Kabla ya vita hii pipa lilikuwa linauzwa si zaidi ya $ 70. Nchi zingependa vita hii iendelee kudumu!

Russia ni mzalishaji mkubwa duniani wa mafuta haya ya petroli/ diseal na na gesi kwa kiwango cha theluthi moja ya mafuta yote duniani. Baada ya vita hii na nchi za Ulaya na Amerika kuanza kususia mafuta yake, Urusi imeteremsha sana bei ya mafuta yake hadi sasa kufikia $ 30 kwa pipa! Uchina na India wamechangamkia fursa hii, wananunua mafuta haya kutoka Russia na wangelipenda vita hii iendelee kudumu! Tukumbuke kuwa population ya China na India ni zaidi ya watu billion 3, yaani theluthi moja ya population ya dunia hii. Wao hawafungamani na upande wo wote kama sisi.

Sasa kwa nini na sisi tusichangamkie fursa hii ( na kupenda iendelee kudumu) kwa kununua mafuta haya toka Russia? Kuna tatizo gani tukifanya hivyo? Tunaogopa nini? Au watalaamu wety wa uchumi mnasemaje?

Usikute hata sasa wananunua huko ila tunapigwa
 
... ni rahisi zana kwao; they will just disconnect us from SWIFT; that simple. Hakuna kununua wala kuuza.
Bado kidogo tu Putin anaenda kuwa LORD OF THE WORLD !! by VANGA BWANGA !!
 
Wabongo mna maneno mepesi sana. Hivi mnajua gharama za kujenga refinery au hata kuifufua hiyo ya zamani? Ni zaidi ya 10 billion USD. Huyo mwekezaji yuko wapi? Na mpaka hiyo refinery ikamilike bado Urusi watakuwa kwenye vikwazo tuu na kulazimika kuuza mafuta yao kwa bei ya chini?
 
Hivi ilikuwaje Nyerere kwa miaka ile aliweza kuwa na uchumi wa viwanda hadi kuwa na refinery pale TIPER ambapo tulikuwa na uwezo wa kuagiza crude oil na kusafisha wenyewe, hivi kuna watu ambao mnahisi kama mimi kwamba kuna kitu hakiko sawa kwenye namna ambayo nchi yetu inatafsiri hatua za kimaendeleo (development realization)......
 
Hata enzi za Nyerere na TIPER refinery bado tulikuwa tunaagiza mafuta na bado kulikuwa na uhaba wa mafuta. TIPER ilikuwa ni refinery ndogo.
 
Ukisikiliza viongozi wetu wanavyoongea kwenye vyombo vya habari, utajua kabisa kwamba hapa hatuna viongozi.. kuwaambia wachangamkie fursa ya mafuta ya Russia ni kuwatwika zigo wasiloweza
Hata hivyo wananunua Rusia lakini wanauza bei mara 10 ya manunuzi
 
Beberu ni mtu mbaya sana. Usishangae ndiye anayenunua mafuta ya Russia kwa mgongo wa India na wenzake.
Hata hivyo ushauri wako kwa nchi yetu ni muhimu sana. Sijui balozi wetu Moscow anafanya kazi gani.
Wahenga walisema, 'Kufa kufaana'. Kwenye kila tatizo linalotokea hapa duniani huwa linafungua fursa kwa baadhi kufaidika nalo. Badala ya kukaa tunalialia linapotokea tatizo, tunapaswa kutazama upande wa pili wa shilingi kwamba tutafaidikaje na hilo tatizo. Hata lile tatizo kubwa la mlipuko wa covid 19, yapo makampuni na nchi zilizopiga pesa ile mbaya wakati wengine wakiwa wameji lockdown na zingependa mlipuko huu wa covid 19 uendelee kudumu!

Hii vita ya Urusi na Ukraine, mara tu ilipoanza nchi kama za Saudi Arabia na zingine zote za OPEC ziliona ni fursa, na zikaanza kupandisha bei ya mafuta yao. Nchi za Ulaya na Amerika walipoamua kususa mafuta ya Russia, nchi za OPEC na Saudia zikachangamkia fursa hiyo kwa kasi zaidi ya kuendelea kupandisha bei ya mafuta yao na hadi sasa yamefikia zaidi ya $ 120 kwa pipa. Kabla ya vita hii pipa lilikuwa linauzwa si zaidi ya $ 70. Nchi zingependa vita hii iendelee kudumu!

Russia ni mzalishaji mkubwa duniani wa mafuta haya ya petroli/ diseal na na gesi kwa kiwango cha theluthi moja ya mafuta yote duniani. Baada ya vita hii na nchi za Ulaya na Amerika kuanza kususia mafuta yake, Urusi imeteremsha sana bei ya mafuta yake hadi sasa kufikia $ 30 kwa pipa! Uchina na India wamechangamkia fursa hii, wananunua mafuta haya kutoka Russia na wangelipenda vita hii iendelee kudumu! Tukumbuke kuwa population ya China na India ni zaidi ya watu billion 3, yaani theluthi moja ya population ya dunia hii. Wao hawafungamani na upande wo wote kama sisi.

Sasa kwa nini na sisi tusichangamkie fursa hii ( na kupenda iendelee kudumu) kwa kununua mafuta haya toka Russia? Kuna tatizo gani tukifanya hivyo? Tunaogopa nini? Au watalaamu wety wa uchumi mnasemaje?

Hata enzi za Nyerere na TIPER refinery bado tulikuwa tunaagiza mafuta na bado kulikuwa na uhaba wa mafuta. TIPER ilikuwa ni refinery ndogo.
Ndo maana nikasema kama tulikuwa na refinery ndogo enzi za mwalimu, kwenye kutathmini hatua za kimaendeleo leo hii tulitakiwa tuwe na refinery kubwa ambayo ingeweza kusafisha hadi mafuta ya nchi jirani......
 
Back
Top Bottom