Chiwa
JF-Expert Member
- Apr 17, 2008
- 4,116
- 4,979
hawa inabidi warudi kwenye kilimo cha mahindi marekani darasa la sita jiografia ya ulimwengu ambapo zaidi ya 80% inatumika kwa mifugo! kiukweli nilikuwa naona kama wanadanganya kwa jinsi ninavyoupenda ugali lakini kwa mazingira ya sasa inabidi mahindi yatumike kwa mifugo kama kutengenezea chakula cha kuku na nguruwe na huko ni wafugaji wazuri tu inaweza kulipa.Uko sahihi Mkuu, huku Mpwapwa vijijini, wakulima wanauza debe 3500 - 4500
mfano ikiwa nguruwe anakula kilo mbili kwa siku unahitaji jumla ya kilo 60 kwa mwezi na kilo 240 kwa miezi minne ambayo sawa na gunia mbili za mahindi kwa mahindi ya dodoma yalivyo mazito ambapo nguruwe huyo atakuwa na kama kilo 70 kama atalishwa vizuri.
ikiwa kilo moja itauzwa shilingi 4000 mkulima atapata jumla ya mauzo 280,000/- ukilinganisha na gunia mbili zenye thamani ya shilingi 54,000/- kwa sasa.
hivyo akitoa 54,000 za chakula ,30,000 za bei ya nguruwe na 16,000 matibabu unabaki na 180,000 wakati gunia likipanda litafika 60,000 sasa kwa gunia mbili 120,000 ukitoa gharama thamani ya mwanzo 54,000 unapata 66,000 gharama za kuhifadhi 10,000 faida inaweza kuwa haizidi 50,000 kwa gunia mbili. haitoshi hata kulimia kwa trekta ekari mbili wakati faida ya nguruwe inalima ekari 6 na kama kila ekari italeta gunia tano yaweza leta gunia 30 zinazoweza kusaidia ufugaji wa nguruwe 15 na kuleta pato la 180,000x15=2,700,000.
hapo vipi!