Bei ya petroli Zanzibar ni Tsh 2600 kwa lita. Bara bei ipo juu zaidi

Bei ya petroli Zanzibar ni Tsh 2600 kwa lita. Bara bei ipo juu zaidi

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Kudadadeeeki walahi ayaaaaa ukisikia kulamba asali ni huko zenji aiseeeee ina maana vita vya ukraine effects zake hazifiki zenji? hivi kule wamachinga walitimuliwa?

Sitashangaa kusikia hata mfumuko wa bei haujaathiriwa na vita vya ukraine au nchi mbili tofauti hizi?

zenji mafuta.jpeg
bara mafuta.jpeg
Screenshot 2022-05-04 at 22.06.12.png
 
Zenji hawana Tozo nyingi...tozo zikishakatwa bara zanzibar wanamgao wao inform of umeme, madawa e.t.c sawa na wanadanga lao linaitwa Tanganyika.

Hio sio sababu sababu ni kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania iliyopewa mamlaka kikatiba kujiamulia na inajiendesha yenyewe mambo yasiyo ya muungano mfano Kodi na Mengineyo mengi usitegemee Zanzibar kufanana na bara sababu kuna mambo Rais wa Jamhuri ya muungano hana mamlaka nayo

Mfano JWTZ na Polisi wanatii amri ya Rais wa Jamhuri ya Tanzania sasa ulitegemea wao kodi zao kugharamia JWTZ na Police wetu?

Kuwalaumu Zanzibar wakati wao wanatumia kodi zao kuendesha serikali yao ni ujuha Zanzibar wana autonomy kitu ambacho Wa Tanzania wengi hawakijui sababu ya elimu ndogo
 
Hio sio sababu sababu ni kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania iliyopewa mamlaka kikatiba kujiamulia na inajiendesha yenyewe mambo yasiyo ya muungano mfano Kodi na Mengineyo mengi usitegemee Zanzibar kufanana na bara sababu kuna mambo Rais wa Jamhuri ya muungano hana mamlaka nayo...
Lakini unakubali bara tunawahudumia Zanzibar? Kwa cost ya Muungano.
 
Lakini unakubali bara tunawahudumia Zanzibar? Kwa cost ya Muungano.

Tanzania inawahudumia nini?

Bajeti ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar haigharamiwi na TRA wao kama Zanzibar wa Mamlaka yao inayokusanya kodi Zanzibar na hiyo pesa ndio ndio inayotumiwa na SMZ/Zanzibar

Jeshi la wananchi JWTZ nje ya jeshi ni mtu mmoja tu anaetoa Amri nae ni rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania sasa ulitaka Jeshi la rais wa Jamhuri ya Tanzania ligharamiwe na serikali ya Mapinduzi Zanzibar? Hivyo hivyo kwa jeshi la Polisi
 
Zanzibar wana Rais mwenye akili na anajua kuzitumia.

Kuwa kiongozi sio kutumia pesa nyingi kucheza movie na kuendeshwa kwa v8, maana halisi ya uongozi ni kuzitambua changamoto zinazokuja, na zilizopo, kuzishughulikia mapema kwa ajili ya unafuu ya wale waliokupa dhamana ya kuwaongoza.

Sio kila ukiulizwa tatizo nini, jibu ni lilelile bei ya mafuta imepanda kwasababu ya vita ya Urusi, vipi hiyo vita isipoisha? bei ya mafuta itaendelea kupanda mpaka lini?

Kama uongozi umewashinda, kistaarabu tu waitishe uchaguzi mkuu mapema, tupate viongozi wapya watakaotumia bongo zao kutuondoa kwenye hii mikwamo, waje na immediate short term plan, na long term plan, ili kuwanusuru wenye kipato cha chini.
 
Muungano wa faida! Visiwani wanatafata sheria ya kiislamu kwenye biashara huku wakilipiwa na bara kila kitu.
mkopo usiokuwa na riba ila bara mtawalipia tu.
Umeme toka bara.
Mafuta
Vyakula
 
Back
Top Bottom