Bei ya sukari yaanza kupaa na bei ya unga yazidi kuongezeka

Bei ya sukari yaanza kupaa na bei ya unga yazidi kuongezeka

toplemon

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
4,612
Reaction score
4,721
Jamani bei ya sukari imeanza kupanda sasa kilo ni 3200 huku bei ya unga nayo ikipanda sana hadi 2100 kwa kilo

Sukari ni baada ya serikali kupiga marufuku kuingiza sukari kutoka nje?

Nashindwa kuelewa kwanini bidhaa nyeti kama sukari izuiwe kutoka nje kwa maneno eti wanalinda viwanda vya ndani?
Viwanda vya ndani vinalindwa vipi wakati sukari inapanda?

Nakumbuka wakati wa tatizo la sukari nchini mwaka 2016 kama sikosei ilisababishwa na haya haya mambo ya kuzuia sukari kutoka nje isiingie mwisho tukaliingiza taifa kwenye hatari kubwa

Serikali inapaswa ihamasishe export zaidi lakini haimaanishi kubana watu wanao-import bidhaa nchini hususan sukari na vyakula muhimu ambavyo uwepo wa bidhaa shindani unasaidia kuondoa mfumuko

Serikali kwanini suala la mfumuko haitilii maanani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na salary kwa Watumishi wa Umma miaka yote haitoshi na bado iko pale pale kama ilivyokuwa 2015!
 
Huku kwetu sukari ni 2600 kwa Kg..Uzuri sukari haiharibiki kama ishaanza kuwa hivyo kwa angalizo hili ngoja ninunue ya kutosha. Huo unga sina tatizo nao.
 
Huku kwetu sukari ni 2600 kwa Kg..Uzuri sukari haiharibiki kama ishaanza kuwa hivyo kwa angalizo hili ngoja ninunue ya kutosha. Huo unga sina tatizo nao.
Fanya hivyo mkuu kabla US hajatuwekea vikwazo zaidi
 
Back
Top Bottom