Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Hunyu

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
4,774
Reaction score
4,327
Kwa muda mrefu nimekuwa nikikerwa na hili jambo.

Bei ya chakula cha hizi hoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri haiendani na huduma wanayopewa lakini naona mamlaka husika zimekaa kimya. Na hili naomba lisichanganywe na suala la wakulima kujipangia bei, msafiri sio mkulima ni mtu anayekuwa hana option maana pengine amesafiri masaa kumi na mbili au ishirini bila kuonja kitu na analazimishwa anunue chankula kwa bei ya juu. Au anaenda hospitali kupeleka mgonjwa.

Kiuhalisia sahani ya wali nyama ni 1500 - 2000 lakini kwenye hiyo migahawa wali nyama wanauza 5000 - 6000. Mbaya zaidi vile vidada vihudumu vinanyodo utafikiri vinahudumia hoteli ya nyota tano kumbe mgahawa wa barabarani tena kwa wasafiri (ref: nangurukuru). Ukiviambia dada ongeza kidogo basi ili nishibe kanakukata jicho utafirikiri umetoa mawe kumbe umetoa 6000.

Wanaosafiri wengine ni wagonjwa, watu wa vijijini na wengine hawajiwezi kabisa, unapomlazimisha mtu kuwa tutachimba dawa hoteli fulani na kupata chakula hapo ni ukiukwaji wa haki za wasafiri. Kwanini mamlaka wasimoderate na kucontrol hili suala? ikiwezekana sehemu ya kuchimba dawa ijitegemee na sehemu ya kula ijitegemee ili hao watoa huduma wasiwalipishe watu bei kubwa kisa umechimba dawa kwao.

Madereva na makondacta wao huwa hawalipii hiki chakula kwasababu ni deal kwa mwenye hicho kihoteli. hii ni ajabu sana, ndio maana inapelekea hawa madereva wanawapeleka abiria sehemu ambayo mwisho wa siku watalazimika kulipia hata kama hawataki.

Naomba mamlaka husika waaanze na Nangurukuru, Singida, Shinyanga, Morogoro, Alj jazeera na sehemu zingine ambazo mimi sijafanikiwa kupita huko kwasababu inakera sana na ni ukiukwaji wa haki za wasafiri kabisa kuwalazimisha kupata huduma wasipopenda halafu mbaya zaidi kwa bei ya juuu kuliko uhalisia.

Bei ya choo cha kulipia inajulikana ni 300, Bei ya wali maharage inajulikana 1500-200, bei ya wali kuku inajulikana ni 3000-4000, bei ya kile kitake away inajulikana kuwa ni 300. Iweje tutozwe bei zisizoendana na uhalisia?

Wakuu wa nchi wao husafiri na private mara nyingi kwahiyo hii inweza isiwe na mashiko sana kwao, lakini kiuhalisia vyombo vya dola na mamalaka za miji na halimashauri ambako huduma hizi hutolewa inabidi walichukulie serious.

Wakuu Nawasilisha, naomba ndugu zangu tusaidiane kupinga huu unyanyasaji kwa abiria.

Pia soma

Kuna ka mgahawa kapo Chalinze aisee kuna siku nimenunua mishikaki pale nakuja nayo ktk gari imeoza kbsa! bahati mbaya hiyo siku sikuwa ktk akili zangu nikachukua panga (ni sime) nikarudi pale ktk ki mgahawa kile nikamwaga vyakula vyoote pale jikoni nikaondoka zangu sikusema na mtu.
 
Soko huria, serikali ikipanga bei za mazao tunailalamikia, wacha soko lipange bei, ni fursa pia kwa wanaotaka kuuza cha kula kwa bei ndogo wakafungue mahoteli ili ushindani uwe mkubwa.

Mwisho kabisa sio lazima kula njiani, nunua maji na korosho za kutosha utakula unapoenda kama una watoto mwambie mama yeyoo awapakilie vyakula.
 
kuna ka mgahawa kapo chalinze aisee kuna siku nimenunua mishikaki pale nakuja nayo ktk gari imeoza kbsa! bahati mbaya hiyo siku sikuwa ktk akili zangu nikachukua panga (ni sime) nikarudi pale ktk ki mgahawa kile nikamwaga vyakula vyoote pale jikoni nikaondoka zangu sikusema na mtu.
Wakwere waogo ndio maana hawakukufanya kitu. hahah
 
Soko huria, serikali ikipanga bei za mazao tunailalamikia, wacha soko lipange bei, ni fursa pia kwa wanaotaka kuuza cha kula kwa bei ndogo wakafungue mahoteli ili ushindani uwe mkubwa.
Mwisho kabisa sio lazima kula njiani, nunua maji na korosho za kutosha utakula unapoenda kama una watoto mwambie mama yeyoo awapakilie vyakula.
Kwa taalifa yako Korosho ukila nyingi lazima ushikwe na tumbo la kuhara pia chakula cha kwenye hizo migahawa hakifanani na bei kinavyouzwa na hakina ubora.Nadhani wewe ni mtoto wa mama/kula kulala hujawahi kusafili na ukisafili huwa umebebwa mgongoni kwa Mama.
 
Niliuziwa chips kavu buku 3 jero,alafu hazina hata kachumbali,zimekaangiwa mafuta ya nyama [emoji23]
Mie sili chips safarini, nilishawahi kupatwa na masahibu. Nilitoka Moshi kwenda Dar, tulivyofika Mombo tukaingia kula hoteli inaitwa Liverpool, nikala viwepe na mishikaki. Uwiiiiii yaani hata hatujafika mbali, tumbo likaanza kuuma, mharo unataka kuchomoza.

Nikawaza, nikimwambia konda nataka "kuchimba dawa" atasema hilo zoezi ilikuwa lifanyike hotelini tulipokula. Basi bwana akili ikaja ya ziada, nikamwendea konda, nikamdanganya kuwa NIMEANZA KU BLEED GHAFLA hivyo wasimamishe gari nikajisetiri, hahahaha, konda kusikia hivyo akamwambia dreva, gari ikasimama nikaenda kwenye hoteli mshenzi mshenzi, nikahariiiiiiishaaaaaa mpaka basi!
 
Chai ndio? Kusema nadanganya ama? kama una maana hiyo sikulazimishi ukubali lakini sisi ndio tunaishi hivyo, maana mpaka unaniuzia kitu unajua kabisa kimeharibika wewe umejiandaa kwa lolote, mm sipendi kuonewa ama kuchukuliwa poa na ikitokea ukanifanyia huwa nafanya jambo ambalo hukuwahi waza kuwa litakutokea hata siku moja.. mimi ni mmoja ya wale wanaotembea zaidi ya siku mbili hawajalala sipendi unyonge..iwe ndan au nje ya nchi. so ndugu ni tukio la kawaida sana hilo
 
Kwa taalifa yako Korosho ukila nyingi lazima ushikwe na tumbo la kuhara pia chakula cha kwenye hizo migahawa hakifanani na bei kinavyouzwa na hakina ubora.Nadhani wewe ni mtoto wa mama/kula kulala hujawahi kusafili na ukisafili huwa umebebwa mgongoni kwa Mama.
Naamini katika ushindani na soko huria, sasa kwanini ujisumbue kununua chakula kisichofanana na gharama ulizolipia, andaa nyumbani hutopata hiyo kadhia.
 
Mie sili chips safarini, nilishawahi kupatwa na masahibu. Nilitoka Moshi kwenda Dar, tulivyofika Mombo tukaingia kula hoteli inaitwa Liverpool, nikala viwepe na mishikaki. Uwiiiiii yaani hata hatujafika mbali, tumbo likaanza kuuma, mharo unataka kuchomoza. Nikawaza, nikimwambia konda nataka "kuchimba dawa" atasema hilo zoezi ilikuwa lifanyike hotelini tulipokula. Basi bwana akili ikaja ya ziada, nikamwendea konda, nikamdanganya kuwa NIMEANZA KU BLEED GHAFLA hivyo wasimamishe gari nikajisetiri, hahahaha, konda kusikia hivyo akamwambia dreva, gari ikasimama nikaenda kwenye hoteli mshenzi mshenzi, nikahariiiiiiishaaaaaa mpaka basi!
Hapo Shukuru Hotel ilikuwa karibu lasivyo kichaka kingekuhusu.😀😀
 
Hapa tutarudi enzi za miaka ya 80's, nakumbuka tukiwa tunasafiri na bi-mkubwa ilikuwa lazima apike chakula cha safari kwenye kimfuko cha naironi then kinatunzwa kwenye kikapu... mzee ukijisikia njaa tu bi-mkubwa anafungua kifuko acha kabisa.
 
Mie sili chips safarini, nilishawahi kupatwa na masahibu. Nilitoka Moshi kwenda Dar, tulivyofika Mombo tukaingia kula hoteli inaitwa Liverpool, nikala viwepe na mishikaki. Uwiiiiii yaani hata hatujafika mbali, tumbo likaanza kuuma, mharo unataka kuchomoza. Nikawaza, nikimwambia konda nataka "kuchimba dawa" atasema hilo zoezi ilikuwa lifanyike hotelini tulipokula. Basi bwana akili ikaja ya ziada, nikamwendea konda, nikamdanganya kuwa NIMEANZA KU BLEED GHAFLA hivyo wasimamishe gari nikajisetiri, hahahaha, konda kusikia hivyo akamwambia dreva, gari ikasimama nikaenda kwenye hoteli mshenzi mshenzi, nikahariiiiiiishaaaaaa mpaka basi!
Kuna mzee ilikua ni New Force ya mbeya alijistiri humo humo ndani ya Basi, gari ilibidi isimame harufu ilitawala halaf mzee kajikausha tu, nadhani ilikua siku mbaya sana kwa yule mzee.
 
Ila nangurukuru wamezidi sana, nadhani kwasababu wanajiona wapo peke yao katika barabara hiyo. Chakula ni bei juu sana, hata wale wanaouza samaki pale ndani ni bei juu kuliko wale wa nje.
Jamani hata soda take away ya sh 600 wao wanauza 2000? Nilishangaa sana.
 
Kuna wakati unawaza bora bei ibaki hiyo wanayotaka lakini chakula angalau basi kiwe cha moto. Chakula kinapikwa asubuhi unakuja kuuziwa SAA 12 jioni. Sio haki in ujambazi usiotumia silaha

Back
Top Bottom