Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

kuna ka mgahawa kapo chalinze aisee kuna siku nimenunua mishikaki pale nakuja nayo ktk gari imeoza kbsa! bahati mbaya hiyo siku sikuwa ktk akili zangu nikachukua panga (ni sime) nikarudi pale ktk ki mgahawa kile nikamwaga vyakula vyoote pale jikoni nikaondoka zangu sikusema na mtu.
kuna kasema hii chai. nataman siku moja awepo ktk msafara wetu aone waliovurugwa kuliko mimi
 
Mie sili chips safarini, nilishawahi kupatwa na masahibu. Nilitoka Moshi kwenda Dar, tulivyofika Mombo tukaingia kula hoteli inaitwa Liverpool, nikala viwepe na mishikaki. Uwiiiiii yaani hata hatujafika mbali, tumbo likaanza kuuma, mharo unataka kuchomoza.

Nikawaza, nikimwambia konda nataka "kuchimba dawa" atasema hilo zoezi ilikuwa lifanyike hotelini tulipokula. Basi bwana akili ikaja ya ziada, nikamwendea konda, nikamdanganya kuwa NIMEANZA KU BLEED GHAFLA hivyo wasimamishe gari nikajisetiri, hahahaha, konda kusikia hivyo akamwambia dreva, gari ikasimama nikaenda kwenye hoteli mshenzi mshenzi, nikahariiiiiiishaaaaaa mpaka basi!
😄😄😄😄
 
Inawezekana mkuu, lakini sio wote wanaosafiri wanahela sana kumudu gharama yeyote, wengine wanasafiri kwa matatizo.
 
Hawa watu ni wapuuzi sana kwakweli, wanawaona wanasafiri hawana akili.
Kuna ka mgahawa kapo Chalinze aisee kuna siku nimenunua mishikaki pale nakuja nayo ktk gari imeoza kbsa! bahati mbaya hiyo siku sikuwa ktk akili zangu nikachukua panga (ni sime) nikarudi pale ktk ki mgahawa kile nikamwaga vyakula vyoote pale jikoni nikaondoka zangu sikusema na mtu.
 
Siku hizi mikate kila kona................ una safari ya mbali mkate au cake juice yako maji................ na apple huna sababu ya kuhangaika na chochote njiani kula mkate wako na juice aaa maisha yanasonga
Wengine hua wananunua vyakula kama showoff , watu wajue kanunua kuku chipsi na mishkaki, kwahio lazima aende na wakati kwanini ale mkate na wengine age yake wale kuku na chipsi, peer pressure inachangia
 
mimi nafikiri sasa tuchukue matatizo kama changamoto.

badala ya kulalamika kila wakati,ni muda wa kuacha mazoa ya kula kula safarini au kubeba chakula binafsi kama imebidi kula.

mimi huwa nashuka nanyoosha miguu,maana safari kwangu sijawahi ihesabu kama ni kadi ya mwaliko wa sherehe,unakuta mtu anaulizia pilau maharage mgahawani[emoji53][emoji53][emoji53],bro utatuponza njiani tuwe tunasimama muda wote,elewa muda na majukumu uliyonayo kwa wakatu huo,utakula ukifika.

wasusieni,wale wenyewe bebeni vyakula.
 
Wengine hua wananunua vyakula kama showoff , watu wajue kanunua kuku chipsi na mishkaki, kwahio lazima aende na wakati kwanini ale mkate na wengine age yake wale kuku na chipsi, peer pressure inachangia


Kabisa mimi huwa sinunui chochote pale na kama niko na luxury huwa wana toa soda so nikifika pale ni huduma ya kijamii na kujinyoosha kidogo narudi kwenye gari safari inaendelea kama nilitoka asbh sana nakuwa na mkate wangu naweka mayai katikati na peanut butter vipande vinne tosha kabisa soseji mbili wala siongei na na mtu wa chips na nyama mbichi za mbuzi kuku na huwa nachukioa yale mainzi yanavyokuwa pale
 
Nikisafiri huwa nabeba hotpot lenye mixer pilau kidogo,mweupe kidogo,kuku kavu,ng'ombe kavu,majani kidogo,pilipili kwa mbali,maji kubwana soda kubwa ya kopo.
Hilo hotpot linaitwa traveller hotpot lina vyumba kibao na linatunza joto masaa 56 na ni ndogo yani saafi na bei yake ni rafiki.
Nilinunua baada ya kupata shida kama hizo hotel za kitonga kule.
Yani saizi nagharamia kuchimba dawa tu lkn napo natafuta hotpot la kuchimbia dawa.
Wakisema kushuka kwenda kula na kuchimba dawa hotelini mi nashuka na hotpot langu nakaa chemba nafanya yangu nafunga tight.
Hela zenyewe zipo wapi bna.
 
Mie sili chips safarini, nilishawahi kupatwa na masahibu. Nilitoka Moshi kwenda Dar, tulivyofika Mombo tukaingia kula hoteli inaitwa Liverpool, nikala viwepe na mishikaki. Uwiiiiii yaani hata hatujafika mbali, tumbo likaanza kuuma, mharo unataka kuchomoza.

Nikawaza, nikimwambia konda nataka "kuchimba dawa" atasema hilo zoezi ilikuwa lifanyike hotelini tulipokula. Basi bwana akili ikaja ya ziada, nikamwendea konda, nikamdanganya kuwa NIMEANZA KU BLEED GHAFLA hivyo wasimamishe gari nikajisetiri, hahahaha, konda kusikia hivyo akamwambia dreva, gari ikasimama nikaenda kwenye hoteli mshenzi mshenzi, nikahariiiiiiishaaaaaa mpaka basi!
Good😁😁😁
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikikerwa na hili jambo.

Bei ya chakula cha hizi hoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri haiendani na huduma wanayopewa lakini naona mamlaka husika zimekaa kimya. Na hili naomba lisichanganywe na suala la wakulima kujipangia bei, msafiri sio mkulima ni mtu anayekuwa hana option maana pengine amesafiri masaa kumi na mbili au ishirini bila kuonja kitu na analazimishwa anunue chankula kwa bei ya juu. Au anaenda hospitali kupeleka mgonjwa.

Kiuhalisia sahani ya wali nyama ni 1500 - 2000 lakini kwenye hiyo migahawa wali nyama wanauza 5000 - 6000. Mbaya zaidi vile vidada vihudumu vinanyodo utafikiri vinahudumia hoteli ya nyota tano kumbe mgahawa wa barabarani tena kwa wasafiri (ref: nangurukuru). Ukiviambia dada ongeza kidogo basi ili nishibe kanakukata jicho utafirikiri umetoa mawe kumbe umetoa 6000.

Wanaosafiri wengine ni wagonjwa, watu wa vijijini na wengine hawajiwezi kabisa, unapomlazimisha mtu kuwa tutachimba dawa hoteli fulani na kupata chakula hapo ni ukiukwaji wa haki za wasafiri. Kwanini mamlaka wasimoderate na kucontrol hili suala? ikiwezekana sehemu ya kuchimba dawa ijitegemee na sehemu ya kula ijitegemee ili hao watoa huduma wasiwalipishe watu bei kubwa kisa umechimba dawa kwao.

Madereva na makondacta wao huwa hawalipii hiki chakula kwasababu ni deal kwa mwenye hicho kihoteli. hii ni ajabu sana, ndio maana inapelekea hawa madereva wanawapeleka abiria sehemu ambayo mwisho wa siku watalazimika kulipia hata kama hawataki.

Naomba mamlaka husika waaanze na Nangurukuru, Singida, Shinyanga, Morogoro, Alj jazeera na sehemu zingine ambazo mimi sijafanikiwa kupita huko kwasababu inakera sana na ni ukiukwaji wa haki za wasafiri kabisa kuwalazimisha kupata huduma wasipopenda halafu mbaya zaidi kwa bei ya juuu kuliko uhalisia.

Bei ya choo cha kulipia inajulikana ni 300, Bei ya wali maharage inajulikana 1500-200, bei ya wali kuku inajulikana ni 3000-4000, bei ya kile kitake away inajulikana kuwa ni 300. Iweje tutozwe bei zisizoendana na uhalisia?

Wakuu wa nchi wao husafiri na private mara nyingi kwahiyo hii inweza isiwe na mashiko sana kwao, lakini kiuhalisia vyombo vya dola na mamalaka za miji na halimashauri ambako huduma hizi hutolewa inabidi walichukulie serious.

Wakuu Nawasilisha, naomba ndugu zangu tusaidiane kupinga huu unyanyasaji kwa abiria.

Pia soma
Hili swala kweli ni taabu tu maana wengine tunasafiri na pesa ndogo mwisho wa siku balance ya nauli inakuwa kubwa sana ukilinganisha na uhalisia
 
Basi Kama ni soko huria kwanini wasipaki stand tukanunua kwenye hotel nyingi hapo stand. Bado mtoto wa mama kwa namna unavyojibu
Nimezaliwa na mama mzazi kwa hiyo sina cha kupinga hapo, tukirudi kwenye hoja ya Msingi sioni mantiki ya Serikali kupanga bei ya chips au Maandazi, kwamba bei ya andazi iwe 200 chips 1000, ni kichekesho una uhuru wa kununua chakula cha bei unayotaka, usilazimishe pia kuuziwa bei unayotaka ndio maana halisi ya soko huria.
 
Back
Top Bottom