IROKOS
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 10,182
- 7,839
Mkuu hilo jina lumenikumbusha mbali.... Urewedi??
Magufuli amebana sana hela!
Pole mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Magufuli amebana sana hela!
Pole mkuu
Hapa tutarudi enzi za miaka ya 80's, nakumbuka tukiwa tunasafiri na bi-mkubwa basi lazima apike chakula cha safari kwenye kimfuko na naironi then kinatunzwa kwenye kikapu... mzee ukijisikia njaa tu bi-mkubwa nafungua kifuko acha kabisa.
Bei zimepanda sana kwa mgano kaskazini no kati Sh. 7000 na 8000 Rock Hill na wengine.. SUMATRA na wadau wa huduma na haki za wasafiri watusaidie.. Na madereva wa mabasi walazimishwa wasipeleke abiria maeneo ya kwenda kuwafilisi..Kwa muda mrefu nimekuwa nikikerwa na hili jambo.
Bei ya chakula cha hizi hoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri haiendani na huduma wanayopewa lakini naona mamlaka husika zimekaa kimya. Na hili naomba lisichanganywe na suala la wakulima kujipangia bei, msafiri sio mkulima ni mtu anayekuwa hana option maana pengine amesafiri masaa kumi na mbili au ishirini bila kuonja kitu na analazimishwa anunue chankula kwa bei ya juu. Au anaenda hospitali kupeleka mgonjwa.
Kiuhalisia sahani ya wali nyama ni 1500 - 2000 lakini kwenye hiyo migahawa wali nyama wanauza 5000 - 6000. Mbaya zaidi vile vidada vihudumu vinanyodo utafikiri vinahudumia hoteli ya nyota tano kumbe mgahawa wa barabarani tena kwa wasafiri (ref: nangurukuru). Ukiviambia dada ongeza kidogo basi ili nishibe kanakukata jicho utafirikiri umetoa mawe kumbe umetoa 6000.
Wanaosafiri wengine ni wagonjwa, watu wa vijijini na wengine hawajiwezi kabisa, unapomlazimisha mtu kuwa tutachimba dawa hoteli fulani na kupata chakula hapo ni ukiukwaji wa haki za wasafiri. Kwanini mamlaka wasimoderate na kucontrol hili suala? ikiwezekana sehemu ya kuchimba dawa ijitegemee na sehemu ya kula ijitegemee ili hao watoa huduma wasiwalipishe watu bei kubwa kisa umechimba dawa kwao.
Madereva na makondacta wao huwa hawalipii hiki chakula kwasababu ni deal kwa mwenye hicho kihoteli. hii ni ajabu sana, ndio maana inapelekea hawa madereva wanawapeleka abiria sehemu ambayo mwisho wa siku watalazimika kulipia hata kama hawataki.
Naomba mamlaka husika waaanze na Nangurukuru, Singida, Shinyanga, Morogoro, Alj jazeera na sehemu zingine ambazo mimi sijafanikiwa kupita huko kwasababu inakera sana na ni ukiukwaji wa haki za wasafiri kabisa kuwalazimisha kupata huduma wasipopenda halafu mbaya zaidi kwa bei ya juuu kuliko uhalisia.
Bei ya choo cha kulipia inajulikana ni 300, Bei ya wali maharage inajulikana 1500-200, bei ya wali kuku inajulikana ni 3000-4000, bei ya kile kitake away inajulikana kuwa ni 300. Iweje tutozwe bei zisizoendana na uhalisia?
Wakuu wa nchi wao husafiri na private mara nyingi kwahiyo hii inweza isiwe na mashiko sana kwao, lakini kiuhalisia vyombo vya dola na mamalaka za miji na halimashauri ambako huduma hizi hutolewa inabidi walichukulie serious.
Wakuu Nawasilisha, naomba ndugu zangu tusaidiane kupinga huu unyanyasaji kwa abiria.
Pia soma
Bei ya vyakula "Kilimanjaro Fast Food" pale Mombo si rafiki
Siku zote fast food za kula unapokuwa safarini huwa ni bei .....kawaida tu hyo Ova Hiyo kusema siku zote umeitoa wap . ?www.jamiiforums.com
[emoji16][emoji16][emoji16]raia hawakumshambulia kweli?
Halina uhusiano na Magufuli. Zamani mabasi yalikuwa yanasimama stendi na wasafiri wanachagua wale wapi na wale nini. Stendi zilikuwa na hotel nyingi na za bei tofauti. Huu ujinga wa mtu kwenda kujenga hotel porini halafu anapanga na wenye mabasi au madereva wasimame kwenye hotel yake ambayo amepanga bei anayoitaka yeye ni ufisadi. Kunakuwa hamna competition na wenye hotel wananyanyasa wasafiri wanavyotaka kwa sababu hawana jinsi nyingine.Magufuli amebana sana hela!
Pole mkuu
kaka kama mnasafiri ki famiia unaweza kujikuta unateketeza karibia laki nzima kisa eti msosi tu wa njiani.Mimi hata sasa, tukusafiri na familia usiku tunaandaa viazi, ndizi za kukaanga na kuku au nyama, matunda, Juice na maji. Weka kwa foil then ndani ya food container... Cheap, high quality na hakuna kusumbuana....
Mkuu tatizo ni kuwa wasafiri wengine wanakuwa na watoto au wagonjwa au wametoka muda mbaya na hawajala chochote. Suluhisho ni serikali kuingia kati na kulazimisha mabasi yasimame stendi kwa muda mrefu. Wapige marufuku kabisa mabasi kusimama kwenye hotel za vichakani.Kwa kweli inakera sana, safari inakuwa chungu wakati kwa wenzetu safari ni adventure.
Mimi siku hizi tukifika kwenye hizo hoteli sinunui chochote zaidi ya kuvuta sigara na kunyoosha miguu.(Ref.Nangulukulu e.t.c)
mgonjwa ndo ajinyee jaman tena mtu mzima[emoji849]Unaanzaje kumshambulia labda ni mgonjwa... Lakini pia mabus nowadays wana tabia ya hovyo sana eti Bus ikitoka Dar kuchimba dawa ni Morogoro, next Iringa, sasa hawajui kwamba kuna baadhi ya watu ni wagonjwa...
Wengine hua wananunua vyakula kama showoff , watu wajue kanunua kuku chipsi na mishkaki, kwahio lazima aende na wakati kwanini ale mkate na wengine age yake wale kuku na chipsi, peer pressure inachangia
Safari za Mwanza huwa sili kitu. Maana tumbo langu ni dakika tu linadai kutoa kilichoingia. Imesababisha nianze tumia loperamide kila safari ili nisiendechoo hata liume vipi
Unafunga taiti? Subiri kwanza,we ni jinsia ganNikisafiri huwa nabeba hotpot lenye mixer pilau kidogo,mweupe kidogo,kuku kavu,ng'ombe kavu,majani kidogo,pilipili kwa mbali,maji kubwana soda kubwa ya kopo.
Hilo hotpot linaitwa traveller hotpot lina vyumba kibao na linatunza joto masaa 56 na ni ndogo yani saafi na bei yake ni rafiki.
Nilinunua baada ya kupata shida kama hizo hotel za kitonga kule.
Yani saizi nagharamia kuchimba dawa tu lkn napo natafuta hotpot la kuchimbia dawa.
Wakisema kushuka kwenda kula na kuchimba dawa hotelini mi nashuka na hotpot langu nakaa chemba nafanya yangu nafunga tight.
Hela zenyewe zipo wapi bna.
Mkuu vp tena huko ni kukaza acha mawazo potofu.Unafunga taiti? Subiri kwanza,we ni jinsia gan
Kusafiri na msosi tena!???! Hapana. Bora nisile tu safarini.Aiseeee kwenye maisha ukitaka ukwame fanya kitu kwa kuhofia au kujilinganisha na wengine... Nyama buchani 7000 kg, nusu 3500 alfajiri wife anakaanga na ndizi 2 au viazi 4, funga kwa foil weka kwa food container.... Ndizi mtaani 100, embe 300, Azam juice kubwa 3000....
kitu pekee ambacho huwa kinanipa shida kwenye safari ni mkojo tu... na hiyo ni kama tu safari yangu inaanzia sehemu ambako kuna baridi... labda njombe to dar au mbeya to dar...Mie sili chips safarini, nilishawahi kupatwa na masahibu. Nilitoka Moshi kwenda Dar, tulivyofika Mombo tukaingia kula hoteli inaitwa Liverpool, nikala viwepe na mishikaki. Uwiiiiii yaani hata hatujafika mbali, tumbo likaanza kuuma, mharo unataka kuchomoza.
Nikawaza, nikimwambia konda nataka "kuchimba dawa" atasema hilo zoezi ilikuwa lifanyike hotelini tulipokula. Basi bwana akili ikaja ya ziada, nikamwendea konda, nikamdanganya kuwa NIMEANZA KU BLEED GHAFLA hivyo wasimamishe gari nikajisetiri, hahahaha, konda kusikia hivyo akamwambia dreva, gari ikasimama nikaenda kwenye hoteli mshenzi mshenzi, nikahariiiiiiishaaaaaa mpaka basi!
Nimezaliwa na mama mzazi kwa hiyo sina cha kupinga hapo, tukirudi kwenye hoja ya Msingi sioni mantiki ya Serikali kupanga bei ya chips au Maandazi, kwamba bei ya andazi iwe 200 chips 1000, ni kichekesho una uhuru wa kununua chakula cha bei unayotaka, usilazimishe pia kuuziwa bei unayotaka ndio maana halisi ya soko huria.