Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Kuna mgahawa mmoja maeneo ya mayoni asee nilikuwanatoka iringa, msosi kidogo afu umepoa bei sasa kaki yako mkooni asee, anzia hapo mi ni maji na keki na fegi basi
Ingependeza zaidi mtu ale biscut na maji kwa sababu zake binafsi si kwasababu kashindwa kulipia chakula au ni kibovu.
 
Lakini mkuu inabidi tuwaze jinsi ya kutatua hili tatizo. Kama ulozi umetawala basi serikali ichukue hatua maana serikali haina dini na hailogeki.
 
Basi Kama ni soko huria kwanini wasipaki stand tukanunua kwenye hotel nyingi hapo stand. Bado mtoto wa mama kwa namna unavyojibu
Stand tena! Nani atawalipa hela,wakati wakipeleka bus hotelini wanalipwa 30,000 Mpaka 40,000.Kwa kila Trip tena wanalipwa Advance hata laki Tano na kuendelea kisha kila akiingiza bus hesabu inapunguzwa kama Ni 30,000 au 40,000 elfu
kuna kasema hii chai. nataman siku moja awepo ktk msafara wetu aone waliovurugwa kuliko mimi

Wengine hua wananunua vyakula kama showoff , watu wajue kanunua kuku chipsi na mishkaki, kwahio lazima aende na wakati kwanini ale mkate na wengine age yake wale kuku na chipsi, peer pressure inachangia
 
Nlitaka niliandikie Uzi hili nashukuru mkuu umeuleta bei imekuwa ni mateso, sio wote tunasafiri tunaweza kuafford gharama ya namna ile wengine tunasafiri sababu ya matatizo. Garama za hizo hotel ipo juu mno mno
Hotelini Bei lazima iwe juu ili wafidie hela wanazotoa kwa Madereva
 
Stand tena! Nani atawalipa hela,wakati wakipeleka bus hotelini wanalipwa 30,000 Mpaka 40,000.Kwa kila Trip tena wanalipwa Advance hata laki Tano na kuendelea kisha kila akiingiza bus hesabu inapunguzwa kama Ni 30,000 au 40,000 elfu
fresh tunalindana lakini sasa kuwe na huduma nzuri na bei inayoendana na hali ya kimaisha kwa sasa, unakuta chakula elfu 5 yani hata mwenyewe unayetoa ile pesa roho inauma. wasafiri mnaelewa. ukila chakula kina mawili kikuzingue au utoboe, vyakula vimelala tunapashiwa dah kmake! ndo hivyo kama unaweza kutembea na hotpot fanya hivyo vinginevyo hayo ndio maisha ya kila siku barabarani, ukiwa mroho unalishwa hata mbwa kwa pesa yako mwenyewe.
 
Hahaha pole sanaaa[emoji1787]
Mimi hiyo ya kuhara haijawahi kunikuta,ila watu wana moyo
Kule kasuru,uvinza ukienda ,mishkaki inauzwa kwenye stand yenye vumbi na watu wanakula tu
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
sawa kabisa....wengine ndio tunaendesha maisha yetu.....wewe unasafiri kaanga chapati zako na maji jifungashie...soko huria..hulazimishwi kununua.......mbona kwenye mahoteli makubwa bei ni ghali hatusemi....
 
Juzi wakati natoka Kigali tulisimama eneo fulani. Basi kama mnavyojua wanaume wa Dar tunapenda Chips zege. Ile najitosa kutoa oda, mhudumu ananiambia chips zege ni tsh 6000.

Nikabaki kutoa macho badala ya kutoa hela.
 
Ukajikuta mjanja mwenyewe ulivyotuchelewesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…