Mie sili chips safarini, nilishawahi kupatwa na masahibu. Nilitoka Moshi kwenda Dar, tulivyofika Mombo tukaingia kula hoteli inaitwa Liverpool, nikala viwepe na mishikaki. Uwiiiiii yaani hata hatujafika mbali, tumbo likaanza kuuma, mharo unataka kuchomoza.
Nikawaza, nikimwambia konda nataka "kuchimba dawa" atasema hilo zoezi ilikuwa lifanyike hotelini tulipokula. Basi bwana akili ikaja ya ziada, nikamwendea konda, nikamdanganya kuwa NIMEANZA KU BLEED GHAFLA hivyo wasimamishe gari nikajisetiri, hahahaha, konda kusikia hivyo akamwambia dreva, gari ikasimama nikaenda kwenye hoteli mshenzi mshenzi, nikahariiiiiiishaaaaaa mpaka basi!