Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Ndio maana nikiwa Safari, nikifika sehemu hizo nakimbilia kaunta nakamata kvant na Maji madogo bhaaaas! Sio unauziwa kitu Kama hutokuja kula Tena!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi naenda zangu Arusha pale Bagamoyo kabla haujafika Wami gari likapaki tuchimbe dawa kwakua ni asubui kiherehere changu si nkasema ngoja ninunue chai na samusa 2 asee na vile nlikua na dogo eti vikombe viwili chai ya maziwa 4000 ikaenda samusa 4 napo elfu 4000 ikaenda ***** sitarudia tena kakikombe kadogo ivi elfu 2

View attachment 1296370
 
Kiuhalisia sahani ya wali nyama ni 1500 - 2000 lakini kwenye hiyo migahawa wali nyama wanauza 5000 - 6000. Mbaya zaidi vile vidada vihudumu vinanyodo utafikiri vinahudumia hoteli ya nyota tano kumbe mgahawa wa barabarani tena kwa wasafiri (ref: nangurukuru). Ukiviambia dada ongeza kidogo basi ili nishibe kanakukata jicho utafirikiri umetoa mawe kumbe umetoa 6000.
Sasa kwa kuwakomesha hao wadada na mwenye mgahawa ukisafiri chukua huo wali wako wa buku 2 tia kwenye hotipoti ukufika kwenye huo mgahawa utaweka poti lako juu ya meza na kujisevia mwenye
 
Mm ni muhanga wa bei kubwa za vyakula tunapokuwa safarini. Niliona nipambane nalo kwa staili yangu. Nilinunua chupa ya chai hizi za kisasa za elfu 20. Inatunza vizuri chakula. Usiku kabla ya safari nachemsha chai yangu na nahikisha na nunua mufin cakes hata za buku naweka kwenye container safi. Hapo naweza kuwa natoka musoma hadi dar.... sinunui chochote njiani zaid ya kuchimba dawa. Na maisha yanasonga. Sijawahi kuteswa na safar na sijui kama itatokea
 
Hoja ya msingi hapo ni kuwepo uwezekano wa kupata huduma kwa bei tofautitofauti katika kituo kimoja,

Tatizo wenye hizo hotel hawataki biashara ya chakula karibu na wao.

Dawa, mabasi yote yasimame kwenye vituo (stand) na Abiria wapate chakula kwa kuchagua mtoa huduma anayemtaka, mfano:- Morogoro stand (Msanvu), Dodoma stand (Nanenane), Singida stand, Korogwe stand, NAKADHALIKA NAKADHALIKA.
 
2020 hii, je kuna mabadiriko? Last week nilipita tena nagurukuru ila safari hii nilinunua chai na chapati mbili kwa 1500/=. Kwahiyo kwasasa pesa yangu wataisikia kwenye bomba tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Au mliingia hoteli ya kitalii?
Juzi naenda zangu Arusha pale Bagamoyo kabla haujafika Wami gari likapaki tuchimbe dawa kwakua ni asubui kiherehere changu si nkasema ngoja ninunue chai na samusa 2 asee na vile nlikua na dogo eti vikombe viwili chai ya maziwa 4000 ikaenda samusa 4 napo elfu 4000 ikaenda ***** sitarudia tena kakikombe kadogo ivi elfu 2

View attachment 1296370

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu nyingi hata nchi za jirani mgahawa hotel za Barabarani vyakula bei yake imechangamka,
Ushauri tu kama unaona garama usile njiaani
We kula korosho na biskuti na juice

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna mahoteli kanda ya kati wanaviepe ladha mbaya zaidi hata ya uswahilini ndanindani ila wanakuuzia bei ya Selena . Wanazingua sana jamaa
 
Back
Top Bottom