Bei za Mafuta zapanda kuanzia Septemba 1, 2021

Bei za Mafuta zapanda kuanzia Septemba 1, 2021

watanzania wapole sana wewe pandisha bei kila kitu wao wapo sawa tu . ila ukipandisha bei ya kiingilio ya uwanjani kuona mechi ndio utasikia kelele kila kona au azam na dstv wapandishe bando la kuona mechi watanzania hawalali watalalamika sana

🤣🤣🤣

Ushuru wa magari uko juu mno na makodi mengine + foods kupanda bei lakiniii uwezi ckia wakiilalamikia sana serikali,,, ngoja sasa bundle za kuongea/internet weeeee kama unakumbuka nini kilitokea babaa.
 
Ila hawa jamaa wanaudhi kinoma. Bado nini? Pandisheni na bei za daladala, M/Kasi, Kivuko, Kodi ya Kichwa, Bei za Bia, Maji, Matibabu.. Kila sehemu kabeni tufe tu mfurahi.
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI KUANZIA JUMATANO, TAREHE 1 SEPTEMBA 2021

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 1 Septemba 2021. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-

(a) Bei za rejareja na jumla za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 4 Agosti 2021. Kwa Septemba 2021, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa shilingi 84/Lita (sawa na asilimia 3.47), Shilingi 39/lita (sawa na asilimia 1.74) na Shilingi 18/lita (sawa na asilimia 0.83), mtawalia. Vilevile, ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa shilingi 83.84/Lita (sawa na asilimia 3.65), Shilingi 39.05/lita (sawa na asilimia 1.84) na Shilingi 18.05/lita (sawa na asilimia 0.88), mtawalia.

(b) Kwa mwezi Septemba 2021, bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya Petroli na Dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa tarehe 4 Agosti 2021. Kwa mwezi Septemba 2021, bei za rejareja za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa shilingi 53/lita (sawa na asilimia 2.13) na shilingi 14/lita (sawa na asilimia 0.59), mtawalia. Vilevile, ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa shilingi 52.81/lita (sawa na asilimia 2.24) na shilingi 13.60/lita (sawa na asilimia 0.62) mtawalia. Kutokana na kuisha kwa mafuta ya taa kwenye maghala ya mafuta yaliyopo Tanga, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka Dar es Salaam. Hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo imekokotolewa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

(c) Kwa Septemba 2021, bei za rejareja na jumla kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa Mikoa ya Kusini (Mtwara, Lindi, and Ruvuma) zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa tarehe 4 Agosti 2021. Kwa mwezi Septemba 2021, bei za rejareja za petroli na dizeli zimeongezeka kwa Shilingi 108/lita (sawa na asilimia 4.50) na Shilingi 49/lita (sawa na asilimia 2.15), mtawalia. Vilevile, ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za petroli na dizeli zimeongezeka kwa Shilingi 108.10/lita (sawa na asilimia 4.74) na shilingi 48.73/lita (sawa na asilimia 2.27), mtawalia. Kutokana na kutokuwepo kwa mafuta ya taa kwenye maghala ya mafuta yaliyopo Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka Dar es Salaam. Hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo imekokotolewa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

d) Mabadiliko haya ya bei yanachangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta (BPS Premium).

(e) EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za mafuta kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

(f) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(g) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na kanuni (formula) iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapishwa katika Gazeti la Serikali Na. 656 la tarehe 21 Agosti 2020.

(h) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

(i) Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.
Ngoja tusubiri na mwezi October, ila naona tumepiga u turn ya hatari, very soon tutakua kama Zimbabwe
 
Badala waweke bei kila m2 aelewe,,,sasa ayo mashilingi na asilimia yana2changanya.

Mleta mada lita moja ya peteroli bei gani??? Dizeli bei gani???
SAVE_20210831_234831.jpg
 
Huyu mama nchi ishamshinda yaani ameshindwa kabisa kuzibiti mfumuko wa bei, napata mashaka na timu ya washauri alionao…

Halafu napata shida sana kumuelewa huyu Mama yetu, kwenye mambo mazito yanayogusa raia wake hutomsikia akikemea au akisema jambo, ila kwenye mambo ambayo hayana tija kwa taifa utamuona yuko mbele kwa mbele mfano ni hili la kuwa zanzibar akirekodi kipindi cha Royal tourism ili hali vitu vinapanda kila kukicha…
Sasahv ni aibu hata kumuita mama. Hastahili heshima
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei za mafuta kuongezeka kutokana na kubadilika kwa bei katika Soko la Dunia na gharama za uagizaji.

Mabadiliko ya bei hizo yanaanza kutumika kuanzia leo Jumanne Septemba Mosi, 2021
IMG_20210901_062454.jpg
IMG_20210901_062451.jpg
IMG_20210901_062448.jpg
IMG_20210901_062444.jpg
 
Eti kwenye soko la dunia!..

Fungeni mikanda watz! Mambo bado!

Magufuli pamoja na kutukanwa kote kwamba ni dikiteta lakini hakukuwa na ujinga wa namna hii!

Sikumbuki kama kuna kipindi mafuta yaliwahi kufika 2500 katika utawala wake.
 
Back
Top Bottom